Makamu wa rais dr bilal ashuhudia nguvu ya chadema jimbo la iringa mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu wa rais dr bilal ashuhudia nguvu ya chadema jimbo la iringa mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 4, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  MAKAMU wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilala ashuhudia kifo cha chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa mjini baada ya chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa mjini kuwataka wafuasi wa chama hicho walioshiriki mkutano wa hadhara wa makamu huyo wa Rais kuonyesha itikadi yao dhidi ya Chadema.

  Makamu wa Rais alishuhudia nguvu hiyo ya chadema baada ya mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Iringa mjini na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kutumia jukwaa hilo la Makamu wa Rais kukionya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kwa kujimilikisha ziara za viongozi wa serikali kwa kuweka bendera za CCM na kujipigia debe .
  " Mheshimiwa makamu wa Rais naomba leo nitoe onyo kwa CCM na kuwaonyesha kuwa si vizuri kuteka misafara ya viongozi wa kitaifa wa serikali wanapokuwa katika ziara mkoani hapa...imekuwa ni kawaida ya CCM kutumia majukwaa haya kujipigia debe sasa naomba uniruhusu kuwasalimu wananchi kwa falsafa ya chama changu cha Chadema .....naomba wananchi wote kunjeni ngumi nikisema peoples semeni Power’ " salamu hiyo ilifanya robo tatu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa juzi kulipula kwa sauti kubwa na kujibu salamu hiyo

  Hatua ya mbunge Msigwa kumwonyesha makamu wa Rais nguvu ya Chadema ilitokana na na Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Kapt. Mstaafu Asseri Msangi kumtaka kupanda jukwaani ili awasalimu wananchi wa Manispaa hiyo kama ilivyokuwa kwa wabunge wa CCM
  Baada ya salaam hizo mbunge huyo alimweleza Makamu wa Rais na ujumbe wake kwamba kwa kuwa na yeye (Msigwa) ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Iringa, angeamua kuwaambia wananchi wake wabebe bendera zao au kuvalia kombati za chama chake ingekuwa balaa.

  “Kama na mimi ningewatuma wananchi wangu wabebe bendera au kuvalia mavazi ya chama (Kombati) ingekuwa balaa lakini naomba niwasalimu wananchi wangu kwa salaamu ya chama chetu…’Iringa, Peoplesssss,wananchi wakaitika Power! huku wakinyoosha vidole viwili juu jambo ambalo lilimlazimu Msigwa kuwaambia wananchi hao, nawaombeni sasa, mumsikilize mheshimiwa Makamu wa Rais,”alisema mbunge huyo.

  Hata hivyo CCM kupitia katibu wake wa mkoa Mary Tesha alipanda jukwaani na kutaka kujaribu kuonyesha nguvu ya CCM kwa kusalimia kwa salamu ya CCM na kujibiwa na watu wasio zidi 50 wakiwemo viongozi wa jukwaa kuu huku watu zaidi ya 10000 wakinyamaza kimya na kuzomea . “CCM Oyeee! Mheshimiwa Makamu wa Rais siyo kweli kwamba tumekuwa tukiteka ziara wala kuipora mikutano ya serikali kwa kuweka bendera zetu.
  Hata mheshimiwa mbunge (Msigwa) anajua kwamba Makamu wa Rais amekuja kukagua miradi inayotekelezwa kwa ilani ya CCM,”alisema katibu huyo akijibu kauli iliyotolewa na mbunge wa Iringa mjini (Chadema).

  Hata hivyo,katika hali isiyo ya kawaida wakati mbunge huyo akitumia salaam ya Peoples Power, Dk.Bilali alikuwa mtulivu na hakuonekana kuvurugwa na falsafa hiyo hata wakati alipopanda jukwaani kuwahutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa waliofika kumsikiliza.

  Mbali ya Chadema kuchukizwa na utaratibu huo wa CCM kupeperusha bendera za CCM katika uwanja huo bado Chadema ililazimika kupamba bendera zake kando kando ya barabara ya Kihesa na wakati msafara wa makamu wa Rais uliokuwa na magari zaidi ya 40 ukipita katika eneo hilo kuelekea uwanja wa ndege Nduli ulishuhudia utitiri wa bendera hizo za Chadema .
   
 2. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  viva cdm
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hajaenda kufungua sijui jiwe gani la msingi this time?....all viongozi wa serikali ya kikwete are such a joke!
   
 4. paty

  paty JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,251
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  usinikumbushe ha ha ha ha, hii mara ya pili kwa bilali , mara ya kwanza ilikuwa kampenzi mtogwa pale,
   
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  imetulia.
   
 6. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hadi 2015 watapokelewa na ma RC, ma DAS, DC na maafisa tarafa maana hata hao vioongozi nao wote watakuwa wameupata na wameukubali ujumbe wa ukombozi na kuachana nao, viva cdm
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  magari 40? Kama kila gari ina watu 4, then watu 160 wa nini wote hao?
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wanajua fika mtoto wa CHADEMA
   
 9. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kazi ya Makamu wa rais ni kuweka mawe ya msingi na kuzindua visima tu? Kama ikitokea mwezi mzima hakuna jiwe la msingi linawekwa mahali au kisima kinazinduliwa mahali, basi yeye ni mwendo wa kula bata tu! Ndo maana post hizi wanapewa Wapemba/Wazanzibari kwa sababu ni watu laini laini?
   
 10. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,125
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  wanakubari kiaina!
   
 11. m

  mharakati JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  Mh Dr G Bilal ni stateman wa kweli kwenye hii CCM inayokufa inayonuka ufisadi isiyokua na viongozi wa kweli iliyojaa wasanii na wachumia tumbo
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wazenji wanapenda kazi rahisi rahisi, a.k.a Mdebwedo, ona mwenzie Maalim Seif alivyobusy kuweka mawe ya msingi kule Zenji... Pia Bilal inabidi ajifariji na kazi hiyo kwani safari zote za nje anachukua JK na kumuacha mshkaji ofisini bila kazi.
   
 13. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  chichiem oyaaaa!!!!! itikieni basi tuone humu tupo wangapi!!
   
 14. kilght

  kilght JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 626
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  hakika mchungaji anaijua siasa
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  humu chichiem hata hawafiki 10... Wanaona noma hata kuchangia huu uzi
   
 16. m

  mzambia JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ccm jamani....
   
 17. Entreprenegro

  Entreprenegro JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2014
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 602
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pamoja daima chadema
   
 18. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2014
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nguvu yoyote ina sifa moja, haipotei. sana sana itabadilika kutoka aina moja hadi aina nyingine ya nguvu. CDM OYEEE
   
 19. M

  Mandingo Nyeti Senior Member

  #19
  Mar 12, 2014
  Joined: Jan 26, 2014
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuonane March 16 Kalenga!
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2014
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni msg ya kumfanya bilal kuwa very insecure..kujiona yupo ktk foreign land na anahitaji kufuata taratibu za wenyeji.nadhani ndio maaana akawa mstaarabu.sijui ingekuwa lukuvi na wengine matusi ynagekuwa kiasi gani..
   
Loading...