Ezekiel 18:21 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ezekiel 18:21

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Prophet, Mar 18, 2011.

 1. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...lakini mtu mbaya akighairi na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kushika amri zangu zote na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.

  Kwa unabii huu, na kwa imani ya milele niliyonayo kwa maandiko matakatifu katika Biblia Taskatifu ya Mungu, naonya na kutamka mambo mawili:

  1. Kinachoendelea kwa babu loliondo ni usanii. dawa siyo kikombe cha babu. dawa ni kutenda yaliyohalali na haki. utaishi. hutakufa.

  2. Lowassa anajiwinda kwa gharama yoyote kutaka kugombea urais upande wa CCM, lakini dhambi alizotenda tunazifahamu na yeye anazijua, ndiyo maana alijiuzulu kwa sababu ya dhambi hizohizo, na wala hajawahi kusimama na kuwaomba radhi watanzania, na sasa anataka kugombea urais. Hajatenda yaliyo halali na haki. Huyu Lowassa hataishi milele, atakufa.
   
 2. m

  mja JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye blue: hivi na hao watakao mchagua kuwa rais watakuwa na akili kweli...?
   
 3. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unazungumziaje Uponyaji uliofanywa na Yesu kwa watu wenye magonjwa mbalimbali.

  Wanasiasa wao kuamua kutumia mwanya huu ,ili wafikie malengo yao hawatafanikiwa kwani la Mungu litasimama tu.

  Tumeumbwa kwa Sura na Mfano wa Mungu,hivyo ni wazi kabisa tunapaswa kufanya yanayompendeza na kufanana naye.

  Na kuhakikisha katika Uchaguzi tunachagua kilicho Bora kwa maendeleo ya Tanzania,tusiangamie kwa kukosa maarifa.

  Maana hata wana wa Israeli walipotaka jambo fulani kwa matakwa yao Mungu aliruhusu wakapata na walipopata shida na kuadhibiwa na baadaye kumgeukia Mungu, Mungu aliwapatia mtu wa kuwatoa huko.

  Hivyo nasi kama watanzania tunapaswa kujifunza,je waliopo huku madarakani wametufanyia nini au wametumia kura zetu kama fimbo ya kutuchapia,na kutunyonya.

  Na si kwasababu mtu anatoa msaada fulani kwa wakati fulani basi huyo anakufaa milele.

  Ubarikkiwe
   
 4. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  The prophet nakuomba uangalie upya bibila yako, maana ya kwangu inanionesha kua kitabu cha Ezekiel sura ya 8, kinaishia mstari wa 18, sasa wewe huo wa 21 sijui umeutoa wapi, ama unataka kuudanganya umma wa jf, ama ni a mistake umefanya kwa bahati mbaya ama ni kitu gani,,, rekebisha tafadhali.
   
 5. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kumbe hata ya kwako!nilidhani yangu imechakachuliwa,hata hivyo ni Ezekia 18:21.alikosea kidogo
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Max Melo nakuona upo humu, tafadhali kama anachokisema mdau hapa ni kweli, chukua hatua kabla thread haijasomwa na wengi zaidi..
   
 7. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmh kweli bana, hata mi sijaona huo mstari wa 21, mkuu ebu chek fresh afu tujadili
   
 8. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Umenishtukia! Ok mkuu, naona mkuu alikosea. Nimebadilisha. Ni Ezekiel 18:21

   
 9. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Uponyaji wa babu unahusiana vipi na Lowassa? Acha kuchanganya mambo.....
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  The Prophet Nakushukuru kwa thread nzuri.

  Mungu alisema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa!

  Ndivyo tulivyo Watanzania. Matatizo yote yanayotupata sasa,shida zote zinazotuumiza sasa nisababu ya kukosa maarifa! ''

  Kuna sehemu kwenye Biblia imeeandikwa ''' TIINI MAMLAKA ZILIZOPO DUNIA NA KILA MAMLAKA DUNIA ILIYOWEKWA IMETOKA KWA MUNGU'' Si kwamba Mungu alisema hivyo kumaanisha kila mamlaka inayoongoza ni halali! Lahasha! Wakati Mwingine tunapokosa maarifa Mungu huacha tupate viongozi Bomu ili tutakapoanza kuumia tumrudie yeye na kumwomba maarifa.....sasa inapotokea mtu kama Lowasa anataka kugombea Urais alafu tumchague kweli maarifa yetu yatakuwa yamezikwa.!!

