Exclusive: Video ya mlipuko wa bomu Arusha

Exclusive: Video ya mlipuko wa bomu Arusha

Moja ya mafunzo ya police ni kulinda crime scene, lakini baada ya mlipuko, kulichofuatia ni milio ya risasi. Je huo mkutano haukuwa na watu wa usalama pamoja na Policcm?
 
Wakuu.
Nimekutana na hii video nyingine ya mlipuko wa bomu la Arusha.

Bofya hapo chini

EXCLUSIVE VIDEO YA MKUTANO WA CDM ULIOSHAMBULIWA SOWETO ARUSHA - YouTube

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
Dah, bahati mbaya na hii haionyeshi aliyerusha bomu. Lakini angalau inatoa ushahidi kwamba si kweli kwamba mwenyekiti aliondoka eneo la tukio kwa makusudi kama alivyosema Mwigulu, bali alikuwa anachangisha hela kutoka kwa wanachama. Na pia inaonyesha kwamba milio ya risasi ilifuata immediately baada ya bomu kulipuka na si kweli kwamba polisi walipiga risasi baada ya wananchi kuwafukuzia na kuwapiga kama ambavyo wamejitetea. Ni dhahiri kwamba madhara yalipagwa yawe makubwa kuliko haya. Na uamuzi wao wa kupiga risasi tank la mafuta la gari la matangazo ni dhahiri walitaka kutengeneza mlipuko mbaya ambao ungekuwa na maangamizi ya kihistoria. Tunamshukuru Mungu alizuia tank la mafuta lisilipuke.
Inahuzunisha sana, kutazama hii video.
 
Video ya Lwakatare mnaikataa hii Mbowe mnaikubali mnawachanganya watanzania.
Ya Lwakatare ni edited. lakini hii ipo natural. Sema ni scene gani ipo edited hapo?
 
Mohamedi Mtoi asante sana niliingalia vizuri sana hadi mwisho, tukio lenyewe linaanza baada ya lisaa limoja dakika ya ishirini na moja sekunde ya hamsini plus (1:21:50..) Kuna watu ni mashetani zaidi ya shetani mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Hii ndio Video ya Mbowe? Usituchanganye

Published on Jun 20, 2013
EXCLUSIVE VIDEO; VIDEO NZIMA YA MKUTANO WA CHADEMA ULIOSHAMBULIWA KWA BOMU LA KUTUPA KWA MKONO, RISASI PAMOJA NA MABOMU YA MACHOZI. MUDA NI 01:31:18.
• TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZA KUTISHA NA MATUKIO AMBAYO SI MAZURI YATAKAYO ONEKANA.
• BAADA YA MLIPUKO {EVENT OCCUR IN REAL TIME} HESABU MILIPUKO YA RISASI MWENYEWE..., MPAKA POLISI WANARUDI NA KURUSHA MABOMU KUNA ZAIDI YA DK. 5 NZIMA HAZIKUONYESHWA KUTOKANA NA KUZIMIKA KWA CAMERA NA HOFU YA MPIGA PICHA WETU KWA MAANA RISASI ZILIKUWA ZINAELEKEZWA UPANDE ALIPO KUWA.
• HAYA NI MAISHA YA WATU YALIYO POTEA... PAMOJA NA WANAHABARI KUWA WAATHIRIKA NA KAZIA HII... TUNAOMBA SANA VYOMBO VINAVYO HUSIKA VIACHE KUTOA KAULI ZA DHIHAKA.
• MWISHO TUNAWAPA POLE WALE WOTE WALIO ATHIRIKA
 
Moja ya mafunzo ya police ni kulinda crime scene, lakini baada ya mlipuko, kulichofuatia ni milio ya risasi. Je huo mkutano haukuwa na watu wa usalama pamoja na Policcm?

hayo ndo madhara ya kutosikiliza kauli za viongozi. si lukuvi amewaambia?
 
Moja ya mafunzo ya police ni kulinda crime scene, lakini baada ya mlipuko, kulichofuatia ni milio ya risasi. Je huo mkutano haukuwa na watu wa usalama pamoja na Policcm?

Unamaanisha kama hivi?

Policcm.JPG
 
Kumbe bomu lililipuliwa ili msafara wa chadema usifanikiwe .. Angalia lema anamaliza kwamaba watakuwa wanaenda tanapa sakina shamsi hilo ndo lilisababisha .... Kupiga bomu kunyima msafara huoo

that true fact
 
Hahaha .. hii ni uhakika kabisa kuwa chadema imetoa wafuasi wake kafara. Hii dxhambi haitawaacha.
 
Video ya Lwakatare mnaikataa hii Mbowe mnaikubali mnawachanganya watanzania.

Kwa nini mahakama ilimwachia Lwakatare Kama video ya kweli?? Jiulize kwanza..... Mwigulu na siri kwa watanzania kimyaaaaa!!
 
Baada ya mlipuko kutokea hakuna polisi anayeonekana kwenye video.

Walikuwa wapi? Walisepa? Kama walisepa ni nani alikuwa anapiga hizo risasi?

Hata aliyekuwa anaomba msaada kwa mic, hakuomba kutoka kwa wanausalama bali kwa "makamanda".

Kwa tukio kama hili nilidhani polisi wangekuwa mstari wa mbele kuokoa na kuwapa watu directions.

Police are part and parcel of any emergecy service. But they were no where to be seen zaidi ya kudaiwa kupiga risasi.

Ni haki umma kujua hizo risasi zilikuwa na nini. Pia walikuwa wanapiga risasi za kujilinda (self-defence) baada ya kuvamiwa?
 
Back
Top Bottom