Exclusive: Video ya mlipuko wa bomu Arusha

Kikwete ndiye kinara na mratibu wa tukio hili. Baada ya tukio polisi wake wakaishia bila kujali usalama wa raia!!
 
Kwa hii bundle yangu ya 60MB itakuwa ngumu, ngoja baadae niweke unlimited ili niiangalie kwa makini kabisa
 
Hakuna hofu, hiyo ndiyo style ya CCM kukata roho! Wako hoi na mahututi! Dawa zote walizokuwa nazo za udini, ukanda, ukabila na ugaidi hazifanyi kazi tena! Wako ICU wakipumulia mashine ya polisi na mahakama!! Tumaini lao la mwisho sasa ni mabomu!! Lakini dawa hii nayo haitafanya kazi. Kaburi linawasubiri kwa hamu!!!
 
"beyond reasonable doubts" bado hii video haijaonyesha kwa uwazi kama wengi wanavyosimulia, hivyo bado nitareserve haki ya kumake up akili yangu ya nani ni mshiriki kamili na chanzo cha mripuko. Dunia ya sasa hasa siasa huwafanya good people do bad things kwa sababu the system has let them..Lisilo na doubt ni walioumia na kufariki dunia ni wanyonge wapenda mabadiliko ya kweli ya nchi yao. Damu yao haitamwagika bure, iko siku ukweli utajulikana.. Ninacondem yeyote anaechochea na kujihusisha na uvunjifu wa amani.. Vile vile nacondem kauli ya Pinda ya "wapige tu", imekkosa utu, uadilifu na ihsani ya ubinaadamu na dhamana ya uongozi katika so called democratic country. Serikali haiwezi kuchoka na changamoto za wananchi, na ndio maana wanalipwa mamilioni ya pesa za walipa kodi, si justification ya blanket statement tena bila ya kiwango gani cha amri ya wapoge alioitoa bungeni against wananchi. Hata vitani kuna rule of engagement seuze kwa raia wako..
 
Mkuu Mtoi, pamoja na kwamba tunamajonzi, lakini lazima nikubali, kawimbo kamenikuna sana. Asante!!
 
mwanzoni hotuba ya mh.lema ya kusisimua ikikolezwa na kamanda wa anga mwisho damu duh,.. magamba?????
 
Jaman watanzania wenzangu, hembu tukumbushane kidogo jambo hili... "TANZANIA NI NCHI YENYE UTAJIRI MKUBWA SANA WA RASIMALI IKIWEMO GESI NA NISHATI ZNGNE. KWANINI TUSIFIKIRI KWAMBA JAMBO HILI HALIHUSIANI NA SIASA? WAPO WANAODAI KUWA NA UHAKIKA NA USHAHIDI WA JAMBO HILI JE NI KWELI AU NI KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA?" Naombeni mawazo yenu wakuu.
 
Mawazo yangu mimi ni kwamba, hii kitu imekua planned na kutekelezwa na sisi wenyewe, utajiri wetu na Cdm vina uhusiano gani?
 
Jaman watanzania wenzangu, hembu tukumbushane kidogo jambo hili... "TANZANIA NI NCHI YENYE UTAJIRI MKUBWA SANA WA RASIMALI IKIWEMO GESI NA NISHATI ZNGNE. KWANINI TUSIFIKIRI KWAMBA JAMBO HILI HALIHUSIANI NA SIASA? WAPO WANAODAI KUWA NA UHAKIKA NA USHAHIDI WA JAMBO HILI JE NI KWELI AU NI KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA?" Naombeni mawazo yenu wakuu.

Sio swala la kuhisi, ameletwa Kachero aliyebobeaanaitwa Chagonja, nadhani muda si mrefu watapatikana waliotenda unyama huu. Wala msiwe na wasiwasi wowote. Kama kwa mauaji ya RPC Mwanza walitumia muda mfupi kumkamata aliyehusika itakuwaje kwa hao wa Kanisani , na kwenye Mkutano wa CHADEMA?

Subirini tu kidogo maana kama serikali ilitwambia maisha bora kwa kila Mtanzania na tumeanza kuyaona kwa ziara za JK, Ujio wa maraisi wakubwa wakubwa wa dunia hata akina Bush wallishastaafu lakini anarudi rudi tu tutanufaika wala msiwe naharaka yoyote. OBAMA atatuletea vitanda na magodoro ya kulalia maana Bush alishatuletea net za mbu.
 
Kama video ndo hii anayoisemea Mbowe haitawatia hatia Police kama tulivyokuwa tunatarajia. Kwa asiyejua anaweza ona kuwa ni kweli walihusika lakini kwa ajuae hii haina tofauti na Video zingine ambazo zime-editiwa kwanza. Je unatakakutuaminisha kuwa hiyo kamera ilikuwa na uwezo wa kuchanganya picha kama inavyojionyesha?. Nasema wazi hata iliyokuwa inamhusu Lwakatale ilionyesha uhalisia kuliko hii. Kama hii itaaminiwa na kufanyiwa kazi basi Lwakatale yeye ahukumiwe kabisa kwa kushiriki kosa. Na kadiri siku zinavyozidi tutachukulia kuwa inatumika Pro- video kwa kucheza na tukiao.

Ni waulize swali, kwa wale wanaoangalia film ya mateso ya Yesu, je mwaamini ni kweli ndivyo ilivyofanyika?. Nawambia sasa kuwa watalaamu wametumia matukio kutengeneza video zile. Ingekuwa rahisi sana kushawishi watu kuamini kama ingetolewa siku ile ile ya tukio.
 
Najua kuna mijitu imekuja imetoa mimacho kwenye hii video ili iwapunguzie kihoro walichonacho,
ili kuujua ukweli CDM walionao,wamekuta hola hakuna sura ya mapolisi gaidi,bado wakati wake hii
lengo ni kuwafanya mjue nini kilitokea,lakini ile ya magaidi mapolisi endeleeni kukaa na pressure zenu,
mpaka wakati mwafaka na mahali mwafaka utatolewa.Pole Chagonja na wenzio waliokutuma waambie
kibarua cha safari hii kigumu'

Nimekupa like 1000...
 
Video ya Lwakatare mnaikataa hii Mbowe mnaikubali mnawachanganya Watanzania.

Si hata nyie mlishindwa ipromote single yenu...hata kwa kupewa coverage kubwa ya mahakama bado mkajizoazoa.
 
Back
Top Bottom