Habari wana jamii?
Naombeni ushauri wakuu. Mwaka juzi niliwahi kudate na mwanaume tuliyekaribiana umri sana. Baada ya miezi sita tuliachana na kila mtu akashika hamsini zake.
Mwaka huu mwezi wa sita tulikutana naye, akafurahia kukutana nami. Tukaanza kuwasiliana. Akaniomba urafiki. Nikaona si mbaya.
Tumekuwa marafiki kwa miezi miwili sasa. Nikipata shida hata usiku wa manane anakuja na kunisaidia.
Pia kwa mahusiano yake ana-date wadada watatu kwa mpigo. Nilipomwuliza kwanini anachezea wasichana wa watu alinijibu kuwa bado hajapata mtu sahihi wa kutulia naye.
Jumamosi iliyopita yameibuka ya ajabu. Ex anataka kupasha kiporo nami, nikamkatalia na kumwelewesha kuwa lazima kuwa na msimamo. Kama ameniacha tupashe viporo hili iweje?
Toka Jumamosi mwenzangu urafiki ni wa kusua sua. Nami nampenda kama rafiki yangu. Wakuu nipeni ushauri wapi nakosea.