Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Mnamo mwaka 1995 hivi, palikuwa na uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania. Uchaguzi ule ulikuwa na ushindani. Nyakati hizo, runinga ndio zinaingia Tanzania-bara. Palikuwa ni kipindi kimoja cha mahojiano, kilijipatia umashuhuri sana. Kilikuwa kinaitwa "Kiti Moto". Mtangazaji, Pascal Mayalla , runinga ya DTV.
Wakati huohuo, walaji wa nyama-choma ya nguruwe walikuwa wakikutanika katika maeneo yao ya kujidai, na kujipatia kitoweo, huku wakiendeleza mijadala motomoto ya mwaka wa uchaguzi. Kuonyesha namna mijadala yao ilivyokuwa muhimu, waliita mikutaniko yao "Kiti Moto", jina ambalo lilipitia transmutation na kuwa kitimoto.
Jina la kitimoto likafunika majina mengine ya zamani, kama vile mbuzi-katoliki au Mkuu wa Meza.
Historia kwa manufaa ya vijana wa leo.