Fahamu madhara ya kiafya wakati unapotumia sukari nyingi kwenye vyakula

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Sote tunajua sukari ni tamu na ni miongoni mwa bidhaa zinazotumika kwa wingi kila siku katika nyumba zetu. Lakini licha ya umuhimu wake, sukari ni hatari kwa ustawi wa afya wakati inapotumiwa kwa wingi kupita kiasi.

Kwa kawaida kiwango cha sukari tunachotakiwa kutumia katika vinywaji vyetu, iwe chai, juisi, na vinginevyo, ni kiasi kidogo sana, ila kwa upande mwingine, unapoweka sukari kiasi kidogo, ladha ya kinywaji au chakula hicho huonekana ni kama haijakamilika vyema.

Tafiti mbalimbali duniani zimeonyesha kwamba ulaji wa sukari kupita kiasi umehusianishwa na saratani ya tumbo, utumbo mpana na saratani ya shingo ya uzazi, kwa hiyo ni muhimu kutumia sukari kwa kiasi ambacho si zaidi ya vijiko (teaspoons) 9 kwa mwanaume na 6 kwa mwanamke kwa siku.

Mazoea yanaonyesha kuwa watu wengi huweka vijiko vitatu hadi vinne vya sukari kwenye kikombe kimoja cha chai wastani kama kiwango chao cha kawaida. Kiwango hicho hakika ni kingi mara nne ya kile kinachokubalika kiafya.

Kikombe wastani cha chai huhitaji kijiko kidogo kisichozidi kimoja na hata ikiwezekana pungufu ya hapo. Pia unashauriwa kujiepusha sana na unywaji wa vinywaji, kama juisi na soda ambavyo huongezewa sukari ya ziada.
 
Back
Top Bottom