Facts za wadada wenye ajira nzuri

Facts za wadada wenye ajira nzuri

Jeuri iko wapi, mambo yamebadilika nakupa ukweli uliopo tu.
Kinachowasumbua wanaume wengi ni kwamba unataka mwanamke awe kama mwanao unamtuma, unamkaripia, unampiga na unamtisha anatetereka... Ni sawa maandiko yanaagiza wanawake wawaheshimu waume zao wengi wanafanya hivyo na Wapo waliovumilia sana wakafika mahali wakachoka maana akili za wanaume wengi hasa wa kiafrika ni kwamba wao wajuaji wa kila kitu wanasahau na wanawake wana akili tena sana tu. Na mwanamke huwa anareact kutokana na unavyo-mtreat vinginevyo ni tabia yake tu.
Kuna wanawake bahati mbaya wameolewa na wanaume wapumbavu (kama nabali ktk biblia,stori ya Daudi) hawa wanawatetea waume zao na kuwafichia aibu lkn wanaume huwatesa ili kijitutumua kwamba wako juu. Mwanaume mwenye akili hatishiki na mafanikio ya mkewe, anajua kuna siku atasaidiwa, asilimia kubwa pesa ya mwanamke inatumika katika familia ataona vyombo atanunua n.k wakati baba analewa na kuhonga.
Ni vema muoe wanawake wa hadhi zenu na wanaowapenda, wanawake wenye mafanikio waachieni wanaume wenye akili.
Mkeo ni partner katika maendeleo ya familia sio mtumwa wala dobi, anatafuta hela ndo maana yuko bize. Tafuta msaidizi wa ndani au saidia kuziba gepu unaloona katika familia ikiwemo kusaidia kufua.
Hizi ni zama mpya, isaidie familia kwa kuipa mama mwenye kipato kizuri.
Uanaume wako uonekane katika matunzo na malezi bora ya familia.
Ukioa wanawake ma feminist ninyi ni sawa na kuwa na wanaume wawili ndani ya nyumba.Huwa amumbiwi wala kusikia ninyi.
 
Ndo Maana Mm Ctaki kuoa tuu.. Ndoa cku hizi karaha tupu.
Sio zote ni karahaa kuna ambao wanaishi kwa raha. Cha muhimu unapochagua mke kuwa makini sana..
Unaweza oa ukakosa rahaa maisha yako yote na unaweza kuwa na furaha isiyokifani.
Siku zote penye miti hapana wajenzi....
 
Naona ume generalise sana, mwanamke mlieoana kwa kupendana hawezi kufanya ushenzi kwa makusudi kisa ana kazi
Kama yupo wa hivyo ni hulka yake na wala sio wote
pengine unapenda kuwa boss wa mkeo na wala sio mume,
hivyo ukioa mke asiependa kuwa bossed kila mara unaona sio basi oa asie na kazi umfanye utakavyo, ndoa inatakiwa kuwe na kuheshimiana pande zote mbili
Sasa kama unataka umpelekeshe mtu utakavyo kisa hawezi kuji take care of, oa wasio jiweza, na siku wakijiweza ndoa inakufa
Ngoja nifanye kautafiti kwa wanaume ambao wake zao ni mawaziri, wakurugenzi au mameneja or may be wakuu wa wilaya, mkoa au hata wabunge. Nitaleta kamrejesho.
 
Mm ninaye huwa akinizingua ni makofi tu na ananijua akikanyaga mlango wa Nyumba yuko mwanaume ambaye hapendi ujinga ujinga
 
Confidence anayo alafu mkigombana kidogo Tuachane hata kama umemzalisha anakwambia nitalea mwenyewe

Na ukimuudhi zaidi atakwambia huyu si mtoto wako...
 
Kimsingi tunapotoka kwenye mstari (njia iliyo sahihi) ni lazima tuharibikiwe, vitabu vyote vya dini vinazungumza mwanamke amtii mume wake hali kadhalika mila zote za kiafrika zinasema hivyo. Pale ambapo mwanamke anadhani kwa kupata mali au elimu anaweza akawa juu ya mume wake, au akafanya maamuzi bila idhini ya mume wake basi hapo ndipo uaharibifu unapoanza. Mwenye enzi Mungu ni mkamilifu, maagizo na makatazo yake ni dawa yetu, tunapofanya kinyume ndiyo tunapojitafutia angamizo letu na kizazi chetu. Kwa mwanamke kuacha kumtii mume wake kinachotokea ni ugomvi usioisha, michepuko, takala, yatima na mwisho ni jamii isiyo na maadili. Hawa wanawake wasio watii waume zao wamekula maharage ya wapi nauliza?
 
