Fahamu kuhusu mende

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Je wajua?

Inatajwa kuwa Mende walikuwepo duniani miaka milioni 120 iliyopita, kabla ya wanyama wakubwa kama vile Dinosaurs na bado hajawahi kupotea. Mende ni mdudu anayetajwa kuwa anauwezo wa kuishi siku 3 akiwa amekatwa kichwa, anaweza kutembea na kuhisi kama mbele kuna hatari.

Kuna vitu ambavyo vinamfanya Mende aishi akiwa hana kichwa, sababu kubwa ni kutokuwa na "Moyo" ambapo kazi kubwa ya moyo ni kusukuma damu mwilini.

Hivyo Mende hana damu kama ilivyo pia kwa Nzi ambaye pia anauwezo huo wa kuishi akiwa hana kichwa. Na anakuwa na uelekeo mzuri zaidi akiwa anapaa tofauti na akiwa na kichwa.

Pia ni mdudu msafi sana, akiguswa na binadamu huenda kujisafisha anaamini amechafuliwa, hukaa miezi hata 3 bila kula wala kunywa

NB:- Kuamini haya inakupasa ufanye majaribio kwa viumbe hivyo.

Credit @biturojr
IMG_20201109_094408.jpg
 
Hawana adabu. Unajua kuna maeneo ndani ya nyumba ukikuta mende unaiambia akili kuwa "Kwa huko alipochagua kuishi sina shida naye"

Baada ya muda anakua kiburi yaani kama vile anachangia kodi vile so utakua umeleta 'ugeni' akili yako inachakata ni kivipi nauhamishia huu ugeni kitandani bila kuonekana nina uchu kisha kwa pembeni unamuona mende anatembea.

Taratibu kama vile anafanya ukaguzi au anahakikisha mazingira ya chumba yako sawa.

Unajaribu kumfurumusha bila kuushtua 'ugeni' wako na yeye hakimbilii alipotokea ila anaenda uelekeo wa 'ugeni' wako ulipo. Ugeni unashtushwa mno na uwepo wa huyu roommate wako anakimbilia kitandani.

Unageuka na kumpa mkono mende wako kwa kukurahisishia kazi na kumnong'oneza "Leo usipike narudi na dinner"
 
Miaka 120 millioni. Chukulia idadi yetu watanzania tangu tumepata uhuru hadi sasa. miaka kama 60 tu. angalia hilo ongezeko la miaka 60. halafu uchukue miaka milioni 1 tu ijayo tutakuwa wangapi
Hii dunia haijafikisha hiyo miaka
 
Kuna binti mrembo nilimtongoza, akanambia ananipenda pia ila ananiogopa kwa sababu mimi"ni mende" hee mimi mende kivipi tena

Sasa nikashindwa kumuelewa, ila kwa uzi huu sasa nimeelewa ,kumbe mimi ni msafi sana na naweza ishi bila kula wala kunywa kwa siku tatu
Hebu jaribu kutoa kichwa halafu usile siku tatu nasubiri mrejesho
 
Kuna binti mrembo nilimtongoza, akanambia ananipenda pia ila ananiogopa kwa sababu mimi"ni mende" hee mimi mende kivipi tena

Sasa nikashindwa kumuelewa, ila kwa uzi huu sasa nimeelewa ,kumbe mimi ni msafi sana na naweza ishi bila kula wala kunywa kwa siku tatu
Duh nimeamini sasa Uchaguzi umeisha na maisha yaendelee,
mm nauliza tu hawa mende watafungulia lini mitandao yetu, tumjibu hata Trump basi
lkn hata wewe walikuita mende hawa Dada zetu wako nusu, wakikuita basha pambana
 
Kuna binti mrembo nilimtongoza, akanambia ananipenda pia ila ananiogopa kwa sababu mimi"ni mende" hee mimi mende kivipi tena

Sasa nikashindwa kumuelewa, ila kwa uzi huu sasa nimeelewa ,kumbe mimi ni msafi sana na naweza ishi bila kula wala kunywa kwa siku tatu
Hhaahh pengne alimaanisha tofaut mkuu
 
Huyo ni mende wa chooni, yaani huwa anakula n'nyaa, sasa anawezaje kuwa msafi???.

Kama ungesema nyuki ningekuelewa.
 
Back
Top Bottom