Ezekiel Maige, Tour Guide wa Kizungu wamevamia Mbuga zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ezekiel Maige, Tour Guide wa Kizungu wamevamia Mbuga zetu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MVUMBUZI, Jul 7, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kwa muda mrefu serikali yetu imekuwa ikisisitiza kuwa ajira ambazo watanzania wana uwezo wa kuzifanya wageni kutoka nje hawaruhusiwi kuzifanya. Msisitizo huu unatokana na malalamiko ya waTanzania katika sekta nyingi kujikuta ajira zao zikichukuliwa na wageni kutoka nje ya nchi yetu tena bila kuwa na kibali cha kufanya kazi.

  Zamu hii ni kilio cha Tour Guides wa Kitanzania ambao walikuwa wanajipatia riziki yao kubwa kutokana na tip walizokuwa wanapewa na watalii wanao wapeleka kuona vivutio vyetu mbalimbali vya kitalii hasusani mbuga za wanyama.

  Namwomba nimweleze Ezekiel Maige kuwa makampuni mengi ya kitalii kutoka nje yamewaajiri Tour Guides kutoka nje(wazungu wenzao) huku wale wa kitanzania wakibakia kuwa madereva tu.

  Tour guide hawa wamekuwa wakijichanganya na watalii na kwa sababu wote ni wazungu inakuwa vigumu kugundua kama mmojawapo siyo mtalii bali ni tour guide wa kizungu. Madereva wanawajua na wameanza kulalamika kwa sababu hawa tour guide wa kizungu ambao hawajui lolote kuhusu mbuga zetu wamekuwa wakichukua ile tip ambayo ni stahili ya madereva ambao wengi wamesoma tour guide.

  Kampuni ya kitalii ya KER & DOWNEY SAFARIES inayomilikiwa na Tom Fredkin ambaye ni raia wa Afrika ya Kusini aishiye Marekani na yenye ofisi yake Ngaramtoni mjini Arusha inaongoza kwa kuwa na Tour guide wote wazungu lakini hujichanganya na watalii ili wasijulikane. Madereva wake wamekuwa wakilalamikia hali hiyo ambayo wamesema inawafanya kuwa hohehahe kutokana na tips zao kuchukuliwa na tour guide fake wa kizungu. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hawa wazungu uchwara hawana vibali vya kufanya kazi nchini na hawana ujuzi wowote wa Tour guide na mara nyingi hutumia mgongo wa madereva wa Ki tanzania kufanya hiyo kazi.

  Mbaya zaidi kuna wazungu ambao wameanzisha makampuni ya kubeba watalii ambao huishi tu porini na huwa hupokea wageni wanaotumia usafiri wa ndege zinazotuwa ndani ya viwanja vya ndege vilivyoko katika mbuga zetu mbalimbali.

  Mh. Ezekieli Maige naomba utueleze kama unajua hili na kama unajua basi tujibu sisi watanzania ambao mbuga ni zetu kuwa hawa wazungu wanafanya nini kwenye mbuga zetu?

  Inakuwa mgeni kumwelekeza mgeni katika mbuga zetu huku serikali imelala usingizi tu huku wenye rasilimali wakibakia wasindikizaji tu?

  Mpaka lini waTZ tutabaki tukitazama bila msaada rasilimali zetu ziporwa na wwageni mchana kweupe bila kufaidi hata ile staili ndogo kama tip?
  Maige naomba usikie kilio cha watanzania wenzako inawezekana Mungu alikupa hiyo nafasi utusaidie kama Yusufu alivyowekwa Misri kuwasaidia ndugu zake.

