Fact: Prince Dully Sykes ndio muanzilishi wa muziki wa bongofleva

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,525
7,377
20240301_110345.png

Watu wengi hawajui historia ya muziki wa bongofleva na hawajui umeanzia wapi.

Fact ni kwamba muasisi wa muziki wa bongofleva ni Prince Dully Sykes aka Mr Misifa.

Sound hii unayoiskia leo ya bongofleva (baibuda) ilianzia kwa Dully.

Kwa wasio na ufahamu, bongofleva ni muziki wa kizazi kipya uliozaliwa Dar es Salaam miaka ya 2000 ukiwa na mchanganyiko wa radha ya mwambao, midundo ya zouk, rhumba, dancehall na chakachaka. Na muasisi wake ni Dully Sykes.

Ni vema hizi facts zikawekwa sawa sababu ya kulinda historia ya bongofleva.
Pia usichanganywe muziki wa bongofleva na aina zingine kama hiphop,reggae, sokousss, RnB, jazz nk
Asanteni!
 
Kwani dully si kawakuta Kaka zake kitambo tu??na yeye alikua ansema yeye anaimba style yake inaitwa Mwanasesere??
Zamani hakukua na bongo flavor, Miziki ilikua inatofautishwa kabisa Taarab, Hip hop, R&B etc. Nakumbuka bongo flavor imeanza Enzi za kina Proffesor Jay, Juma Nature, inspector Haroun etc. Wakati Ule kina Hadija kopa na Nasma Hamis kidogo wapo on Top taarabu, Inspector anaimba sijui rap cartoon kukaanza mesh, unakuta Inspector kamshirikisha Nasma, hapo ndio vikaanza vijembe wasanii wanaitwa Wabana Pua.

Hawa Wabana pua ndio waanzilishi wa Bongo flavor, sina Uhakika kama Dully Sykes ni wa kwanza kabisa ila ni katika kundi la mwanzo kabisa la wasanii wa bongo flavor.
 
Pole boss
 
Back
Top Bottom