  Tukumbuke hata wana Israel walimchagua SAULI kwa kukosa maarifa.....SAULI akawatesa sana. Walipopata Shida wakamlilia Mungu Ndiposa alipowachagulia DAUD.....Basi wandugu tumwombe Mungu ili tusichague makapi na Masauli wengine!
   
 11. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  EZEKIEL 18:21 ''''...lakini mtu mbaya akighairi na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kushika amri zangu zote na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.

  unaweza kuanzia mstari wa EZEKIEL 18:20-
   
 12. bona

  bona JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  hata mwinyi aliupata urais baada ya mutenda dhambi na kujiuzulu ndio akakubalika kwamba ni muadilifu anakubali na ana take responsibility kwa action zake! kwa iyo hizi talk za what lowassa did tuziweke pembeni na tujadili ya msingi we not gonna live our lives everyday in the shadow of what he did! tutamjudge kama atakavyokuja mbele yetu!
   
 13. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante mkuu.

  mods wamekusoma pia (wamenisaidia kurekebisha). ni Ezekieli 18:21

  thanks
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,657
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Neno linasema rushwa hupofusha, kwa vile atatumia rushwa, basi watakaopokea lazima watapofushwa.
   
 15. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu hawatendi haki. yakiwafika ya kuwafika badala wamkimbilie Mungu wanatafuta masangoma. and now it's getting even worse...politicilization is taking place. watu wanafisadi, wanatumia fedha walizofisadi kufadhili safari za wapigakura kwenda kwa babu. where is maarifa?
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  The Profhet...

  Shalom, mkuu natumaini u mwema na Mungu anazidi kukuhifadhi na damu ya thamani..nimesoma hapo juu ila nikupe tu angalizo si vyema kuwa na kisasi na mtu fulan kwa kumuunganisha mtu fulan..nimependa ulivyoweka hilo neno lakn ninachoona kwenye maandishi yako tofauti kabisa.

  Kumbuka babu hana uhusiano na Lowassa...na Lowassa ameenda kule si kama waziri mkuu mstaafu bali mtanzania kama wewe na mimi kwenda kupokea uponyaji.. Ndugu The Prophet kumbuka kinachofanyika kwa babu ni imani na si utapeli unachosema...nikukumbushe kwa maneno yako kama tapeli basi YESU angekuwa tapeli maarufu.

  ...lakini kwa Kuwa NENO LA MUNGU NI KWELI SAWA NA YOH 17:17 BASI SINA BUDI KUKWAMBIA ALICHOFANYA YESU AKINA TOFAUTI NA KINACHOENDELEA LOLIONDO...YAWEZEKANA...BADO HUJAPATA KIKOMBE LAKINI NAKWAMBIA KABLA UJAMWONA MUNGU LAZIMA KIKOMBE KIPITE KINYWAN MWAKO...HUU NI USHUHUDA NA ITACHUKUA WAZUNGU KUTOKA NJE KUJA KUMWAMINI HUYU BABU NA KUPATA UPONYAJI HALI WATANZANIA MKIKAA NA KUTOAMINI NA KUISHIA KUFA VIFO VYENYE UPONYAJI...

  SI MBAYA KULETA MAWAZO YAKO KWA LOWASSA LKN SI VYEMA KUMJUMUISHA HUYU BABU NA MAWAZO YAKO...

  SOMA

  ZABU 51:....YOOTE
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Habari hii i a aana kubwa sana mwaka 2015. - CHAGUO LA MUNGU.
  Ikiwa mganga wa maradhi sugu ametoka jimbo la mbunge X....
  Basi hata umasikini wetu ambao ni gonjwa sugu litawezekana kutoka kwa mbunge wa Loliondo....
   
 18. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shika amri za Mungu ZOTE. Hautaenda kwa Babu.

  Babu hatumii hata Biblia! Uchawi in another style. Najua utaniuliza kwani Yesu alikuwa na Bible? Nitakujibu Jesus is the Bible himself.
   
 19. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  connect the dots buddy!
   
 20. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Bado hujajibu swali,

  Usichukulie kina Lowasa kwenda kwa babu kama kiwakishi kuwa wengineo wote wanaokwenda huko ni wadhambi na mafisadi kama yeye!
   
Loading...