Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 23,251
- 28,406
Ukiingia kituo cha treni ya SGR Dar es Salaam ili upate tikiti ya shs. 13,000/= utahudumiwa na wafanyakazi kama wanne ukianza na kaunta ya mapokezi ambaye hana kazi.
Ukienda dirisha la tikiti yupo unayemuambia unakokwenda na muda wa treni unayotaka, kisha anaelekeza kwa mwandika tikiti naye anakurusha kwa mpokea malipo ya tikiti na kukurusha kwa mtoa tikiti!
Mlolongo huu umepunguza ukosefu wa ajira ila umepunguza faida kwenye tikiti hiyo ya sh.13,000/= kwenye hatua ya kwanza ukiacha ngazi za umeme zinazokupeleka kwenye malipo na kukushusha.
Hatua ifuatayo ni sehemu ya ukaguzi wa kabegi kako, hapo ipo skana na wakaguzi zaidi ya watatu wanapiga soga, safi sana maana bila soga watasinzia, nao mshahara unatoka kwenye ile tikiti ya sh.13,000/=, hapa angalau waweke malipo ya gharama za ukaguzi kufidia hasara.
Hatua ya mwisho ni baba lao, kusafirishwa kwa treni ya umeme kwa kutumia tikiti hiyohiyo ya sh 13,000/=!Humo ndani ya treni sasa kunawafanyakazi wengi kuliko hoteli ya kitalii ambao utawaona wakipanda treni lakini mpaka unafika Morogoro hautawaona wanachokifanya ndani ya treni, nao mshahara unatoka ndani ya hiyohiyo sh.13,000/= na treni ya SGR bado inapata faida! Kweli Mungu Mkuu.
Asante TRC mmenifikisha salama japo kachupa kangu ka maji ya kunywa na mfuko wangu wa shangazikaja mmeninyanganya(mmeninyang'anya).