Mimi ningependa kujua kama Zitto anaujua mshahara wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mshahara wa makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ule wa raisi wa Zanzibar.
Na kama anajua mishahara yao, yeye kajuaje? Maana sisi wengine au nijiongelee mwenyewe, mimi sijui na nimekuwa nikitaka kujua tokea mwaka 2007 na mpaka leo hii bado sijajua na sijakutana na mtu anayejua kwa uhakika.
Na kama nikipenda kujua ni wapi pa kwenda? Na kama mishahara ya hao waheshimiwa haiwekwi wazi, sababu ya/za kutokuwekwa wazi ni nini/zipi hasa maana kwa ufahamu wangu sisi walipa kodi ndiyo tunalipa mishahara yao, na sisi ndiyo waajiri wao hivyo kimsingi tunastahili kujua tunawalipa kiasi gani kwa kazi wanazozifanya.
Nina mengi sana ya kusema na kuuliza kuhusiana na hili suala ila kwa kuanzia nadhani haya yanatosha kwa sasa. Nategemea Zitto atajibu maswali bila kukwepa wala kuurapa.