FAHAMU KABILA LA OVAHIMBA

FAHAMU KABILA LA OVAHIMBA

kax bedui Jr

Senior Member
Joined
Aug 11, 2015
Posts
134
Reaction score
96
Kabila la 'Ovahimba' ambalo mgeni wa kiume hukaribishwa kwa kufanya mapenzi....
Wakati dunia nzima ikipambana kuzuia ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya ngono kama UKIMWI, Kaswende, Gonorea na magonjwa mengine yanayoshabihiana, hii ni tofauti kabisa na kabila la OVAHIMBA ambalo hadi karne hii ya 21 bado wanatamaduni hatari kwa afya zao.
Kabila la OVAHIMBA ambalo linapatikana kaskazini mwa Namibia katika mikoa ya Kunene na Omusati, bado wanautamaduni wa kuwapokea au kuwakaribisha wageni wa kiume kwa kufanya mapenzi wakiamini kuwa hiyo ndiyo heshima anayostahiri mgeni.
Imeelezwa kuwa mgeni anapowasili kwa siku ya kwanza kama ilivyokawaida huandaliwa chumba na kisha kumteua mwanamke/binti ambaye hajaolewa kwenye familia kulala na mgeni kitanda kimoja kwa siku ya kwanza.
Na kama kwenye familia aliyofikia mgeni hakuna mwanamke ambaye hajaolewa basi wanaume kwenye familia hiyo hupiga kura ili mmoja wao kumuachia mgeni chumba chake alale na mkewe.
Kama mwanaume huyo nyumba yake itakuwa na chumba kimoja na sebule basi atamuachia mkewe alale na mgeni chumbani kwake.
Kwa maelezo ya makala iliyochapishwa na mtandao wa shirika la habari la AP, imeelezwa kuwa wanawake huwa hawana njia ya kukataa maamuzi hivyo moja kwa moja hutii maamuzi ya wanaume kwenye jamii yao.
Kwa wageni wa kike hao huachwa walale na watoto na huwa hawafanyiwi chochote.
Kabila hilo ambalo linaamini mpaka sasa kifo kama wanavyoita wenyewe ‘Omtiti’ husababishwa na wachawi kwenye jamii hizi.
Asubuhi mwanamke ambaye amelala na mgeni hukaguliwa kama alishiriki tendo la ndoa na kama hakushiriki huongezewa usiku mwingine.
Kabila la Ovahimba wanaamini kuwa mwanaume yeyote hutembea na bahati, hivyo kwa kulala na mwanamke aliyekwenye familia yao huongeza bahati.
Kwa sensa ya mwaka 2010 kabila hilo lilikuwa na watu 50,000 na tayari serikali nchini Namibia imepanga namna ya kuiokoa jamii hiyo ya wafugaji ambayo inaishi karibia na jangwa la Namib.
Kwa upande mwingine kabila hilo wasichana huchaguliwa na baba zao wanaume wa kuwaoa na mahari huwa ni ng’ombe na asali.View attachment 840513
IMG_20180818_185248_333.jpg
View attachment 840514

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimepata kusikia hata hapa kwetu TZ kuna kabila moja kutoka mkoa mmoja wa kaskazini-mashariki hapo zamani walikuwa wakitekeleza mila ya aina hiyo.

Hiyo ni zinaa kabisa. Na bila shaka ustaarabu bado haujapiga hodi na hii ni jukumu la serikali yao kuhakikisha hao jamaa wanachangamana na jamii zingine wapate kuona mambo mapya na
mtazamo mpya (the new mind set) kwa ajili ya kuwanusuru.
 
Mimi nimepata kusikia hata hapa kwetu TZ kuna kabila moja kutoka mkoa mmoja wa kaskazini-mashariki hapo zamani walikuwa wakitekeleza mila ya aina hiyo.

Hiyo ni zinaa kabisa. Na bila shaka ustaarabu bado haujapiga hodi na hii ni jukumu la serikali yao kuhakikisha hao jamaa wanachangamana na jamii zingine wapate kuona mambo mapya na
mtazamo mpya (the new mind set) kwa ajili ya kuwanusuru.


kuwanusuru vipi sasa?? kwa hiyo watu wanavyofanya mapenzi inakuuma nini.....?? una u CCM ndani yako watu wanapata papuchi za bure we unaumia dhhuuu wewe ndo unusuriwe
 
Back
Top Bottom