EXTRAVAGANZA Safari's za treni ya SGR reli ya kati

Acha uchawa, reli imeishia Dodoma, safari nne kwenda nne kurudi wewe unasema imeleta mabadiliko makubwa kiuchumi wakati haibebi mizigo! Uchumi upi! Uchawa usio na tija.
Mabadilikoo yaweza kuwa chanya ama hasi -- Hasi kulingana na mfano ulioutoa.
 
Hiyo SGR cha mtoto.
Miaka ya mwanzoni ya sabini mabucha yote ya nyama Dar yaliendeshwa na serikali yaani yalikua shirika la umma. Kwenye bucha kulikua mlangoni kuna mgambo na rungu lake, huyu alihusika na ulinzi. Kisha kulikua na karani wa kuchukua order yako kisha anampa mkata nyama, ikishakatwa inapelekwa kwa cashier ambaye anachukua pesa na kukupa nyama yako lakini kuna boss au meneja wa bucha ambaye anawasimamia hawa maskini wanne.
Kipindi hicho mkuu wa mkoa wa Dar ni mheshimiwa Kingunge Ngombale mwana wa Mwiru.
 
Ukiingia kituo cha treni ya SGR Dar es Salaam ili upate tikiti ya shs. 13,000/= utahudumiwa na wafanyakazi kama wanne ukianza na kaunta ya mapokezi ambaye hana kazi.

Ukienda dirisha la tikiti yupo unayemuambia unakokwenda na muda wa treni unayotaka, kisha anaelekeza kwa mwandika tikiti naye anakurusha kwa mpokea malipo ya tikiti na kukurusha kwa mtoa tikiti!

Mlolongo huu umepunguza ukosefu wa ajira ila umepunguza faida kwenye tikiti hiyo ya sh.13,000/= kwenye hatua ya kwanza ukiacha ngazi za umeme zinazokupeleka kwenye malipo na kukushusha.

Hatua ifuatayo ni sehemu ya ukaguzi wa kabegi kako, hapo ipo skana na wakaguzi zaidi ya watatu wanapiga soga, safi sana maana bila soga watasinzia, nao mshahara unatoka kwenye ile tikiti ya sh.13,000/=, hapa angalau waweke malipo ya gharama za ukaguzi kufidia hasara.

Hatua ya mwisho ni baba lao, kusafirishwa kwa treni ya umeme kwa kutumia tikiti hiyohiyo ya sh 13,000/=!Humo ndani ya treni sasa kunawafanyakazi wengi kuliko hoteli ya kitalii ambao utawaona wakipanda treni lakini mpaka unafika Morogoro hautawaona wanachokifanya ndani ya treni, nao mshahara unatoka ndani ya hiyohiyo sh.13,000/= na treni ya SGR bado inapata faida! Kweli Mungu Mkuu.

Asante TRC mmenifikisha salama japo kachupa kangu ka maji ya kunywa na mfuko wangu wa shangazikaja mmeninyanganya(mmeninyang'anya).
Iyo yote ili mpate huduma bora...lakini bado tu mnalalama wakuu!!na serikali muda mwingine haingalii faida tu bali na raia wake mpate ajira...mbona hamna jema!!!!
 
Bila shaka we jamaa umezoea kudandia mafuso ya ndizi uko mikumi ndo maana unashangaa kupewa huduma bora na wadada wa mikumi, sokapo apa!!!!!
 
Hii lot 3 ya SGR, Makutupora kwenda Tabora itakamilika lini
 
Iyo yote ili mpate huduma bora...lakini bado tu mnalalama wakuu!!na serikali muda mwingine haingalii faida tu bali na raia wake mpate ajira...mbona hamna jema!!!!
Mbona likizima hatuwaoni wakilisukuma liendelee na safari, kwenye biashara gharama za matumizi zikiwa chini husababisha bei ya bidhaa kushuka, hivyo na hili nauli zao zingeweza kushuka kwani ni kawaida nauli za treni kuwa za chini kutokana na mabehewa mengi kutumia injini moja.
 
Acha uchawa, reli imeishia Dodoma, safari nne kwenda nne kurudi wewe unasema imeleta mabadiliko makubwa kiuchumi wakati haibebi mizigo! Uchumi upi! Uchawa usio na tija.
Abiria wanasafiri bure? Huoni kila tiketi kuna pesa ya kodi ? Kodi huelewi zinafanya kitu gani kwenye uchumi?

Tiketi inakusanya kodi kila ukatapo

Treni ya Abiria ya SGR ni kitega uchumi cha TRA pia kukusanya kodi
 
Tikiti ya sh 13,000/= ina TRA, wakatishaji wanne!, treni, kundi wahudumu wa ndani ya treni, umeme, maji na uchakavu, fikiria TRC inabaki na nini kwenye hiyo sh.13,000/=?
 
nashauri tu maintanance. vile vidude vya kutundika kakitu pale kwenye seat baafh vimeng'olewa.
Sio utamaduni... watasubiri mpaka utokee uharibufu mkubwa... ndio watumie Bilions kurekebisha...
 
