Dah, bahati mbaya na hii haionyeshi aliyerusha bomu. Lakini angalau inatoa ushahidi kwamba si kweli kwamba mwenyekiti aliondoka eneo la tukio kwa makusudi kama alivyosema Mwigulu, bali alikuwa anachangisha hela kutoka kwa wanachama. Na pia inaonyesha kwamba milio ya risasi ilifuata immediately baada ya bomu kulipuka na si kweli kwamba polisi walipiga risasi baada ya wananchi kuwafukuzia na kuwapiga kama ambavyo wamejitetea. Ni dhahiri kwamba madhara yalipagwa yawe makubwa kuliko haya. Na uamuzi wao wa kupiga risasi tank la mafuta la gari la matangazo ni dhahiri walitaka kutengeneza mlipuko mbaya ambao ungekuwa na maangamizi ya kihistoria. Tunamshukuru Mungu alizuia tank la mafuta lisilipuke.
Inahuzunisha sana, kutazama hii video.