sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 2,568
- 7,430
Watu wengi hawajui historia ya muziki wa bongofleva na hawajui umeanzia wapi.
Fact ni kwamba muasisi wa muziki wa bongofleva ni Prince Dully Sykes aka Mr Misifa.
Sound hii unayoiskia leo ya bongofleva (baibuda) ilianzia kwa Dully.
Kwa wasio na ufahamu, bongofleva ni muziki wa kizazi kipya uliozaliwa Dar es Salaam miaka ya 2000 ukiwa na mchanganyiko wa radha ya mwambao, midundo ya zouk, rhumba, dancehall na chakachaka. Na muasisi wake ni Dully Sykes.
Ni vema hizi facts zikawekwa sawa sababu ya kulinda historia ya bongofleva.
Pia usichanganywe muziki wa bongofleva na aina zingine kama hiphop,reggae, sokousss, RnB, jazz nk
Asanteni!