Ushauri wangu kwa TRC ni wapunguze idadi ya wahudumi ndani ya treni bsdals yake watumie Dinning Car(behewa la huduma ya chakula na vinywaji). Wapunguze idadi ya madirisha ya kukatia tikiti na waanzishe tikiti za muda mrefu ambapo msafiri atahitajika kuthibitisha siku na saa ya kusafiri, kwenye skana mhudumu mmoja anatosha.
 
Ukiingia kituo cha treni ya SGR Dar es Salaam ili upate tikiti ya shs. 13,000/= utahudumiwa na wafanyakazi kama wanne ukianza na kaunta ya mapokezi ambaye hana kazi.

Ukienda dirisha la tikiti yupo unayemuambia unakokwenda na muda wa treni unayotaka, kisha anaelekeza kwa mwandika tikiti naye anakurusha kwa mpokea malipo ya tikiti na kukurusha kwa mtoa tikiti!

Mlolongo huu umepunguza ukosefu wa ajira ila umepunguza faida kwenye tikiti hiyo ya sh.13,000/= kwenye hatua ya kwanza ukiacha ngazi za umeme zinazokupeleka kwenye malipo na kukushusha.

Hatua ifuatayo ni sehemu ya ukaguzi wa kabegi kako, hapo ipo skana na wakaguzi zaidi ya watatu wanapiga soga, safi sana maana bila soga watasinzia, nao mshahara unatoka kwenye ile tikiti ya sh.13,000/=, hapa angalau waweke malipo ya gharama za ukaguzi kufidia hasara.

Hatua ya mwisho ni baba lao, kusafirishwa kwa treni ya umeme kwa kutumia tikiti hiyohiyo ya sh 13,000/=!Humo ndani ya treni sasa kunawafanyakazi wengi kuliko hoteli ya kitalii ambao utawaona wakipanda treni lakini mpaka unafika Morogoro hautawaona wanachokifanya ndani ya treni, nao mshahara unatoka ndani ya hiyohiyo sh.13,000/= na treni ya SGR bado inapata faida! Kweli Mungu Mkuu.

Asante TRC mmenifikisha salama japo kachupa kangu ka maji ya kunywa na mfuko wangu wa shangazikaja mmeninyanganya(mmeninyang'anya).
Hiyo 13000,watowa wewe peke yako?Au wako maelfu ya abiria?Tumia akili,hao we zako wamepata ajira,ili mkono uwende Kinywani.Pigq hesabu 13000 mara idadi ya abiria wa kila siku.
 
Iyo yote ili mpate huduma bora...lakini bado tu mnalalama wakuu!!na serikali muda mwingine haingalii faida tu bali na raia wake mpate ajira...mbona hamna jema!!!!
Apige hesabu hiyo 13000 mara idadi ya abiria,ni shiling ngapi.Halafu apige hesabu idadi ya safari kwa siku,halafu apige hesabu ya nauli nyinginezo mara idadi ya abiria ni shilingi ngapi.Hao watu wanne,waliopata ajira,roho inamuuma.Ni roho mbaya tu,aliyonayo mleta uzi.
 
Asante TRC mmenifikisha salama japo kachupa kangu ka maji ya kunywa na mfuko wangu wa shangazikaja mmeninyanganya(mmeninyang'anya
Hapa ni shida, hadi chakula cha mtoto mchanga ni challenge kuingia nacho, sijui Kama ipo sawa au ni mimi?! Naona km tumezidisha complications.

Na restrictions za uzito wa mzigo ni zaidi ya kwenye ndege! Duh😄
 
Tikiti ya sh 13,000/= ina TRA, wakatishaji wanne!, treni, kundi wahudumu wa ndani ya treni, umeme, maji na uchakavu, fikiria TRC inabaki na nini kwenye hiyo sh.13,000/=?
Kila behewa Lina mhudumu 1 ambaye anahudimia abiria 45-78,posho 40,000*1*14=280,000
Wakataji ticket kwa posho labda ya 40,000*4 kwa siku.
Dereva 2*40,000=80,000
Umeme 2,000,000 kwa trip
Wahudumu wengineo 16*40,000
Jumla ya matumizi kwa minadhiri ya trip moja kwenda Moro ni 3,250,000
Kuja mapato baada ya vat ya 16%
12,400*78*14=13,759,200
Tuseme treni imejaza kwa 60%=8,255,520
Unabaki na 5,005,520 kwa trip moja .
Sio hela ndogo kama unavyofikiria.
Kumbuka hao wahudumu wananne wa counter wanahudumia karibia treni zote Tano za Dodoma na morogoro ukija piga hesabu kwa siku unaweza Kuta trip moja tu inakuwa Inaweza lipa posho au mshahara wa siku kwa wahudumu wote kwa treni ya abiria kuanzia dar mpaka Dom namaanisha malipo ya siku
 
Back
Top Bottom