Facebook yafunga akaunti tatu zinazomilikiwa na raia wa Urusi kutokana na kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Messages
1,497
Points
2,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2012
1,497 2,000
Mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook umeondoa akaunti tatu za mitandao nchini Urusi, kurasa na makundi, kama sehemu ya mkakati wake unoendelea wa kukabiliana na akaunti bandia zinazotumika kuwahadaa watumiaji.

Kampuni ya Facebook imesema kwenye taarifa yake kwamba ingawa watu wanaohusika na mitandao hiyo walijaribu kuficha utambulisho wao na namna wanazivyoratibu kurasa hizo lakini uchunguzi uliofanywa na Facebook umehusisha kampeni za mitandao hiyo na watu wenye mahusiano na mfadhili ambaye ni raia wa Urusi Yevgeniy Prigozhin ambaye huko nyuma aliwahi kushitakiwa na wizara ya sheria ya Marekani.

Prigozhin ni mlengwa muhimu anayeshukiwa kwa kufadhili taasisi ya uchunguzi wa wakala wa utafiti wa intaneti ama Internet Research Agency ambayo ilikuwa na jukumu mahsusi katika mkakati wa Urusi wa kuingilia uchaguzi wa Marekani mnamo mwaka 2016. Prigozhin pia anatajwa kuwa mtu wa karibu wa rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Wizara ya sheria ya Marekani mnamo mwezi Septemba ilisema kwamba kundi la Prigozhin pia lilijaribu kuingilia kwenye chaguzi za katikati ya muhula za mwaka jana, lakini jaribio lake hilo halikufanikiwa.

Kampuni ya Facebook ambayo ni mtandao mkubwa kabisa wa kijamii ulimwenguni tayari umeondoa jumla ya akaunti 66 bandia, kurasa 83 na makundi 11 pamoja na akaunti 12 za mtandao wa Instagram, ukiilenga Madagascar, Jamhuri ya Afrika ya Kati, msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Cote d'Ivore, Cameroon, Sudan na Libya.

Kwa ujumla, akaunti milioni 1.1 zilifuata moja ama kurasa zote miongoni mwa hizo zilizoondolewa huku takriban watu 1,750 walizifuatilia ama kujiunga na moja ya makundi hayo. Zaidi ya watu 32,200 pia wanatajwa kuwa walikuwa wafuasi wa moja ya akaunti hizo za Instagram.

Facebook imesema imegundua mitandao miwili kati ya mitatu ilitumika katika uchunguzi wa ndani dhidi ya watu wenye mahusiano na Urusi walioshukiwa na kile walichokitaja "kuratibu tabia zenye mwelekeo mbaya barani Afrika."

Kugunduliwa kwa matandao wa tatu kulitokana na uchunguzi ulioibuliwa na dokezo lilitosambazwa na shirika la ufuatiliaji kwenye masuala ya intaneti la Stanford Internet Observatory. Kulingana na shirika hilo kila mtandao ulisambaza maudhui kadhaa ambayo ni pamoja na sera za nje za Urusi.

=========

Facebook Removes Russian Networks Targeting African Users
1572529220059.png

Facebook has been forced to take action again to remove illegal Russian attempts to influence its users — this time in African countries.

The “coordinated inauthentic behavior” has been linked to notorious Russian financier Yevgeniy Prigozhin, already indicted by the US for funding the Kremlin-linked Internet Research Agency (IRA), which was involved in information warfare efforts ahead of the 2016 US Presidential election.

Facebook removed three separate networks originating in Russia and which targeted Madagascar, Central African Republic, Mozambique, Democratic Republic of the Congo, Côte d’Ivoire, Cameroon, Sudan and Libya.

The first involved the take-down of 35 Facebook accounts, 53 Pages, seven Groups and five Instagram accounts focusing on users in Madagascar, the Central African Republic, Mozambique, Democratic Republic of the Congo, Côte d’Ivoire and Cameroon.

At least one of the Pages accrued around 475,000 followers, and around $77,000 in advertising was spent.
The next campaign centered around 17 Facebook accounts, 18 Pages, 3 Groups and six Instagram accounts, accruing over 457,000 followers. They re-posed Sudanese state news and Russia propaganda from RT and Sputnik.

Finally, Facebook removed a network of 14 Facebook accounts, 12 Pages, one Group and one Instagram account that originated in Russia and focused on Libya.

As per the other campaigns, they often posted a mix of local and global news from local and Russian sources, on multiple sides of political debate, and from authentic and fake accounts. In this case, the accounts and Pages gained over 241,000 followers and around $10,000 was spent on ads.

“Although the people behind these networks attempted to conceal their identities and coordination, our investigation connected these campaigns to entities associated with Russian financier Yevgeniy Prigozhin, who was previously indicted by the US Justice Department,” said Facebook head of cybersecurity policy, Nathaniel Gleicher.

“We’re taking down these Pages, Groups and accounts based on their behavior, not the content they posted. In each of these cases, the people behind this activity coordinated with one another and used fake accounts to misrepresent themselves, and that was the basis for our acti
on.”

Chanzo: .Infosecurity-magazine
 

Times9

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Messages
1,075
Points
2,000

Times9

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2017
1,075 2,000
Mitandao kama Facebook skuiz tumewaachia 4m4 leaver... Ishakua kama trash tu! Tofauti na kutumia kwa biashara tu kwa kumiliki pages zake...
 

BASIASI

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
8,559
Points
2,000

BASIASI

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
8,559 2,000
Hana jipya fb

Kama aliweza kutoa siriza ndan za acc akaomba radhi anashangaa nn na hao jamaa kufanyayaoo

Fankurumanyiyàfb
 

Forum statistics

Threads 1,391,998
Members 528,520
Posts 34,095,131
Top