Ezekiel Maige, Tour Guide wa Kizungu wamevamia Mbuga zetu

Serikari yenu isipowasikia tembeeni na mishale, ukiona mzungu anajifanya tour guide piga mshale washingo! wataanza kuwaelewa mnachosema ...
kama mbwai mbwai bwana kwani nini ?? usiogope noma hata kama ni noma...
 
Tanzania na hasa JK na Maige sijui kama wanaelewa lugha tunayo endelea kuitumia .Tumesha waeleza sana juu ua ujinga lakini wanasema tumesikia na yanaishia hapo hapo .Hawako serious na haya mambo na kweli kampuni nyingi ziko Ulaya na hawalipi kodi kabisa .Ndiyo tunavyo umizwa .TATO si huru kabisa .Wazungu wana honga mno kuwapata viongozi wanao wataka ili waendelee kula .Kuna uhalifu mwingi unafanywa kwenye utalii na serikali haiko pamoja nasi kabisa .Sijajua kigugumizi hiiki ni cha nini .

Ndugu yangu haswa hapo kwenye red nakuunga mkono kwani ukiingia deep kwenye mbuga/mapori yetu utagundua kuna wazungu wengi wamejichimbia poriri sijui wanafanya nini na huko hata serikali haifiki. Ukifika maeneo ya Lake Natroni kwa mfano wananchi wa kule wengi wanatumia fedha za Kenya na hatujui kulikoni na hata ukikuta pikipiki nyingi kule zina namba za Kenya. Huko porini kuna viwanja vingi vya ndege na wanaotuwa humo ni wazungu na hakuna mtu yeyote wa idara ya uhamiaji au TRA kwani wengi wanapenda kukaa mijini kunako patikana rushwa kirahisi. Nchi inaporwa mno na tunapoteza mapato mengi si tu kama nchi bali hata watanzania. wazungu wamejua sisi ni wapumbavu na wameamua kukaa porini kufanya mambo mengi ambayo hata serikali haijui na wala haijulikani wako pale kufanya nini na wamekuja kivipi?
 
Sasa mtu katoka majuu kuja tanzania kupata experince ya kitanzania kwa nini apewe tour guide wa kizungu.
  • Ina maana tour guide wetu hawana qualification au hawajafundishwa jinsi ya kuwahudumia watalii wa nje?
  • Hospitality industry ya tanzania iko hoi ?
But wahatver the case nadhani mtalii wa kweli anapenda akija apate tour gider wa sehemu asili hata kama anachapia lugha. Huo ndio utalii na ndio experince yenyewe ya utalii.

Siwezi kwenda kutalii UK nikafurahia kupewa tour guider mtanzania. Pamoja na kizungu changu cha kuunga unga nitataka nipate huyo huyo mzungu.


Hapa jirani Kenya huwezi kuta Tour Guide mzungu, nenda Israel kwa wale waliokwisha kwenda hakuna tour guide asiye Mwisrael. Ina maana kule maboma ya wamasai si wamasai ndo wanaongea na wanakuwa na mkalimani mtanzania tena mmasai na mbona kila kitu kina kuwa ok tu.

Kuna mtu amesema wazungu wana waonga viongozi wenye dhamana ya kuhakikisha haya mambo hayatokei. Kama ujuavyo hata kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa rushwa hupofusha na hupindisha haki ya mtu kwa hiyo naona hawa viongozi wetu wamepigwa upofu na rushwa na si kama hawajui haya mambo.
 
madini yashindikane kudhibiti ndio itakuwa utalii? na bado mtachonga sana mwaka huu


Sasa dropingcoco umeamua kujikalia tu kwa kukata tamaa au kuwazomea wanao piga kelele? say something positive my friend au wewe ni Kaburu?

Mtembea bure au msema bure si sawa na mkaa bure au mkaa kimya kwani naamini kilio chetu kitasikika kama si leo basi kesho. Kumbuka hotuba maarufu ya Martin Luther Jr. " I have the Dream" haikufa naye bali ile dream imekuja kuwa realized . Na sisi tunafanya hivyo kuliko just kukaa kimya huku nchi yetu ikiishia mikononi mwa watu wachache wenye uroho wa mali hata ikibiri kuwauza waTZ wenzao
 
inauma sana..!

preta vipi?...say something.halaf nasikia na wewe ni mod?
 
We unaongelea tour guide sasa hivi nyumba zingine Dar zina mahausigeli kutoka Ufilipino usiniulize wamepata wapi work permit.
 
We unaongelea tour guide sasa hivi nyumba zingine Dar zina mahausigeli kutoka Ufilipino usiniulize wamepata wapi work permit.


Hii nchi basi haina wenyewe na viongozi wetu kwa kiasi kikubwa hawajulikani wanafanya nini hasa kwa sasa zaidi ya kushambulia upinzani na kusafiri wakati nchi inavamiwa. Ufagio unatakiwa upite kila kampuni kumulika na ninaishauri serikali iunde tume neutral ya kushughulikia wageni walioko nchini na kufanya kazi kinyume na sheria la sivyo tunabaki watupu na hatimaye kupoteza heshima mbele ya mataifa mengine.
 
Mvumbuzi,
Nashukuru sana kuwa umetoa angalizo kwa serikali juu ya kadhia hiyo, ili wafanye uchunguzi.

Kampuni hii naifahamu, maana kwa namna moja ama nyingine ofisi yangu ina udau na kampuni za Watalii.
Mara baada ya kusoma article ya Mvumbuzi nilifuatilia kwa jamaa wenye uhusika wa moja kwa moja na uendeshaji wake wakanipa maelezo yao.
Wanasema kwamba ni kweli wazungu wanafanya hiyo kazi ya tour-guide. Lakini wanasema kuwa kampuni hiyo ina namna tofauti ya operations kulinganisha na tour companies tulizozizowea hapa. Wazungu hao(tour-guides) wanatafuta watalii wenyewe katika nchi mbalimbali huko duniani na kuja nao huku, hivyo hawawezi kuwakabidhi kwa waswahili wawatembeze, wakati wao ndio wamebeba risk yote kuwasafirisha na kuwa 'care, na wanasema itakuwa si customer care nzuri, kitu ambacho kitawafanya wageni hao wasirudi tena kwa kampuni hiyo!

Kwa reasoning ya kawaida, sababu hiyo haitoshelezi kabisa kuwakosesha kazi tour guides wetu, zaidi sana ninachokiona mimi hapo ni aina ya ubaguzi wa rangi wa wazungu ambapo wanaona mswahili hataweza kutoa maelezo fasaha kwa mgeni!
Lakini hilo ni kosa la kiufundi. Tunafungua milango hadi ya vyumba vya siri kwa wageni.

Naungana na Mvumbuzi hizi ni kazi rahisi sana za waswahili wenzetu, hii ingekuwa sheria rahisi sana kuimplement dhidi yawatu hawa weupe, sielewi ugumu unatokea wapi.
 
Mvumbuzi,
Nashukuru sana kuwa umetoa angalizo kwa serikali juu ya kadhia hiyo, ili wafanye uchunguzi.

Kampuni hii naifahamu, maana kwa namna moja ama nyingine ofisi yangu ina udau na kampuni za Watalii.
Mara baada ya kusoma article ya Mvumbuzi nilifuatilia kwa jamaa wenye uhusika wa moja kwa moja na uendeshaji wake wakanipa maelezo yao.
Wanasema kwamba ni kweli wazungu wanafanya hiyo kazi ya tour-guide. Lakini wanasema kuwa kampuni hiyo ina namna tofauti ya operations kulinganisha na tour companies tulizozizowea hapa. Wazungu hao(tour-guides) wanatafuta watalii wenyewe katika nchi mbalimbali huko duniani na kuja nao huku, hivyo hawawezi kuwakabidhi kwa waswahili wawatembeze, wakati wao ndio wamebeba risk yote kuwasafirisha na kuwa 'care, na wanasema itakuwa si customer care nzuri, kitu ambacho kitawafanya wageni hao wasirudi tena kwa kampuni hiyo!

Kwa reasoning ya kawaida, sababu hiyo haitoshelezi kabisa kuwakosesha kazi tour guides wetu, zaidi sana ninachokiona mimi hapo ni aina ya ubaguzi wa rangi wa wazungu ambapo wanaona mswahili hataweza kutoa maelezo fasaha kwa mgeni!
Lakini hilo ni kosa la kiufundi. Tunafungua milango hadi ya vyumba vya siri kwa wageni.

Naungana na Mvumbuzi hizi ni kazi rahisi sana za waswahili wenzetu, hii ingekuwa sheria rahisi sana kuimplement dhidi yawatu hawa weupe, sielewi ugumu unatokea wapi.


Mkuu PJ kwanza shukrani kwa kufanya follow up nzuri sana. Nafikiri wamekuwa wazi kueleza wanaovyoichezea Tanzania. walichoeleza kuhusu kutafuta wageni wenyewe na kuwatembeza wao ni kutaka kutueleza kuwa wao ni brokers /madali na tour guide. Naomba wajibu je hao makaburu wanaofanya kazi ya kutembeza watalii wana work permit? na je walikuja TZ kwa kazi hiyo?
 
Pia naomba nifafanue jamani SI KWELI KWAMBA HAWA WAZUNGU(tour guide fake) wanatafuta watalii nje na UKWELI NI KWAMBA Hawa tour guide wa kizungu wanaishi hapa hapa Arusha na wao hudandia magari ya tours kama makonda na wao huchukua kilicho cha madereva. Madereva wa KER & DOWNEY siku hizi hawapewi TIP kabisa na badala yake HUCHUKULIWA NA HAO MAKABURU NA KUWA HADAA KUWA WANAZIPELEKA OFISINI NA HUKO watapewe kwa utaratibu wa kiofisi jambo ambalo ni usanii mtupu. Madereva wamebaki na ahadi chungu nzima huku TIP zote wakichukua makaburu hao wanaojibanza kwenye gari za tours
 
Kama hao wazungu ndo wanaleta wageni kutoka nje basi waendeshe magari wao na wakifika getini wakaombe permit za wageni waliofuatana nao. Kama ni kweli mbona wakifika Ngorongoro getini hawathubutu kujitambulisha kama Guides wala kuomba permit kwa wageni wao na badala yake wanawachomekea madereva? Uoga walio nao wa kuomba permit kwa wageni wanao jidai ni wa kwao unadhihirisha wazi kuwa hawafanyi kazi kihalali nchini.


Ngorongoro getini wanafahamika ila hatujui kwa nini hawachukuliwi hatua na ukiuliza hao wahusika walioko getini wanasema tatizo ni TANAPA hawataki kuwashughulikia.
 
Kuna percent TANAPA wanachangia hili tatizo kuwepo kwa kutofuatilia hawa guide wa kizungu kwani inasemekana wanalifahamu. sijajua kwa nini hawataki kusimama kwenye nafasi yao kuwasaidia watanzania wenzao
 
Hii inasikitisha mno kwa wageni kupokonya hata kile kidogo kinachoangukia katika mikono ya watanzania. Tip ni mabaki ya fedha za watalii pia ni kuonyesha shukrani kwa aliyewafikisha pale walipotaka yaani madereva sasa inashangaza kuwepo watu wengine ndani ya gari ambao lengo lao kuu ni kuvizia tip. Tanzania mbona tumeacha mpaka kuvuliwa nguo za ndani jamani. Hatukatai hao wazungu wasifanye kazi humu ila tunachokataa ni kufanya kazi bila work permit na pia kufanya zile kazi ambazo ni raia tu anaruhusiwa kufanya. Uhamiaji , TANAPA, Ngorongoro Conservation Authority na wahusika wengine inabidi mfanye juhudi za makusudi kuondoa hii hali.
 
Tumegundua kwamba tour guides wa kitanzania na hususani wanaofanyia makampuni ya kizungu au wageni kutoka nje wanabanwa mno mno na wamebaki kuwa tu madereva huku wakidhulumiwa na marafiki wa wenye makampuni ambao wengi wana njaa kali na ndoo maana wanachukua tips zao.

Nashauri Mh. Maige ili kurudisha heshima ya Tanzania katika sector hii fanya utafiti na ufuatiliaji wa makusudi kutambua makampuni mengine including KER & DOWNEY ili wahusika wakamatwe na ikiwezekana kama ameingia nchini isivyo halali basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria za nchi ili wajue nchi hii inasimamia sheria zake na siyo tambara la kufutia uchafu wao.
 
Follow up inaweza fanyika pale geti la Ngorongoro ili kuwabaini hawa watu pia kufanya uchunguzi ndani ya haya makampuni haraka iwezekanavyo. Bila hivyo haitakuwa na maana kuendelea na mikakati ya kuondoa umaskini kama MKUKUTA(1&2), Tanzania Development Vision 2025, Kiilimo Kwanza n.k kama misingi ya umaskini kama hii haitavunjwa. Hii ni sawa na kujenga juu wakati huku chini kuna mtu au watu wanavunja msingi na matokeo yake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu au kujaza maji ndani ya gunia.
 
Heshima kwako Mvumbuzi.

Mkuu ni kweli tour guide wageni wamevamia kazi za wazawa.Bahati mbaya serekali ya magamba haina habari na masuala kama haya UWT iko kwaajili ya kuidhibiti CHADEMA na chama chochote kitakachotishia maslahi ya CCM.Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nafanyakazi fulani na kampuni ya SOKWE ASILIA nilishangaa kuanzia muhasibu,Inventory,manager wa camps,IT manager na key posts zote zimekamatwa na wageni [Kenya,Zimbabwe na S/Africa wazungu].Mishahara ya wafanyakazi wa wageni ulipwa kwa US Dollar[$ 5,000 - 12,000] pia haikatwi SDL,PAYE na NSSF.Hesabu za SOKWE ASILIA zinafungwa Kenya na South Africa.Hii ni kampuni moja yenye wafanyakazi wazawa zaidi ya 300 lakini wenye kulipwa kiwango kidogo cha mishahara Tsh 100,000 - 500,000/=.

Ukienda SERENA utashangaa nafasi zote kubwa zimeshikwa aidha na wahindi au wakenya.Ukwepaji wa kodi za serekali SDL,PAYE na Corporate Tax ni mkubwa kupita maelezo.Maafisa wa TRA mkoa wa Arusha wengi wana maisha ya juu kwasababu ya kushirikiana na haya makampuni kuinyima serekali mapato.wengi wanamiliki majumba na magari ya kifahari yasiyolingana na vipato halali.
 
Back
Top Bottom