F.F.U wametapakaa kila kona ya manispaa ya Iringa Mjini!

Waislam walifanya maandamano Dar nani aliwagusa, halafu maandamano sio sababu, dunia nzima watu wanafanya maandamano na Polisi wanawalinda, ikitokea vurugu wanadhibiti. Inakuaje TZ hata maandamano tu ni marufuku tena yawe ya CDM tu.

mkuu maandamano siku 365! kweli siasa ni ajira, ngenga inamfanya mtu aishi vizuri
 
Ya sensa yamewashinda - kasoro kibao. Wamehamia kuwazuia CHADEMA. Kazi ipo.
 
ccm acheni siasa za maji taka tumeshawaelewa mmejificha kwenye mgogo wa dola lakini nchi haitatawalika hilo mlifahamu mapema
 
Midahalo mnaogopa Mikutano Mnaogopa kuongoza nchi hamuwezi mkienda kwenye majukwaa mnatukana huku mwenyekiti wenu akianguka kwa kisingizio cha Swaumu kinacho wafanya mng'ang'anie ni wizi mnaoufanya ambao muda wake umefika kama kwa kanali mwenzake Gadaffi

daa umempa ukweli akirudi ntajua anaroho ya paka
 
ccm acheni siasa za maji taka tumeshawaelewa mmejificha kwenye mgogo wa dola lakini nchi haitatawalika hilo mlifahamu mapema

Napata wasiwasi na uwezo wako wakufikiri, nchi haitawaliki wakati mambo yanakwenda kama kawaida mkuu ? unasema kutawalika huko ni kwa namna gani ? labda ufafanue tukuelewe kinaga ubaga

 
ccm acheni siasa za maji taka tumeshawaelewa mmejificha kwenye mgogo wa dola lakini nchi haitatawalika hilo mlifahamu mapema

kila penye chadema kuna mauaji.ilianza arusha,ikaenda iramba na sasa morogoro.hii ni laana.
 
Ndio tatizo la kupata uongozi kupitia kwa Sangoma, watu wanapoanza kuomba kwa nguvu juu ya mabadiliko ya nchi yao, matunguli yote yaliyowapatia uongozi yanaungua na moto kinachofuata ni kupanick.

ndio mnavodanganyana huko uchagani na makanisani ili watanzania waichukie serikali yao ee?
 
img_0883.jpg


huwezi
amini kinachoendelea hivi sasa katika viunga vya manispaa ya iringa
mjini, askari wasio na idadi wenye silaha nzito pamoja na magari
yaliyofungwa vitaambaa vyekundu kuashiria hali ya hatari yanarandaranda
kutisha wananchi, aidha wasifanye maandamano, fujo au wasihudhurie
kabisa mkutano wa chadema unaotarajiwa kufanyika uwanja maarufu wa
mwembetogwa.

Hivi sasa niko eneo moja linaitwa kihesa, mbunge wa viti maalumu mh,
chiku abwao amezingirwa na ffu kwenye gari yake, huku mh, msigwa
akikaririwa leo na kituo cha redio cha ebony fm kuwa chama chake
hakitafanya maandamano bali watafanya mkutano wa hadhara kuanzia saa 8
mchana hadi 12 jioni.

Ntaendelea kuwajuza kila linalojiri wakuu.....

hawa ffu ndio wale wanaoishi kwenye mabanda ya mabati na familia zao wanapinga mabadiliko ccm haina hata mpango wa kuwachimbia choo
 
Napata wasiwasi na uwezo wako wakufikiri, nchi haitawaliki wakati mambo yanakwenda kama kawaida mkuu ? unasema kutawalika huko ni kwa namna gani ? labda ufafanue tukuelewe kinaga ubaga

Kwani walikuwa wanatuliza fujo gani?
 
Ya sensa yamewashinda - kasoro kibao. Wamehamia kuwazuia CHADEMA. Kazi ipo.

mie nilikuwa nasikia kuna maswali 62 mbona nimeulizwa maswali matatu tu ...umri wangu na kama ninna cheti cha kuzaliwa hata hajataka kukiona na umesoma kiwngo gani cha elimu?
 
Hayo ndio kama jana walivyofanya Morogoro, wao walipewa kibali cha mkutano, wao wahamasisha maandamano, sasa hapo hawa jamaa wa FFU wakiwafanyia kitu mbaya watalaumu ? cdm ndio chanzo cha mauaji yote


Sio kweli. Wananchi wana haki ya kutemnbea kwa pamoja na kwa hamasa kwenda mkutanoni. Alijaribu Mubarak kuzuia hilo kwa mtutu akashindwa, na sasa anasubiri kunyongwa.

Kuwanyima wananchi haki yao ya kuandamana kwa kuwapiga risasi sio haki, na sio "nguvu za dola" bali ni UNDULI.

Tumeshakuwa na Nduli Idd Amin, na sasa naona wanajitokeza manduli hapa hapa nyumbani. Watanzania watawashinda NDULU MWEMA na NDULI KIKWETE kama walivyomshinda Nduli Idd Amin.
 
Back
Top Bottom