Extremism is on the rise in Zanzibar - Financial Times

Extremism is on the rise in Zanzibar - Financial Times

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,243
Reaction score
44,519
Under the peach arches of Al-Noor charitable agency for the needy just outside Stone Town in Zanzibar, a 24-hour Islamic radio station broadcasts religious guidance.

Female tourists should wear headscarves and cover their knees, says Mohamed Suleiman Ali, director of Radio Al-Noor, echoing the opinions voiced on radio. "It's too early to fight for an Islamic state because there are several stages to that, but a lot of things are being done contrary to the teachings of Islam," he says. "There's no social responsibility; the government keeps producing more [social] freedom."

Famed for its beaches, more than 170,000 holiday makers come to Zanzibar every year to swim with dolphins and lie beneath coconut trees. But the relaxed way of life that lures tourists to the mainly Muslim islands off the east coast of Africa is coming under threat from a rise in less tolerant forms of Islam. This is tapping into festering discontent over the island's sovereignty and beginning to influence social mores.

The islands – which make much of their money from tourism – are home to 1m people and more than 2,000 Muslim religious schools. Most of these draw on a long tradition of moderate and Sufi forms of Islam. But these are underfunded and staffed by volunteer teachers. Increasingly, parents are sending their children to better financed alternatives in a process that is beginning to parallel that taking place across a swath of sub-Saharan Africa from Somalia to Mali, where the growing influence of more radical forms of Islam can be felt.

READ MORE
 
em cut and paste hiyo story katika details zake kama una subscription hapo aise. details zinagoma hadi registration. wengine si registered FT. Please do the needful. Hebu iweke hapa story yote Mkuu, tafadhali...

High quality global journalism requires investment. Please share this article with others using the link below, do not cut & paste the article. See our Ts&Cs and Copyright Policy for more detail. Email ftsales.support@ft.com to buy additional rights. Extremism on the rise in Zanzibar - FT.com

Under the peach arches of Al-Noor charitable agency for the needy just outside Stone Town in Zanzibar, a 24-hour Islamic radio station broadcasts religious guidance.
Female tourists should wear headscarves and cover their knees, says Mohamed Suleiman Ali, director of Radio Al-Noor, echoing the opinions voiced on radio. “It’s too early to fight for an Islamic state because there are several stages to that, but a lot of things are being done contrary to the teachings of Islam,” he says. “There’s no social responsibility; the government keeps producing more [social] freedom.”

More

On this story

IN Africa

Famed for its beaches, more than 170,000 holiday makers come to Zanzibar every year to swim with dolphins and lie beneath coconut trees. But the relaxed way of life that lures tourists to the mainly Muslim islands off the east coast of Africa is coming under threat from a rise in less tolerant forms of Islam. This is tapping into festering discontent over the island’s sovereignty and beginning to influence social mores.
The islands – which make much of their money from tourism – are home to 1m people and more than 2,000 Muslim religious schools. Most of these draw on a long tradition of moderate and Sufi forms of Islam. But these are underfunded and staffed by volunteer teachers. Increasingly, parents are sending their children to better financed alternatives in a process that is beginning to parallel that taking place across a swath of sub-Saharan Africa from Somalia to Mali, where the growing influence of more radical forms of Islam can be felt.

READ MORE
 
Mzee mwanakijiji, this is the western propaganda which is always against Islam and Muslims. The radio presenter was addressing his views and he was not in no way urging people to take any steps against those who act contrary to islamic teachings. Wewe mwenyewe kwa vile ni mkristo ndio maana unashabikia hizo article. ZNZ haijafikia hiyo stage you kusema kuna extremism. Punguza chuki zako na wazanzibar Mzee au tatizo ni nini?
 
Haijafikia huko wakati Makanisa yanachomwa na Wachungwaji wanatunguliwa kwa risasi kama Swala
 
Mzee mwanakijiji, this is the western propaganda which is always against Islam and Muslims. The radio presenter was addressing his views and he was not in no way urging people to take any steps against those who act contrary to islamic teachings. Wewe mwenyewe kwa vile ni mkristo ndio maana unashabikia hizo article. ZNZ haijafikia hiyo stage you kusema kuna extremism. Punguza chuki zako na wazanzibar Mzee au tatizo ni nini?

Ukweli utatuweka huru. Kwenye hili sio 'Western Propaganda'. Makanisa yameanza kuchomwa zaidi ya miaka 4 sasa! Makaburi ya wakristo nayo yamevamiwa, wakristo wanaoishi Zanzibar wanakuwa treated kama '2nd claa citizen. It is impossible to explain hapa hofu waliyonayo wakristo huko Zanzibar. Na nasema haya si kwa kuhadithiwa!
 
.Balozi Seif asema wahusika wasakwe
headline_bullet.jpg
.Hamad Rashid awanyooshea kidole CUF

pole%20padri.jpg

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Padri Cosmas Shayo wa Kanisa la Roman Katoriki Jimbo la Zanzibar wakati alipokwenda kutoa mkonao wa pole kwa uongozi kanisa hilo na familia kufuatia tukio la kupigwa risasi kwa Padiri Ambrose Mkenda.

