Diwani wa CHADEMA huko Iringa mjini ahamia CCM adai Peter Msigwa ni dictator,uongozi manispaa haueleweki


Metakelfin

Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Messages
2,337
Likes
1,932
Points
280
Metakelfin

Metakelfin

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2017
2,337 1,932 280
Diwani wa kata ya kihesa jimbo la iringa mjini Edgar Mgimwa amejitoa chadema na kuhamia CCM

1ac7897edb56179f965426f4c14a0ef3.jpg

Moja ya sababu amedai ni udikteta unaofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Peter Msigwa. Huku akidai hakuna maeleweno kati ya mbunge na mkuu wa wilaya hali inayochangia kuzorota kwa mipango ya maendeleo na mwisho akadai hata wajumbe wa manispaa hawana maelewano mazuri kuhamia CCM.

276dd60cc8efe80cbf00a9869b6836c0.jpg
Diwani wa Chadema Kata ya Kihesa, Manispaa ya Iringa, Edgar Mgimwa amekihama chama hicho na kujiunga na CCM.


Mgimwa amejiondoa katika chama hicho wakati kukiwa na ushindani mkali kati ya Chadema na CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye kata mbili mkoani Iringa unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.
Alitangaza uamuzi huo jana Jumapili Novemba 5,2017 wakati wa mkutano wa kampeni za CCM katika Kata ya Kitwiru.

Kata nyingine inayofanya uchaguzi ni Kimala iliyoko wilayani Kilolo.
Mgimwa ameungana na wenzake watatu waliohama Chadema miezi kadhaa iliyopita akiwemo Baraka Kimata anayewania tena udiwani katika Kata ya Kitwiru, safari hii kupitia CCM.


Wengine ni waliokuwa madiwani wa Viti Maalumu (Chadema), Leah Mleleu na Husna Daudi ambao baada ya kujiuzulu walisema wataendelea kuwa wanachama wa chama hicho.


Hata hivyo, katika mkutano wa kampeni wa CCM jana walitangaza kujiunga na chama hicho. Wanachama hao wapya walipokewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.


Mgimwa akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Novemba 6,2017 amesema miongoni mwa sababu zilizomfanya ahame Chadema ni alichodai udikteta wa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.


Amesema kutokuwepo maelewano baina ya mbunge huyo na mmoja wa viongozi wa wilaya ya Iringa kunasababisha kuzorota kwa maendeleo jambo ambalo haliungi mkono.
Akizungumzia madai hayo, Mbunge Msigwa ameieleza Mwananchi kuwa, Chadema haibabaishwi wala kuyumbishwa na hatua ya diwani huyo kuhama.


Mchungaji Msigwa amesema chama hicho kina uhakika kuwa huo ni mwendelezo wa kile alichodai baadhi ya madiwani kununuliwa.
Amesema wanachokifanya sasa ni kujipanga kwenye uchaguzi mdogo ili kurejesha kata zilizokuwa zinashikiliwa na Chadema.


“Ukiwa vitani, inapotokea askari anaanguka huna haja ya kugeuka nyuma kwa sababu hafanyi jeshi zima kuyumba, sisi tunasonga mbele; na kwa sababu tunajua ni mpango wa kutengeneza hatuna wasiwasi katika hilo,” amesema Mchungaji Msigwa.


Amesema kwa sababu kata zinazoachwa wazi zitaitishwa uchaguzi mdogo, kazi yao itakuwa kuhakikisha wanashinda kwa kishindo.


Kuhusu hilo, Katibu wa Itikadi, Hamasa na Uenezi wa CCM Manispaa ya Iringa, Edol Bashiri ameieleza Mwananchi kuwa wataendelea kuwapokea madiwani wengine wanaohamia chama hicho kwa kuwa milango ipo wazi.


“Wanafuata sera safi na demokrasia inayoendeshwa kwa vitendo, tunaendelea kuwakaribisha wengine wanaotaka kuja na tutaendelea kuwapokea,” amesema.


