Matamshi ya Chuki na jinsi ya kukabiliana nayo

copy_of_notohate_-_say_no_to_hate_speech_1600_x_900_px.png


Matamshi ya chuki yaweza kuwa maneno au vitendo vinavyoonyesha hisia za uadui, dhihaka, au kutokuwajali kuelekea mtu au kundi fulani. Yanaweza kujitokeza kwa misingi ya tofauti za kijamii, kitamaduni, kidini, kisiasa, au mambo mengine. Chuki inafarakanisha makundi, huchangia vurugu na migogoro, na hudhoofisha jitihada zetu zote za amani, utulivu na maendeleo endelevu.

Hata hivyo, sasa ukubwa na athari yake umesambazwa zaidi na teknolojia mpya za mawasiliano ambayo sasa yanawafikia watu wengi sana kwa haraka sana.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anasema "Tunahitaji kuchukulia hotuba za chuki kama tunavyochukulia vitendo vyovyote vibaya: kwa kuzilaani, kutoziendeleza, kukabiliana nazo na ukweli na kuchagiza wanaozitekeleza kubadili tabia. Na ni baya kwamba hatuwezi kufanya jambo hili peke yetu, tunategemea msaada wa serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na nyie vyombo vya Habari kwa sababu kukabiliana na sumu ya chuki ni wajibu wa kila mtu.”

Namna ya kupambana/kuzuia matamshi ya chuki

Sitisha/Acha kusambaza
Ni vizuri wewe mwenyewe ukachukua hatua ya kuacha kuzalisha maoni yoyote ya chuki/au kupeleka maudhui kama hayo iwe mtandaoni au nje ya mtandao. Mabadiliko haya ya kuibadili jamii juu ya matamshi ya chuki inapaswa ianze na wewe, hivyo sisi sote tunapaswa kuchukua jukumu la kusitisha kuenea kwa chuki na habari potofu.

Hakiki taarifa kabla ya kuiamini
Siyo kila taarifa unayokutana nayo unatakiwa kuiamini, tuwe na desturi ya kuhakiki taarifa yoyote ili kupata ukweli. Ili kugundua habari potofu na upendeleo, ikiwa ni pamoja na propaganda ya chuki, hakikisha kuchunguza chanzo cha maudhui kupitia zana za utafutaji na uhakiki wa taarifa, na vyanzo vingine vya kuaminika.

Kuelimisha na kujenga uelewa
Ni vizuri ukajenga mazoea ya kuielimisha na kuijengea uelewa jamii inayokuzunguka mtandaoni au nje ya mtandao juu ya athari zinazoweza kutokana na matamshi ya chuki. Athari zinazoweza kutokana na matamshi ya chuki zinaweza kuwa za kijamii, kiuchumi, kidemokrasia n.k

Ripoti na zuia maudhui ya chuki
Jenga mazoea ya kuripoti kwa bidii maudhui ya chuki endapo umekutana nayo ili kuzuia kusambaa. Kwa kufanya hivyo, unachangia kujenga nafasi salama mtandaoni na kuzuia kuenea kwa ujumbe wenye madhara. Mitandao mingi ya kijamii imeweka sheria na kanuni na miongozo ya kushiriki mijadala kuhakikisha maoni ya wanachama yanakuwa ya heshima, pia imeweka nyenzo ambayo ni rahisi kuripoti maudhui ya chuki kwa wasimamizi.

Ibua/dhihirisha ukweli
Endapo umekutana na mada za chuki, unaweza kutumia njia ya kuibua na kudhihirisha ukweli wa jambo lile ili kudhoofisha ujumbe wa chuki uliokuwa umetumwa.

Mwisho, Ni muhimu kujenga uelewa na kukuza mazungumzo yenye heshima ili kuepuka matamshi ya chuki na kujenga jamii inayoheshimu tofauti na inayothamini ushirikiano na amani, hivyo hatua zote zinazotakiwa kushughulikia na kukabiliana na hotuba za chuki zinapaswa kuwa endelevu ili ubadilisha mitazamo na kukuza jamii yenye uelewa zaidi.
 
Nawashauri mfungue thread maalum ya kuwaanika wote wanaofungua nyuzi zenye maudhui za chuki.

Manake kuna nyuzi zingine zinapita Content Management Systems kwa sababu wanaorusha nyuzi hizo wanajua namna ya ku cirumvent.

Itoshe, inawezekana kabisa kwamba baadhi ya content moderarors wanaachia nyuzi hizo, aidha kwa makusudi, kwa kutotambua, au kwa kufumbia macho kwa sababu tu, na labda Jamii zao ndizo zinazofaidika na maudhui hayo.

Unakuta nyuzi imeanza kwa lugha nzuri lakini baada ya bandiko mbili tatu, ndio unakuta maudhui maalum yaliyokusudiwa yakiwa yamejaa chuki yakitamalaki.

Hivyo basi,kwa wale ambao tuna uzoefu wa kutambua lugha, maudhui, magenge, yaani wenye ID zinazofanya hivyo tuwe na sehemu ya kuwabandika wale hapo kwenye thread maalum.

Awali ya yote, nawapongeza kwa kazi nzuri mliyo anza kuionyesha katika kupiga vita Lugha za Chuki.

Amani iwatawale
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom