Fahamu kuhusu Uume Kuvunjika (Penile Fracture)

Fahamu kuhusu Uume Kuvunjika (Penile Fracture)

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,564
Reaction score
7,324
Leo wanajamiiforum tuzungumzie kuvunjika kwa Uume "Mbolo" ambayo kitaalamu uitwa Penile fracture hii hali uwa ni yenye kuhitaji Matibabu ya dharula au haraka yani ni medical emergency 🚨— ingawa ya jina hilo, lakini hakuna Mfupa ndani ya uume. Hii hali inaweza kukutokea ukiwa unaichapa au huko faragha na ukichukulia poa na usijue nini cha kufanya, kumbe inaweza kukuletea madhara hapo badae.

Je ni hali gani?​

Kuvunjika kwa Uume utokea pale tunica albuginea (nyama ngumu inayozunguka sehemu za ndani ya Uume) inapochanika wakati Uume umesimama au kudinda. Nyama hii uchanika na kupelekea uume kukosa uwezo wa kusimama kidete kuhimili mapambano ukiwa faragha.

Visababishi​

  • Kufanya Mapenzi kwa vurugu, kasi au kwa nguvu (Hiki ndio kisababishi kikuu). Wewe unaichapa kwa kukomoa au kwa sifa unaona ndio ujanja mwisho wa siku uume unavunjika
  • Kukunjika kwa ghafla kwa uume uliosimama. Hii inaweza kutokea wakati wa kujamiiana kwa bahati mbaya mwanamke akakalia uume kupelekea kuvunjika, au mwanaume mwenyewe anaweza kuisukuma vibaya na kupelekea kukunjika na kuvunjika.
  • Kujichua kwa nguvu au kwa purukushani. Wale wazee wa puchu au kujichukulia sheria mkononi unaweza kufanya masterbation kwa nguvu sana au kasi kwa kubinya kwa nguvu ukavunja uume bila kujua
  • Kuulalia uume uliosimama wakati umesinzia au umelaliwa. Hii utokea labda umelala na ukapata hali ya uume kusimama alafu gafla ukajigeuza na kulalia uume na kupelekea kuuvunja

Dalili kuu​

Watu wengi ambao wamekumbana na hali hii usema:

  • Kusikia mlio wa kitu kupasuka au kuchanika
  • Maumivu ya ghafla baada ya kuuvunja
  • Kushindwa kusimamisha uume ndani ya muda mfupi
  • Kuvimba na michubuko (Uume unaweza kuwa na rangi ya zambarau — “ulemavu wenye kufanana na biringanya” 🍆)
  • Uume uonekana uliopinda au kukunjika
  • Damu kwenye tundu la uume au Kushindwa kukojoa (inadhihirisha mrija wa mkojo umepata shida — hatari zaidi)

Kwa nini ni hatari​

Kama haitatibiwa haraka, inaweza kusababisha:

  • Tatizo la kudumu la Kushindwa kusimamisha uume au kudinda
  • Maumivu makali wakati wa kusimamisha uume
  • Uume uliopinda (Kama ulemavu)
  • Matatizo ya kupitisha mkojo

Tiba (Muhimu Zaidi)​

Upasuaji wa haraka wa kurekebisha uume ndio jawabu la moja kwa moja

  • Matokeo uwa mazuri kama utawai tiba ndani ya masaa 24

Nini cha kufanya​

👉 Wai hospitalini mapema kwenye huduma ya dharula
👉 usijaribu kusubiria
👉 usijaribu kuifanyia masaji au kuinyoosha
 
Ifike wakati tuwe na staha. Leo BBC imetoa ripoti ya kutisha na kusikitisha ya mauaji ya kikatili ya watanzania wenzetu kutoka serya CCM.

Siyo wakati wa kuleta mada za miti na mijolobe kuvunjika.

Huu ni wakati wa huzuni.

Kuweni na huruma. Tunzeni hizi mada hadi tutakapolikomboa taifa.

adriz de mbusii
Kwamba unataka wote humu tuzungumzie BBC, kati ya ripoti ya BBC na Elimu ya afya kuhusu mwili wako kipi ni cha muhimu.