Ni dhahiri kwamba hali ya amani visiwani Zanzibar ni tete, huku viongozi wakitajwa kuhusisha dini katika harakati za kufikia malengo yanayotajwa kuwa na nia ovu.

Viongozi wa dini, wanasiasa na wanazuoni, wanaelezea umuhimu kwa Taifa kudhibiti uhalifu na kuwachukulia hatua kali wahalifu wanaochochea vurugu, ili kulinda na kuendelea amani visiwani humo.

Zanzibar inakabiliwa na kukua kwa vurugu, hujuma na njama za kutekekeza mali na maisha ya raia wasiokuwa na hatia, dalili zikionyesha wazi kuwepo ‘mkono wa wanasiasa.’

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ANENA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema serikali itahakikisha inawasaka na kuwachukulia hatua za kisheria waliompiga risasi Padri Ambrose Mkenda, Desemba 25, mwaka huu.

Balozi Seif alisema kitendo hicho kimetoa sura mbaya kwa Taifa na serikali, hivyo kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani na umoja wa kitaifa.

“Ni jambo baya na la kusikitisha, tena limetoa sura mbaya kwa Taifa. Serikali haitosita kuachukulia hatua dhidi ya watu waliofanya uhalifu huo,”alisema Balozi Iddi na kuwataka wananchi kuheshimu na kulinda misingi ya amani na umoja wa kitaifa Zanzibar.

Balozi Seif alitoa msimamo huo wa serikali alipokwenda kutoa pole kwa uongozi wa kanisa hilo na nyumbani kwa Padri Mkenda mjini hapa jana.

Alisema SMZ imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika mazingira ya hofu isiyokuwa ya lazima wakati Tanzania ni nchi ya amani.

PADRI WA KATOLIKI AWAONYA WANAOWAPOTOSHA WATOTO

Padri Cosmas Shayo wa Kanisa Katoliki, aliiomba serikali kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu iliyotanda mioyoni mwao, kutokana na matukio ya hujuma yanayojitokeza visiwani humo.

Padri Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa sababu ya utofauti wa kidini, inawajengea msingi wa maisha mabovu watoto hao.

“Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine, tuelewe kwamba Taifa halitakuwa na mwelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye,” alisema.

Padri Shayo alisema serikali inawajibika kufanya uchunguzi wa kina kufuatia kupigwa risasi kwa kiongozi huyo.

Padri Mkenda alipigwa risasi na watu wawili waliokuwa wamepanda pikipiki majira ya saa 1:45 usiku wakati akitoka kumuangalia mgonjwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja akiwa ndani ya gari wakati akisubiri kufunguliwa geti na mlinzi na hakuna kitu kilichoibiwa baada ya kiongozi huyo kupigwa risasi.

Tukio la kupigwa risasi mbili za shingo kiongozi huyo wa kiroho limetanguliwa na mkasa wa kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga wakati akifanya mazoezi ya viungo Novemba 6, mwaka huu.

Hata hivyo hakuna watu waliyokamatwa kuhusiana na matukio hayo. Lakini Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuwatafuta watu waliyofanya mashambulio hayo tofauti visiwani hapo.

HAMAD RASHID AINYOOSHEA KIDOLE CUF

Mbunge wa Wawi (CUF) Hamad Rashid Mohammed, alisema Zanzibar itaingia katika machafuko makubwa endapo hakutafanyika jitihada za haraka kukomesha chuki za kidini zinapandikizwa miongoni mwa raia wake.

Alisema hali si shwari visiwani humo, akiifananisha na ‘yai jeteta’ ambalo kupasuka kwake, kunaathiri watu wote.

Hamad alisema kihistoria Zanzibar ni nchi iliyokuwa na watu wenye uvumilivu wa kidini kwa miaka mingi na hakuna aliyetarajia siku moja watu watatengana na kuhujumiana kwa sababu ya tofauti za kiimani.

Alisema matukio ya kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti Fadhili Soraga na tukio la hivi karibuni Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni baadhi ya matokeo ya chuki hizo zilizopandwa na wanasiasa.

"Hali ya Zanzibar inasikitisha sana, matukio yote mawili ya kujeruhiwa viongozi wa kidini ni jambo la kulaaniwa kwa nguvu zote na inathibitisha kuwepo kwa watu wanaochochea hali hiyo kwa manufaa yao," alisema Hamad.

Alisema kumekuwepo na viongozi wa kisiasa wanashindwa kukemea hadharani jambo hilo kwa sababu wanahusika kuwashawishi na kuwachochea viongozi wa dini kushiriki vurugu hizo.

"Uongozi wa kisiasa umeshindwa kukemea kwa sababu kuna baadhi ya wanasiasa wanahusika, wakati mwingine wanakwenda kwa viongozi wa dini zote kuchochea, lakini ikumbukwe ikitokea vurugu hakuna atakayepona," alisema.

