Ex wangu alivyonitesa leo ananililia

Ex wangu alivyonitesa leo ananililia

Miaka ya nyuma nilikuwa na msichana wangu mweupe(ugonjwa wangu aisee) Ni msichana ambae nilimpenda sana kwa sababu wenge la mapenzi ndo alinitoa yeye.In short nae alikuwa mzuri sana(according to my eyes) mpaka ikafika point akawa anavuma pale chuoni.

Nakumbuka ilipofika mwaka wa pili mwenzangu akawa na mambo mengi mimi nipo bize na masomo.Ilifika point akawa anafuata na gari kila ijumaa pale chuoni na jamaa fulani wa makamo.

Nikimuuliza mwenzangu anajibu kuwa yule ni uncle wake huwa anampenda sana na pia anafanya kazi pale mlimani city mall hivyo kila ijumaa anamchukua ili aende kwake na mke na watoto.Kwa uzoba wangu ilinibidi nikubali tu japokuwa kuna kitu kilikuwa kinanistua moyoni nikawa nakikemea.

Yule dada kwa kweli aliuwin moyo wangu kwa sababu kila sababu aliyokuwa akiniambia nilikuwa naiubali hata kwa kujilazimisha.

Uncle nilianza kumsuspect kwa sababu alikuwa anamnunulia zawadi nyingi sana including laptop,
na mazaga mazaga akawa ananitenga nikiuliza anakuwa mkali,Niwe tu muwazi mwaka wa pili nilijikuta matokeo yangu ya UE yamekaa vibaya(graph la matokeo likawa limeshuka),marafiki zangu wakawa wanaona ninavyonyanyasika kimapenzi.Ki ukweli alinipenda ila kosa langu kubwa ni kuwa nilikuwa sina hela(mwanafunzi mwenzie).

Lile li uncle likawa lipo bize nae mpaka usiku likawa linampigia simu.Kuna rafiki yangu mmoja ambae tulisoma nae shule ya msingi tumekutana pale chuo akanikalisha chini na kunipa ushauri nikubali kuwa huyu msichana kashatekwa na wajanja coz hata huyo uncle wake kuja kufuatilia kupitia kwa mdogo wake mchumba wangu akaniambia hawana mjomba mwenye jina kama hilo na pia hawana mjomba anaefanya kazi mlimani city.

Nilianza kujifunza kukubali kuwa nimeshatemwa taratibu kwa msaada na usimamizi wa rafiki yangu akaanza kunikeep bize na masomo na mazoezi mpaka ikafika point nikakubali kuwa huyu sio wangu japokuwa kuna wakati alikuwa ananimiss na kujirudi kiuongo uongo ila upendo nikaanza kuuvua taratibu nikajiapiza sitaki mbwa yeyote wa kike aharibu furaha,masomo,moyo na hata afya yangu.

Niliweza kumove on ila niliapa kutafuta pesa kwa juhudi ili nilipize kisasi(japokuwa niliona upuuzi kulipa kisasi).Nilidelete kila kitu kwenye ubongo wangu kinachomhusu yeye nikawekeza nguvu kwenye kutafuta maisha

SABABU YA KUANDIKA:Baada ya kupotezana kwa muda mrefu mwenzangu kumbe ananitafuta kwa muda mrefu sana na kubahatika kunipata kupitia namba ya simu,White ameomba kuonana na mimi bahati mbaya mi nipo mkoa nje ya Dar ikabidi kumuonesha mi mbweha nikamfanyia booking ya Go and return fast jet ili aje huku nilipo tuonane nae nikamuandalia mtu wa kumpokea airport(nina gari yangu Carina TI inafanya service ya Tax) amefikia Hotel fulani kubwa hapa Mkoa nilipo, nimeenda kuonana nae kachoka mbaya ule uzuri wote aliokuwa nao umepungua.

Mbaya zaidi nikatoka nae out mpaka kwenye kitimoto tukapiga story nyingi mi nikamuambia kuwa nimeshaoa hivyo sipo tayari kufanya chochote kibaya nae kwa sababu mi sitaki kuumiza wasio na hatia.

