Joeli
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 4,941
- 3,417
Facebook imefuata mkondo Twitter kwa
kuanzisha akaunti na kurasa zilizothibitishwa (verified pages/
accounts) ili kuwawezesha watu mashuhuri kuthibitisha akaunti akaunti na fan page zao. Facebook wamesema wamefanya hivyo ili kusaidia watumiaji wa Facebook kuzitambua akaunti za kweli za mastaa na watu wengine mashuhuri
wanaotumia mtandao huo, pia ikiwemo
biashara zenye majina makubwa.
Kurasa zilizothibitishwa zitakua na alama ya blue ya pata check-
mark kama inavyoonekana kwenye
picha hapo juu. Watu
wataoruhusiwa kutumia huduma hiyo ni,
viongozi wa serikali, waandishi wa habari
maarufu, makampuni au bidhaa maarufu.
Hivyo kuanzia sasa, utaweza kufahamu
akaunti/pages zipi ni za kweli na zipi ni feki.
Ili mtu mashuhuri kupata akaunti
iliyohakikishwa, mhusika atahitaji kuwasilisha kitambulisho halali kinachotambuliwa kiserikali. Nadhani
celebrities (mastaa) Wengi wa Afrika
wataipenda hii. Kama mfano Wema, kuna
page zaidi ya kumi zinazodai kuwa ni
Wema Sepetu