Naona ume generalise sana, mwanamke mlieoana kwa kupendana hawezi kufanya ushenzi kwa makusudi kisa ana kazi
Kama yupo wa hivyo ni hulka yake na wala sio wote
pengine unapenda kuwa boss wa mkeo na wala sio mume,
hivyo ukioa mke asiependa kuwa bossed kila mara unaona sio basi oa asie na kazi umfanye utakavyo, ndoa inatakiwa kuwe na kuheshimiana pande zote mbili
Sasa kama unataka umpelekeshe mtu utakavyo kisa hawezi kuji take care of, oa wasio jiweza, na siku wakijiweza ndoa inakufa
Ndoa huwa haina kanuni unaweza ukaoa asiye na kazi pia nae badala ya kumpelekesha akakupelekesha zaidi
 
A weak man can't have a strong woman, he won't know what to do with her . Dawa msiwasomeshe mabinti zenu na mkaoe kijiji wale std seven. Kukaa mnawakandia wanawake wanaofanya kazi na waliopitia shida na majaribu wakafanikiwa katika maisha ni ishara ya udhaifu.
Ukiona huwawezi just know you are not man enough for them, waachie wanaume waoe hawa wanawake wanaojenga taifa.
Mnataka nini hasa, wanaume bwana sasa unataka ukifa au usipokuwepo basi maisha ya familia yasimame.
Mijini hakuna STD VII?
 
Pia wanabutuliwa sana kwenye magari na ze so koldi mabosi wao....
 
Kimsingi tunapotoka kwenye mstari (njia iliyo sahihi) ni lazima tuharibikiwe, vitabu vyote vya dini vinazungumza mwanamke amtii mume wake hali kadhalika mila zote za kiafrika zinasema hivyo. Pale ambapo mwanamke anadhani kwa kupata mali au elimu anaweza akawa juu ya mume wake, au akafanya maamuzi bila idhini ya mume wake basi hapo ndipo uaharibifu unapoanza. Mwenye enzi Mungu ni mkamilifu, maagizo na makatazo yake ni dawa yetu, tunapofanya kinyume ndiyo tunapojitafutia angamizo letu na kizazi chetu. Kwa mwanamke kuacha kumtii mume wake kinachotokea ni ugomvi usioisha, michepuko, takala, yatima na mwisho ni jamii isiyo na maadili. Hawa wanawake wasio watii waume zao wamekula maharage ya wapi nauliza?
Kutii ni jambo lingine na kuwa na mali ni jambo lingine. Ukiona mke hamtii mmewe eti kwa sababu ana mali huyo mke ni limbukeni. Ndio wale wakinunua kanga mpya mtaa mzima unajua.
Kumbuka kuna wanawake hawana kipato ilka ni majeuri hatari, kuishi nae mpaka uwe agressive!
Mme kuwa katika position yako na mke pia kuwa katika position yako.
 
Ukioa wanawake ma feminist ninyi ni sawa na kuwa na wanaume wawili ndani ya nyumba.Huwa amumbiwi wala kusikia ninyi.
Kila mwanaume na mwanamke wake, wengi hawaongei ila wanakubaliana na hoja zangu. Wawe feminists wasiwe femists wanapendwa na waume zao. Wewe kaa unalalamika humu wakati wenzio wanaoa majembe hawana hofu hata wakifukuzwa kazi.
 
1.Wengi wao ni single mothers
2. Wana confidence sana, waliolewa, hawaheshim ndoa, wanajua hata ukimuacha anaweza kuendeleza maisha
3. Wabishi sana wanajiona wanakaribia hadhi ya mume kwenye famila kwa kuwa nae ana kipato
4. Ukiwaoa sio kwamba kila siku utapata haki yako, Mara atakuwa kachoka, Mara kasafiri kikazi, mara kachelewa kurudi kazini nk
5. Wengi wao wanaolewa wakiwa wakubwa, umri umewapita
6. Wana midomo sana sio wasikivu kabisaa
7. Wanaume wengi wenye such wives wana michepuko, either lazma house maid akusaidie
8. Wavivu sana kupika na kufua, na 100% ya watoto wao wanawapenda ma
TOO MUCH JUDGEMENT
 
Hela ni maua hakuna uhakika wa kuwa nazo siku zote iwe ajira au biashara,cha muhimu hapa ni kuheshimiana kila upande.
 
Kutii ni jambo lingine na kuwa na mali ni jambo lingine. Ukiona mke hamtii mmewe eti kwa sababu ana mali huyo mke ni limbukeni. Ndio wale wakinunua kanga mpya mtaa mzima unajua.
Kumbuka kuna wanawake hawana kipato ilka ni majeuri hatari, kuishi nae mpaka uwe agressive!
Mme kuwa katika position yako na mke pia kuwa katika position yako.
That's a point right there, wanaume wanadhani mtu anakuwa mtii akiwa tegemezi kumbe kuna vichwa vimezaliwa vigumu tu.
 
Mbona umepanic sana, pointless kabisa kwahiyo kijijini hakuna wasomi?? std 7 wapo hata mjini, halafu hapo sio wanawake wote ni baadhi yenu ukiwepo na wewe maana si kwa povu hili
Sijapanic wala nini, mwanaume ni mtu tu.
Hujaelewa hoja kwa sababu your ego can't let you take the point and swallow the fact that u are not man enough for a successful woman.
Std seven wa kijijini hafanani na std seven wa mjini, Mjini yuko exposed na anakuwa ana matamanio ya kufanikiwa kuliko wa kijijini... Huyu utamuona ana kiburi, kumbe anataka vitu vizuri na yeye hata kama kaishia std 7.
Wanawake wanafanya vitu kuwasaidia mwanaume wasijisikie wadhaifu, kama mzazi ambavyo anajua akili ya mwanae inavyofanya kazi hivyo anaenda nae tu na kukubali maneno ya mwanae ili asijisikie vibaya.
Na wewe ili ujisikie vizuri, tufanye nimekubaliana na hoja yako
 
Back
Top Bottom