Bashiri amesema wanaendelea kufanya kampeni na kwamba, wapo wanachama wengine wanaohamia CCM wakitokea Chadema.
 
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
13,621
Likes
11,449
Points
280
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
13,621 11,449 280
Diwani wa kata ya kihesa jimbo la iringa mjini Edgar Mgimwa amejitoa chadema na kuhamia CCM
1ac7897edb56179f965426f4c14a0ef3.jpg

Moja ya sababu amedai ni udikteta unaofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Peter Msigwa.Huku akidai hakuna maeleweno kati ya mbunge na mkuu wa wilaya hali inayochangia kuzorota kwa mipango ya maendeleo na mwisho akadai hata wajumbe wa manispaa hawana maelewano mazuri
276dd60cc8efe80cbf00a9869b6836c0.jpg
Yawezekana Ufipa wanauza madiwaniii kupata fedha za kuendesha chama!Vyama hivi sasa vimekuwa kama Simba na Yanga na hao madiwani ndio akina Yondani, Okwi, Nyoinxima na Ajibu yaani full biashara!!
 
likandambwasada

likandambwasada

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Messages
5,461
Likes
5,864
Points
280
likandambwasada

likandambwasada

JF-Expert Member
Joined May 27, 2015
5,461 5,864 280
KUMBE MGIMWA.

R.I.P WAZIRI MGIMWA
 
MZEE MSASAMBEGU

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Messages
2,743
Likes
2,388
Points
280
MZEE MSASAMBEGU

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2013
2,743 2,388 280
Diwani wa kata ya kihesa jimbo la iringa mjini Edgar Mgimwa amejitoa chadema na kuhamia CCM
1ac7897edb56179f965426f4c14a0ef3.jpg

Moja ya sababu amedai ni udikteta unaofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Peter Msigwa.Huku akidai hakuna maeleweno kati ya mbunge na mkuu wa wilaya hali inayochangia kuzorota kwa mipango ya maendeleo na mwisho akadai hata wajumbe wa manispaa hawana maelewano mazuri
276dd60cc8efe80cbf00a9869b6836c0.jpg
Mwache aende ni haki yake kikatiba...ingekuwa kahamia chadema ccm wangeanza kudai huyo ni fisadi
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
9,931
Likes
1,509
Points
280
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
9,931 1,509 280
ahsante kwa tarifa
Nalog off
 
karekwachuza

karekwachuza

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2013
Messages
955
Likes
152
Points
60
karekwachuza

karekwachuza

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2013
955 152 60
Huyu hana akili kabisa anashikiliwa akili mna maccm
 
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
4,003
Likes
1,443
Points
280
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
4,003 1,443 280
Kituko ni kwamba tunaposhangilia tukumbuke ni kodi zetu zitagharamia uchaguzi huo!! Milioni hamsini kila kijiji zinayeyushwa na upuuzi huo tunakenua tu!!
Alipata kusema bondia mmoja "wakila mamba wanacheka, mamba akila mtu wanalia"
 
libeva

libeva

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Messages
2,636
Likes
984
Points
280
libeva

libeva

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2015
2,636 984 280
Diwani wa kata ya kihesa jimbo la iringa mjini Edgar Mgimwa amejitoa chadema na kuhamia CCM
1ac7897edb56179f965426f4c14a0ef3.jpg

Moja ya sababu amedai ni udikteta unaofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Peter Msigwa.Huku akidai hakuna maeleweno kati ya mbunge na mkuu wa wilaya hali inayochangia kuzorota kwa mipango ya maendeleo na mwisho akadai hata wajumbe wa manispaa hawana maelewano mazuri
276dd60cc8efe80cbf00a9869b6836c0.jpg
Mbona kachelewa kuhama?
 
Double Elephants

Double Elephants

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2013
Messages
472
Likes
396
Points
80
Double Elephants

Double Elephants

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2013
472 396 80
Angehama kabla ili uchaguzi wa marudio ufanyike.
 

Forum statistics

Threads 1,236,780
Members 475,220
Posts 29,268,129