  Kama uko tayari details zote utazipata na ili kurudisha heshima ya nchi maana hawa wazungu wanatuonea na kutuona mama huruma.
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  katika sector ambayo watanzania wametupwa ni utalii tena kwa kisingizio cha lugha,
  hali mimi nimekutana na watalii wengi wanapenda sana kuugumiwa na watu LOCAL maana wana mengi wanapenda kujua
  sasa kuna wapilipino kwenye mahoteli huko mbugani kama mchanga
  na siri kubwa ya wapilipino ni kuwa CHEAP labour
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mvumbuzi, you have nailed it................... unfortunately, what you said, may not be applicable in tiizii
   
 4. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tatizo la lugha siyo kubwa kihivyo haswa kwenye kuongoza watalii ni kwamba mgeni akija na kampuni anakuja na ndugu zake ili kupata zile tips ambazo waTZ wangefaidi.Pia ni kweli kwamba wageni wengi wanapenda kuhudumiwa na LOCAL kwa sababu wanawapa maelezo asilia na wanaijua nchi yao zaidi na kwa hiyo wanawapa uelewa zaidi kuliko wazungu wenzao.

  Ukiongea na tour guides wengi wa kiTZ wanakwambia kwamba ukienda mbugani wazungu ni wengi mno na wako makundi mawili. Kundi la kwanza ni watalii na kundi la pili ni wamiliki wa makampuni ya kitalii kutoka nje na wenzao. Yaani ukifika porini utafikiri mbuga haziko tena mikononi mwa Tanzania bali wazungu kwani hawana limit ,hawana msimamizi na wanajifanyia mambo wanavyotaka.
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu inahitajika commitment tu hapa kwani akiwaomba wa TZ wanaofanya kazi na makampuni haya watapata msaada mkubwa kwani wengi tayari hali hii inawakera. Madereva wengi wa Tours hapa Arusha ambao wengi ni tour guide miaka 7 iliyopita walikuwa na kipato kizuri sana na waliweza kujenga na kupeleka watoto wao shule nzuri ila baada ya hii tabia wengi wamebaki na vile vimishahara wanavyolipwa yaani 100,000 hadi 140,000.

  Hata hivyo mkuu inabidi tuendelee kupiga kelele kuna wakati masikio yao kama si kuzibuka basi walazimika kuzinduka usingizini penda wasi pende
   
 6. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Mvumbuzi,uliyosema ni kweli na hayajaanzia leo,yapo yanaonekana,lakini hakuna wa kumfunga paka kengele,ni bahati mbaya kuwa kati ya wizara ambazo hazijapata kuwa na waziri committed basi ni hii ya utalii na maliasili,Maige analifahamu sana hili swala la guides wa kigeni ila hata yeye hana ubavu wa kuwatoa,maana na yeye ni sehemu ya tatizo
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  Source please.......
   
 8. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Angalia nimetaja kampuni ya Ker & Downey ambayo tour guide wake ni wazungu (makaburu) wanaojichanganya na watalii na kukinga tips ambazo kwa kawaida ni staili ya madereva ambao pia wana professional za tour guide. Siwezi taja kampuni kama hakuna evidence na nimesema waweke mtego hata wiki haipiti watawakamata hao wazungu njaa wanaojidai Tour guide
  Source ni mimi na ushahidi ninao na kama unataka detail zipo na kama unataka kuhakikisha mtafute Tour driver yoyote wa hiyo kampuni ukae naye privately na kama hilo ni ngumu ni PM maana hapa pia nalinda ajira za watu
   
 9. p

  plawala JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama wizara yenyewe ina waziri
  Ni ombwe kubwa sana kama wizara zingine
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Matatizo ni mengi tuu sana, siyo hayo ya kuwa na wazungu waongoza watalii ni makampuni mengi yaliyoko nje hayana manufaa yote kwa uchumi wetu, kwani wanatuma pesa chache tu za ku cover parkfees and running expenses na makampuni hayo ni mengiiiii saaaana. Maige tunaamini uko vizuri lifanyie hili kazi kwani serikali inakosa mapato mengi wanabaki kuongeza kodi kenye sigara, bia , soda . Mafuta ya taa na mengineyo kila mwaka. Shida kubwa ni upeo wa viongozi wetu kufikiri na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kama amekaa kimya basi naomba wabunge ambao ni wazalendo wa kweli na wanaowapenda waTZ nawaomba wakusanye evidence kwangu na ikiwezekana wakati wa kuchangia hotuba ya bajeti wambane vilivyo huyu waziri. najua hayo makampuni yakitumiwa hata barua za onyo waki site mifano halisi hali hii lazima itapungua. Nimeanza na Ker & Downey na hili likianza kufanyiwa kazi makampuni mengine yatajulikana tu na tutakuwa tume okoa ajira na kuongeza vipato vya watanzania wengi tu
   