Mbunge huyo asiyetambuliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) alichokitumia kugombea na kushinda kiti hicho, alisema suluhu ya tatizo hilo ni kuanzishwa mjadala wa kitaifa kujadili kuhusu chanzo halisi na namna ya kufikia suluhu ya kudumu.

Pia Hamad alisema hakuna viongozi wenye maoni na nguvu ya kuzuia jambo hilo, kwa vile viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa wanatofautiana kiitikadi.

Katika suala hilo alionyesha kufadhaishwa na msimamo wa viongozi wa CUF kutokuwa na upande wa kusimamia kuhusu Muungano, moja ya madai yanayotajwa kutumika kama kigezo cha kuchochea vurugu visiwani humo.

“Ndani ya CUF kuna watu wanataka Muungano wa Mkataba na wengine wanataka Muungano wa serikali tatu, tofauti na CCM ambao wana msimamo mmoja wa serikali mbili,” alisema.

"Hili ni jambo baya sana kwa viongozi wa CUF kutokuwa na msimamo wa kimaadili, haiwezekani chama kuwa na makundi mawili yenye tofauti ya msimamo, kutokana na hili huwezi kusimamia serikali hata mara moja," aliongeza kusema.

Naye Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alielekeza lawama kwa jeshi la polisi na kusema linafanya kazi kisiasa na kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Profesa Lipumba alisema kama polisi wangefanya kazi kwa weledi na kuachana na kutumika kisiasa, matukio yanayotokea Zanzibar yasingekuwepo kwa sababu wahusika wote wangekamatwa.

Hata hivyo alipinga hoja ya Hamad kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeshindwa kutekeleza wajibu wake katika kuidhibiti hali hiyo.

CHUKI ZILIATHIRI UTENDAJI WA TUME YA KATIBA MPYA

Wakati huo huo, imefahamika kuwa kutokana na kuenea kwa chuki za kidini, wajumbe wa Tume ya kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wanafanya katika hali ya tahadhari, baada ya kukabiliana na matukio ya kibaguzi.

Vyanzo vya habari vimeieleza NIPASHE Jumamosi kuwa baadhi ya wajumbe wasiokuwa waumini wa dhehebu moja wanaofanya kazi kwenye tume hiyo visiwani humo, wanachukua tahadhari kubwa huku wakishindwa kwenda kwenye maeneo yanayoonekana kuwa na watu wenye msimamo mkali wa kidini.

"Mimi mwenyewe ni muathirika wa mambo hayo, lakini siwezi kuzungumzia sana jambo hilo, tunachokifanya ni kutokwenda sehemu tunayoona kuna dalili mbaya," kilieleza chanzo chetu kutoka tume hiyo.

CHANZO: NIPASHE

It is a problem we need to solve before it becomes cancerous.
 
Mzee mwanakijiji, this is the western propaganda which is always against Islam and Muslims. The radio presenter was addressing his views and he was not in no way urging people to take any steps against those who act contrary to islamic teachings. Wewe mwenyewe kwa vile ni mkristo ndio maana unashabikia hizo article. ZNZ haijafikia hiyo stage you kusema kuna extremism. Punguza chuki zako na wazanzibar Mzee au tatizo ni nini?

Mkuu,

Hakuna mwenye chuki binafsi na wazanzibari wala hiyo unayoiita 'western propaganda'.
Ukweli utabaki kuwa ukweli.
Tuache kujifanya kama mbuni anapoona mambo magumu anachimbia kichwa chini kwenye mchanga.
Hili ni tatizo na ni lazima tuliweke hadharani ili lizungumzwe na ikiwezekana lipatiwe ufumbuzi.
Wahenga walisema 'mficha ugonjwa kilio kitamuumbua'.
 
ukiisoma hii kwa undani inaonekana kama kikundi fulani cha watu wachache wanafanya matukio ya namna hii kwa ajili ya kuoandikiza migogoro kwa manufaa yao binafsi......
 
ZANZIBAR hamuiwezi nyie WATANGANYIKA kashindwa yule nabii wenu ameondoka ameiwacha mate yanamtoka ..mm nawashauri kufocus kwenye majanga yenu kwani mapadri na maskofu kila siku yanauliwa huko kwenu na haiwi chochote huyu kukwaruza imekuwa balaa padri padri au wakipigwa huko bara ni sawa kwa vile ndio moja ya tamaduni zenu ikiwemo na ile ya kuchunana ngozi na kuuza viungo vya albino? Laana iwe juu yao isblis shetaan
 
Mzee mwanakijiji, this is the western propaganda which is always against Islam and Muslims. The radio presenter was addressing his views and he was not in no way urging people to take any steps against those who act contrary to islamic teachings. Wewe mwenyewe kwa vile ni mkristo ndio maana unashabikia hizo article. ZNZ haijafikia hiyo stage you kusema kuna extremism. Punguza chuki zako na wazanzibar Mzee au tatizo ni nini?

mkuu unaishi nchi gani ,umeshasahau kuwa siasa kali wanachoma moto makanisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom