Ezekiel Wenje awasha moto Bungeni

Wakati freedo inakuja kesho mtaweza kuzima moto wa hiyo freedom? Maana haiji kibaridi baridi... Kitawaka hapa ohooo... Mimi mbio sina jamani
 
Ana kheri mtu yule atakayemwangaikia mtanzania mmoja wapo wa hawa: yatima; wajane; wanafunzi walotelekezwa (hakuna madawati, vifaa vya maabara, walimu wao wamekopwa nk); wagonjwa (hospital dawa hakuna ili hali msd inaozesha dawa za zaidi ya Shs 6 bln kwa mwaka); wakulima (wanaporwa mazao yao kwa bei ya chee ili hali mborea za ruzuku wakilaguziwa); nk nk; na alaaniye mtu yule atakaye ngangana kuwaibia watu hao kwa mgongo wa amani au style ya kujuvua magamba.
 
CCM mpendwa wangu Baba. Kwani wewe ndiwe mkombozi wa watanzania kibenzi cha watanzania! CCM ndiye Baba...... CCM yajenga nchi....... na kikwete ndezi nguzo yetu.............CCM yajenga nchi. Jamani nimejaribu kubadilisha wimbo huu lakini naona maneno hayakubali vile! nisaidieni.
 
hapo kwenye red 100/100=1

pia naunga mkono hoja kwa 100%, tena ikiwezekana kabla vikao vya bunge hili havijaisha tuingie barabarani.

Nadhani yuko sawa tu. Kapata 60/100 au 20/100, sasa hii ya 100/100 means perfect ever.
 
Toka nje, nimesema kaa chini .Kazi kutoa hoja za kitoto. Ukweli utawaweka huru.
 
Hawa ndio viongozi ambao mnasema wataipeleka Tanzania kwenye rank ya kimataifa? Hizi kauli za kitaarabu taarabu na mipasho ndio mnataka zijenge the best economy in EA? Two wrong cant make it right, rushwa ni sumu ya maendeleo either iliwe na JK au iliwe na mwalimu wa msingi pale Sukita. It's obvious kwamba baadhi ya wabunge wetu wana either maono madogo au wanafuata upepo.
 
Leo Wanje kanifurahisha sana

Wanje kasema
hawezi kusema ni sahihi polisi kula rushwa pia hawezi kutumia nguvu na akili nyingi kupiga kelele kwa polisi wapunguze rushwa
Akaongeza wabunge wengi wa CCM wanawakandia polisi kwa kula rushwa ila wanasahau kuwa polisi wameamua kujimegea kilicho mbele yao kama vile mawaziri wanavyojimegea.

Akamaliza hivi :kama tunataka rushwa ikomeshwa ndani ya jeshi la polisi tuimalize kwanza kwenye baraza la mawaziri na wakuu wa idara vinginevyo tuwaache polisi waendelee hivyohivyo walivyo.

my take: ccm wasilinyooshee kidole jeshi la polisi kwa rushwa kwani na wao (ccm) NI MAFISADI WAKUBWA.

Hii inanikumbusha miaka ile wakati Jenerali Ulimwengu alipokuwa bado anaingia bungeni, aliwahi kuimbia serikali kwamba haipashwi kupoteza muda kujadili rushwa za manesi na polisi ambao wanachopata ni kuwasaidia tu kuganga njaa, alisema tunapashwa tupigie kelele 10% wanazopata watu kwenye mikataba mikubwa kwani hiyo ndio rushwa inayoliangamiza taifa. Sijui kama kauli hiyo ndio ilimfanya apigwe uhamisho kutoka kuwa mkuu wa wilaya ya Ilala na kutupwa Singida, lakini aliwaambia ukweli na wakubwa huo ni ukweli walikuwa hawataki kuusikia.

Bravo Wenje keep it up!!!!

Tiba
 
Nilikuwa sijawahi kumsikia yule Mb Lusinde akichangia hoja, leo nimemsikia ilibidi nisonye pekee yangu, yaani jamaa alikuwa anaongea pumba kiasi nikaanza kujiuliza hivi ni kipi hasa kilichowafanya wana Mtera wakampiga chini tingatinga na kupeleka hiki kibajaj Bungeni? well kama Wenje ndivyo hivyo alivyosema ( kuwa baraza la mawaziri linakula rushwa) na spika/naibu spika hajamuomba alete ushahidi basi kuna ukweli tosha katika hayo, maana niwajuavyo CCM, Lukuvi angeisha simama mara moja kutoa taarifa!
 
Huu mgao wa umeme unatunyima uhondo mjengoni, wenzetu wenye umeme mnafaidi sana, ila nawapongeza saaana kwa kutokuwa wachoyo wa habari, tunaomba muendelee hivyo hivyo kutujuza
 
Leo Wanje kanifurahisha sana

Wanje kasema
hawezi kusema ni sahihi polisi kula rushwa pia hawezi kutumia nguvu na akili nyingi kupiga kelele kwa polisi wapunguze rushwa
Akaongeza wabunge wengi wa CCM wanawakandia polisi kwa kula rushwa ila wanasahau kuwa polisi wameamua kujimegea kilicho mbele yao kama vile mawaziri wanavyojimegea.

Akamaliza hivi :kama tunataka rushwa ikomeshwa ndani ya jeshi la polisi tuimalize kwanza kwenye baraza la mawaziri na wakuu wa idara vinginevyo tuwaache polisi waendelee hivyohivyo walivyo.

my take: ccm wasilinyooshee kidole jeshi la polisi kwa rushwa kwani na wao (ccm) NI MAFISADI WAKUBWA.

Kwa hiyo Wenje anasema nini sasa? Ni halali kwa wadogo kula rushwa kwa sababu wakubwa wanakula rushwa?

Kwa minajili hii anatuambia kwamba na yeye anakula rushwa kwa sababu mawaziri wanakula rushwa?

Kama hali rushwa, kwa nini anasema "hawezi kutumia nguvu nyingi kupigia kelele polisi wapunguze rushwa" ?

Anaelewa kwamba "two wrongs do not make a right"?

Kwamba wrong is wrong, even if the entire Tanzanian population is doing it.

Wabunge wetu wanaelewa kwenda kwa principle au ni bendera kufuata upepo?

Hawa ndio wanamageuzi wenyewe hawa? Wanao excuse rushwa kwa sababu mkubwa anakula rushwa?

:kama tunataka rushwa ikomeshwa ndani ya jeshi la polisi tuimalize kwanza kwenye baraza la mawaziri na wakuu wa idara vinginevyo tuwaache polisi waendelee hivyohivyo walivyo.

Really?

Wenje anataka kero za wananchi wa kawaida zifugwe eti kwa sababu Mawaziri wanakula rushwa?

Kama tuna uwezo wa kukamata traafic police wanaoomba rushwa, tuwaachie kwa sababu mawaziri wanakula rushwa?

Huyu ndiye mbunge wetu msomi huyu?

Hivi alikuwa anamsema Lusinde hajasoma, yeye kasoma nini? Alichosoma kimemsaidiaje mpaka sasa kiasi anaweza kutoa kauli za kipumbavu kama hizi?
 
Muongozo wa SUPIKA,
MH. SUPIKA MBONA MH.WENJE ANAONGEA UKWELI SANA,NAOMBA MH WENJE ASITUVUE NGUO,,,,,,,hahahahahaaa
 
Mtoto wa mama ntilie namkubali heko CDM

Mbona unataka kuleta kashfa? Kwani kuwa mtoto wa mama ntilie kuna ubaya gani? Si afadhali huyo mama ntilie anajua wajibu wake wa kufanya kazi ili kutunza watoto wake!?
 
Hawa ndio viongozi ambao mnasema wataipeleka Tanzania kwenye rank ya kimataifa? Hizi kauli za kitaarabu taarabu na mipasho ndio mnataka zijenge the best economy in EA? Two wrong cant make it right, rushwa ni sumu ya maendeleo either iliwe na JK au iliwe na mwalimu wa msingi pale Sukita. It's obvious kwamba baadhi ya wabunge wetu wana either maono madogo au wanafuata upepo.

Mkuu upo sahihi kabisa lakini je ni halali watu wanaopokea rushwa ili wapitishe bajeti za wizara fulani fulani wanayo haki ya kuweka midomo juu na kuwanyooshea Polisi vidole as if wao ni wasafi? Wanapashwa watoe kwanza boriti kwenye jicho lao kabla ya kuona kibanzi kwenye jicho la polisi. Tukatae au tukubali, polisi walio wengi wanadai na kupokea rushwa ili kuziba pengo llililopo kati ya kipato (Mshahara) na hali ya maisha!!! Polisi analipwa laki mbili kwa mwezi ana watoto watatu wanaosoma shule ana mke analipa kodi ya nyumba umeme na maji hapo niambie hiyo laki mbili anaipangiaje bajeti?. Ni unafiki uliopitiliza kuwalaumu wanaodai na kupokea rushwa ndogo ndogo wakati waliopokea rushwa zinazoliumiza taifa kina Chenge na Idrisa Rashidi tunawaona ni mashujaa!!!!.

Kama kweli tunataka kupiga vita rushwa ndogondogo tuache unafiki tuilazimishe serikali iwalipe watumishi mshahara unaolingana na hali halisi ya maisha, baada ya hapo mtu akikuomba rushwa ni haki kuminin'giza. Na kama kweli tuko serious na kupiga vita rushwa, tuanze na hao hao wabunge!!!! Pambafa!!! Naogopa ban la sivyo ningetukana kabisa!!!

Tiba
 
Kwa hiyo Wenje anasema nini sasa? Ni halali kwa wadogo kula rushwa kwa sababu wakubwa wanakula rushwa?

Kwa minajili hii anatuambia kwamba na yeye anakula rushwa kwa sababu mawaziri wanakula rushwa?

Kama hali rushwa, kwa nini anasema "hawezi kutumia nguvu nyingi kupigia kelele polisi wapunguze rushwa" ?

Anaelewa kwamba "two wrongs do not make a right"?

Kwamba wrong is wrong, even if the entire Tanzanian population is doing it.

Wabunge wetu wanaelewa kwenda kwa principle au ni bendera kufuata upepo?

Hawa ndio wanamageuzi wenyewe hawa? Wanao excuse rushwa kwa sababu mkubwa anakula rushwa?

Really?

Wenje anataka kero za wananchi wa kawaida zifugwe eti kwa sababu Mawaziri wanakula rushwa?

Kama tuna uwezo wa kukamata traafic police wanaoomba rushwa, tuwaachie kwa sababu mawaziri wanakula rushwa?

Huyu ndiye mbunge wetu msomi huyu?

Hivi alikuwa anamsema Lusinde hajasoma, yeye kasoma nini? Alichosoma kimemsaidiaje mpaka sasa kiasi anaweza kutoa kauli za kipumbavu kama hizi?
utatumia miaka kumi kueleweshwa na hutaelewa
 
Hawa ndio viongozi ambao mnasema wataipeleka Tanzania kwenye rank ya kimataifa? Hizi kauli za kitaarabu taarabu na mipasho ndio mnataka zijenge the best economy in EA? Two wrong cant make it right, rushwa ni sumu ya maendeleo either iliwe na JK au iliwe na mwalimu wa msingi pale Sukita. It's obvious kwamba baadhi ya wabunge wetu wana either maono madogo au wanafuata upepo.

Thank you, nimelisema hili pia.

Hatari ni kwamba sasa tunakaribia kutochambua mada, watu wanangalia, nani kasema? CHADEMA? Oyeeeee, hata kama upuuzi.

CHADEMA ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kutetea rushwa ndiyo Demokrasia na Maendeleo?

Manifesto ya CHADEMA inasemaje kuhusu rushwa? Katiba ya CHADEMA inasema nini kuhusu rushwa?

Ndivyo miongozo ya CHADEMA inavyosema kuhusu rushwa hivi au huyu bwana katetereka yeye kama mtu binafsi tu?

Tuambizane tujue kabisa kwamba CHADEMA wakichukua nchi rushwa "ndogo" itaruhusiwa mpaka rushwa "kubwa" imalizwe kwanza.
 
utatumia miaka kumi kueleweshwa na hutaelewa

Of course sitaelewa kama kueleweshwa kwenyewe kunakuja kwa sentensi ya "utatumia miaka kumi kueleweshwa na hutaelewa"

Let's face it, Wanje kwa kutetea rushwa kachemsha.

Hii ndiyo misingi ya CHADEMA hii?

Kati yangu mie niliyeuliza maswali ambayo umeshindwa kuyajibu, na wewe unayetoa a cryptic defence, anani anaonyesha uelewa?

Kama kuua watu milioni moja ni vibaya, kuua mtu mmoja kusisimamishwe mpaka kuua watu milioni moja kusimamishwe?

Hawa polisi wanaotetewa leo kula rushwa, kesho hawawezi kuwa viongozi wakubwa? Ukishawaachia kula rushwa leo, kesho wakienda kwenye deal kubwa ndio utaweza kuwazuia?
 
Rushwa kwa Watanzania mi sehemu ya maisha.Serikalini na kila pahala.Ni kweli hatuwezi kuwanyooshea kidole Polisi peke yao.
To be honest,wengi tunatoa rushwa au kupokea in one way or another.
 
Back
Top Bottom