 12. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kwa sababu tangu enzi za Shamsa Mwangungu hali hii ilikuwepo na kilichowakatisha waTZ wa makampuni haya tamaa ni pale walipokuwa wakimwona waziri huyu akitembelea ofisi za makampuni makubwa ya Tour kutoka nje na mara nyingine kupata chai na kushiriki hafla mbalimbali bila hata kuongea na wafanyakazi kujua changamoto zao. bila shaka alikuwa hatoki bure bila bakshishi.

  Mambo waliyoyafanya akina Carl Peters na mtemi Kimweri na wengine yalituudhi sana tuliposikia eti kwa sababu sisi ni wajanja ila naona tunarudi kulekule kwa kudanganywa na vihela, chai na tafrija
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Senkyuu Mvumbuzi, nikuongezee listi kuna Dany MCullum , Robin Hurt na kuna kampuni moja ingine ntafAnyia uchunguzi na kukuambia jina.
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Senkyuu Mvumbuzi, nikuongezee listi kuna Dany MCullum , Robin Hurt safaris na kuna kampuni moja ingine ntafanyia uchunguzi na kukuambia jina.
   
 15. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Je una uhakika niiongeze kwenye list yangu? Maana inabidi uniambie iko mkoa gani na ofisi zake ziko wapi.
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tanzania na hasa JK na Maige sijui kama wanaelewa lugha tunayo endelea kuitumia .Tumesha waeleza sana juu ua ujinga lakini wanasema tumesikia na yanaishia hapo hapo .Hawako serious na haya mambo na kweli kampuni nyingi ziko Ulaya na hawalipi kodi kabisa .Ndiyo tunavyo umizwa .TATO si huru kabisa .Wazungu wana honga mno kuwapata viongozi wanao wataka ili waendelee kula .Kuna uhalifu mwingi unafanywa kwenye utalii na serikali haiko pamoja nasi kabisa .Sijajua kigugumizi hiiki ni cha nini .
   
 17. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Nilipata kusema huko nyuma,kuchagua ccm ni maafa,na haya ndio matokeo ya sera mbovu za serikali ya ccm,kwani mmesahau hawa wazungu walivyotunisha msuli kwenye utalii wa uwindaji,serikali ikafyata?
   
 18. d

  dropingcoco Senior Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona nlkigoogle hiyo kampuni na huyo mmiliki wake napata taarifa tofauti,
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa mtu katoka majuu kuja tanzania kupata experince ya kitanzania kwa nini apewe tour guide wa kizungu.
  • Ina maana tour guide wetu hawana qualification au hawajafundishwa jinsi ya kuwahudumia watalii wa nje?
  • Hospitality industry ya tanzania iko hoi ?
  But wahatver the case nadhani mtalii wa kweli anapenda akija apate tour gider wa sehemu asili hata kama anachapia lugha. Huo ndio utalii na ndio experince yenyewe ya utalii.

  Siwezi kwenda kutalii UK nikafurahia kupewa tour guider mtanzania. Pamoja na kizungu changu cha kuunga unga nitataka nipate huyo huyo mzungu.
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hili nakubaliana na wewe mia kwa mia ila najua hizi rasilimali ni zetu na lazima zitunufaishe wa TZ wote. Kama inafikia hatua waziri au serikali inajali maslahi ya wageni badala ya watu wake basi inabidi wenye nchi wakomboe nchi yao. Leo Kenya wameanza maandamano ya hali mbaya ya maisha na kama mchezo na tusishangae yakahamia huku. Sasa sijajua kama huko Kenya ni CDM walikuwepo au ni hali mbaya imewasukuma wananchi ku- respond. Ni ukweli tunahitaji Musa wetu wa kututoa utumwani Misri turudi nchi waliyo itabiri waasisi wetu.
   
Loading...