ALILIA SANA AISEE ANAJUTIA MAZOMBIE ALIYONIFANYIA ANATAMANI MOVIE IRUDIWE ILI ASINIUMIZE NA ANATAMANI AWE MKE WANGU ILA NDO HIVYO TENA ANAISHIA KULIA LIA TU HAPA.Mbaya zaidi nimemkatia tiketi ya go n return ili nimuumize kidogo kwa alichonifanyiaga mpaka ikapelekea mimi kudrop kiufaulu.
UJUMBE WANGU:WASICHANA PENDENI WATU BILA KUANGALIA KIPATO CHAO,KWENYE LIFE KUNA UPS N DOWN TAJIRI WA LEO ANAWEZA AKAWA MASIKINI WA KESHO AND VICE VERSA.
USIMJUDGE MWANAUME ENZI ZA UTAFUTAJI WAKE KWA SABABU BADO ANAFIGHT HUJUI ATAPATA NINI?
Wale ma anko wanaopitia wanachuo na kuwatafuna tafuna huwa wanalipizia jinsi walivoumizwa na wao enzi hizo. So the circle continues...
 
Shida ya hawa viumbe hawezi kukaa na mabwana zao wakajenga future zao, huwa wanaona wanachelewa maisha na kuwahi kutafuta waliofanikiwa baadae giza likiwashinda wanajirudi. So sad!

Nimekuelewa zaidi ulivyoelezea kuna mwanamke alizingua kipindi cha chuo sasa hivi ana mtoto kazalishwa mtoto miaka mitatu anasema nimuoe mimi namwangalia nacheka tu
 
Kuna ka ujumbe nilikapata jana kalinifurahsha na kunichekesha sana, NANUKUU

"Kwa wale waliowapoteza ndugu na Marafiki na wanataman wapate mawasiliano nao, usihangaike we tafta tuu pesaa, watakutafta wenyewe, wapi watapata namb zako? Hilo sio jukumu lako"

Mwisho wa kunukuu
Umenichekesha na mm hase bonge la ujumbe usitafute mtu tafuta pesa tu
 
Kuna Mwanamke nilikua nae Juzi hapa Tumetoka kuonana sehemu Akataka Nimpe hela ya Nauli Wakati huo Sina Sikumpa Akamaind Sana Akasema Eti Nimemdharisha Akaniacha Eti Hawezi Kuwa Na Mimi Kisa Simpi Hela Bhana Namuonea Huruma Sana Kwani Yajao Yanafurahisha
 
Kuna Mwanamke nilikua nae Juzi hapa Tumetoka kuonana sehemu Akataka Nimpe hela ya Nauli Wakati huo Sina Sikumpa Akamaind Sana Akasema Eti Nimemdharisha Akaniacha Eti Hawezi Kuwa Na Mimi Kisa Simpi Hela Bhana Namuonea Huruma Sana Kwani Yajao Yanafurahisha
Mkuu alikuona uko na 30 Age anajua huwezi kutusua
 
Aisee , hii story haina tofaut na story ya kangu , kama kwamba vile umenicopy my real life story na ku paste kwako

Mm pia yalinikuta na kisingizio kilikua hiko hiko uncle
 
Nimeona nitie neno hapa
Huu ujumbe ni wakweli kabisa
Kuna ka ujumbe nilikapata jana kalinifurahsha na kunichekesha sana, NANUKUU

"Kwa wale waliowapoteza ndugu na Marafiki na wanataman wapate mawasiliano nao, usihangaike we tafta tuu pesaa, watakutafta wenyewe, wapi watapata namb zako? Hilo sio jukumu lako"

Mwisho wa kunukuu
 
Ulianza mapenzi chuoni kama hivi bado sana kwenye game mimi demu aliyenifuta wenge na kujuta kupenda ni wakati nipo kidato cha pili ila sasa hivi akiniona ananiomba selfie
Haya mambo ni psychology tu hakuna anayewahi wala anayechelewa ukipenda umependa na ukiumizwa unaumia vile vile
 
Back
Top Bottom