Nyie ndio mnafanya nchi iwe na mazezeta wengi. Unalikomboaje Taifa kwa ripoti ya BBC ambayo inasahaulika baada ya siku mbili tu. Kwani ni mara ya kwanza BBC kuandika ripoti mbaya kuhusu Tanzania?

Alafu sio kila mtu ni mtu wa siasa humu, siasa tunazifanya kama tunaona kuna umuhimu wa kuzifanya kwa wakati muafaka... na sio kila muda tu kupingana pingana na mambo ya siasa au serikali.
 
Ifike wakati tuwe na staha. Leo BBC imetoa ripoti ya kutisha na kusikitisha ya mauaji ya kikatili ya watanzania wenzetu kutoka serikali ya CCM.

Siyo wakati wa kuleta mada za miti na mijolobe kuvunjika.

Huu ni wakati wa huzuni.

Kuweni na huruma. Tunzeni hizi mada hadi tutakapolikomboa taifa.

adriz de mbusii
1. Anzisha uzi kuhusu hao vibaka na wezi waliokula misumari, watu watakuja huko kujadili

2. Hatuwez kujadili vifo vya vibaka throughout the year

3. Alichokiweka mtoa mada kinaihusu jamii na ametoa msaada mkubwa kwa jamii

4. Hatufanani kama mayai, usilazimishe mawazo yako yawe yake

5. Hatuwezi kupoteza muda kuwajadili vibaka waliokufa kama vile wengne hatutakufa (wote tutakufa)

7. Nenda huko tecdema mkajadili huo ujinga wenu ambao hauna jipya

8. Hili ni jukwaa la kila aina ya mawazo, usipangie watu wajadili au wasome nini
 
Asili ya Missionary style ni nini
The missionary position or man-on-top position is a sex position in which, generally, a woman lies on her back and spreads her legs and a man lies on top of her.
It allegedly stems from reports that Western Christian missionaries in the 19th and early 20th centuries promoted this face-to-face, man-on-top position as the only moral or "civilized" method of intercourse to indigenous populations.
 
1. Anzisha uzi kuhusu hao vibaka na wezi waliokula misumari, watu watakuja huko kujadili

2. Hatuwez kujadili vifo vya vibaka throughout the year

3. Alichokiweka mtoa mada kinaihusu jamii na ametoa msaada mkubwa kwa jamii

4. Hatufanani kama mayai, usilazimishe mawazo yako yawe yake

5. Hatuwezi kupoteza muda kuwajadili vibaka waliokufa kama vile wengne hatutakufa (wote tutakufa)

7. Nenda huko tecdema mkajadili huo ujinga wenu ambao hauna jipya

8. Hili ni jukwaa la kila aina ya mawazo, usipangie watu wajadili au wasome nini
SAYNGAY
 
Kwamba unataka wote humu tuzungumzie BBC, kati ya ripoti ya BBC na Elimu ya afya kuhusu mwili wako kipi ni cha muhimu.

Nyie ndio mnafanya nchi iwe na mazezeta wengi. Unalikomboaje Taifa kwa ripoti ya BBC ambayo inasahaulika baada ya siku mbili tu. Kwani ni mara ya kwanza BBC kuandika ripoti mbaya kuhusu Tanzania?

Alafu sio kila mtu ni mtu wa siasa humu, siasa tunazifanya kama tunaona kuna umuhimu wa kuzifanya kwa wakati muafaka... na sio kila muda tu kupingana pingana na mambo ya siasa au serikali.
Brother watu hao ni wakuwaonea huruma kabisa.
Wengi wao ni majob less, wapo mitandaoni kutukana viongozi na watu wote walio fanikiwa kimaisha.
Binafs huwa nawaita wapumbavu.
 
Brother watu hao ni wakuwaonea huruma kabisa.
Wengi wao ni majob less, wapo mitandaoni kutukana viongozi na watu wote walio fanikiwa kimaisha.
Binafs huwa nawaita wapumbavu.
Kabisa
 
Ukifika hospital unawekewa POP bandage au zile antenna utachagua wewe 🤪
Anyway inatisha sana, don't try this at home😆😆😆
 
Back
Top Bottom