Experience yangu na cat converter (masega) ya kichina

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,327
Kwanza kabla sijaanza kueleza kisa changu naomba niongee kitu kimoja.

Huwa nashangaa sana unakuta mtu ana IST old model, passo, harrier old, Noah Sr40/sr50, Noah voxy za mwanzoni, Harrier chogo matoleo ya mwanzo, raum, spacio, n.k. anapagawa gari yake ikitolewa masega. Tena kibaya zaidi kama gari yake ikiwa inakunywa mafuta mengi kuliko kawaida. Kichaka kitakuwa masega.

Hizo gari nilizotaja hapo na zingine zinazofanania na hizo, ikitolewa masega kitachoongozeka zaidi ya kelele. Lakini hakuna chochote kitakachotokea kwenye performance. Wala haitowasha taa ya check engine.

Kama una gari kama hiyo na inakunywa mafuta na unawaza sababu ni masega anza kutafuta sababu nyingine ya tatizo lako.

Nirudi kwenye kisa changu.

Week tatu zilizopita kuna mtu alinitext whatsapp ana gari Mitsubishi Outlander ya mwaka 2011. Aliiagiza Japan na muda ameenda kuichukua ilikuwa inawaka check engine.

IMG_20230324_180431.jpg


Akawa amepita kwa watu wawili watatu kufanya diagnosis ikawa inakuja code ya P0420 Cat converter low efficiency.

Basi mimi sikutaka mambo mengi nikamuambia ishu yako naweza kuisolve nikampa na gharama.

Ingawa yeye alitaka tupitie hizo sababu zote zaidi ya 10 ambazo zinaweza kusababisha hiyo shida. Lakini nilijua mwisho wa siku check engine itoke na gari irudi kwenye normal performance.

Basi tukapanga siku, Ila siku moja kabla ya siku tuliyopanga akanicheck akaniambia walifungua exhaust inaonekana wamelamba.masega yote.

Kwa hiyo shida ikawa ishajulikana kwamba masega hayapo. Akaniuliza mimi kama nina masega nikamwambia sina, basi akasema kuna mahali amepata kibuyu cha masega kwa 140k.

IMG_20230324_180921.jpg


Lakini pia sikuacha kumshauri kwamba ipo solution nyingine ambayo ni rahisi na uhakika. Japo bei kidogo iko juu kuliko hivyo vibuyu.

Na nikamuambia kabisa hivyo vibuyu ni vya kichina, Sina tatizo na kununua vitu china na hata mimi mwenyewe ni mnunuaji mkubwa ila shida ni pale mtu anapoangalia urahisi wa bei na kuchukua kitu chenye low quality.

So akaniambia hivyo vibuyu jamaa wamemuambia vimetoka japan😂😂😂. Jamani kununua vitu China siyo dhambi. Vipo vitu vizuri na vipo vitu vya Hovyo.

IMG_20230324_181002.jpg


Lakini pia nikamuambia masega Original siyo bei rahisi. Na kama anabisha aingie hata beforward aulizie kipande cha masega original cha gari yake ni bei gani.

IMG_20230324_181125.jpg


Basi akaamua aende akafunge hicho cha 140k.

Siku iliyofuata asubuhi na mapema akanicheck.

IMG_20230324_181200.jpg


Taarifa ilikuwa ni kwamba amechomelea kibuyu ameendesha gari baada ya muda mfupi taa ya check engine imerudi.

So kilichobaki tufanye kama tulivyokuwa tumeplan.

Basi tukapanga siku

IMG_20230324_181239.jpg


Akaja nikamfanyia kazi. Nikaclear code ikawa imebaki confirmation ya Catalyst monitor kwenye IM readness. Status ilikuwa ni 'Not ready'.

Hii IM readness huwa inaonesha kama ukisolve limetatulika au lah, Kwa baadhi ya matatizo kama hilo la masega ni mpaka uendeshe gari kidogo ndio status inakuwa ready. Na kam kunakuwa na shida inaandika Incomplete.

So tukatoka magomeni mpaka sinza status ikawa ready. Nikamuambia bro gari yako imepona akawa haamini. Tukaendesha mpaka kibaha maili moja na kurudi magomeni Check engine haikuwaka.

Basi ishu yake ndio ikawa imeisha. Nilimtext leo kumuuliza maendeleo lakini naona hayupo Online.


Turudi kwenye vibuyu vya masega.

1679672954198.png


Hivi vibuyu vinaonekana vinafanya kazi kwa sababu wengi gari zao hazina Oxygen sensor ya nyuma. Mfano wa gari nilizotaja pale juu.

Wengi mnaweka mkiamini kutakuwa improvement ya performance lakini kiuhalisia kama gari yako haina o2 sensor ya nyuma ni kazi bure.

Pia kwa ambao gari zenu zina rear o2 sensor na imeibiwa masega. Ukiamua kuweka hicho jitahidi upate ambacho ni kizuri. Otherwise modify O2 sensor ya nyuma endelea kula maisha,

Check engine itapotea na performance itarudi ila kelele zitabaki. Kelele unaweza kutafuta namna nyingine ya kuziondoa.

Alamsiki.
 
Gari ikitolewa masega inakuwa na mlio mbaya sana aisee, na hicho ndio watu wengi kinawakera hadi wanaamua kununua masega. Gari ikiwa na masega inaunguruma vizuri mno
 
Napenda sana mafundi kama wewe.

Binafsi naendesha passo. Nlipigwa sega pia ila ilikuwa ni kwa ruhusa yangu.

Ilikuwa hivi
Ghafla gari iliishiwa nguvu nikiwa natoka musoma to mwanza ikawa haivuki 60 to 80kmh kwenye tambarare miteremko na 40 to 20 km kwenye vipando na slight mpando.

Sasa nilikuwa kama robo ya safari ikabidi niende nayo hivo hivo tu nlitumia 5 hrs safari ya 220km.
Basi nikapeleka kwa fundi akaninunulisha pump mpya haikumaliza tatizo akachomoa oxyge sensor gari ikapata nguvu senso ya passo ipo palepale kwenye engine so ukiito unakuwa umedisconect exhaust na engine inatoka sauti kuuuuubwa.

Akaniambia sege limeziba nikamwambia alizibua akaniambia hata ukizibua litaziba tena hapa dawa ni kununua jipya au kuliondoa ubakie bila sega.. bei ya sege laki3 sikua nazo nikamwambia liondoe.

Wakalitoa then wakaniambia wanitengenezee la kubumba huwa yapo yanauzwa nafikiri ni bati za stanless still nzito wanauza elf 60 nikamwambia sawa wakaniwekea bati 2 ili kupunfuza sauti na muungurumo mbaya.

Binafsi sijaona changez kubwa sana ila tu ulaji umeongezeka japo ni kidogo huwezi kujua kabisa.

Nasafiri sana na hii gari kila week nasafiri 600 to 700 km ukiondoa safari za kazini na kurudi. Sijaona utofauti zaidi ya muungurumo kusikika
 
Gari ikitolewa masega inakuwa na mlio mbaya sana aisee, na hicho ndio watu wengi kinawakera hadi wanaamua kununua masega. Gari ikiwa na masega inaunguruma vizuri mno

Mkuu mlio unatokana na exhaust kukatwa au materials za masega? Kazi ya muffler ni nini kwenye exhaust?
 
Kama masega ya kichina hayahawork bado tunaweza kumodify gari yoyote na kila kitu kikawa sawa
 
Back
Top Bottom