Ewura yatamba Kumaliza uchakachuaji kwa kupandisha bei ya mafuta ya taa, je ni haki?!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ewura yatamba Kumaliza uchakachuaji kwa kupandisha bei ya mafuta ya taa, je ni haki?!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by namimih, Jan 11, 2012.

 1. n

  namimih Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepitia mtandao wa mwananchi na kukutana na kichwa cha habari kisemacho "EWURA YATAMBA SASA UCHAKACHUAJI HISTORIA" kwa kweli nilianza kuona hawa jamaa wapo makini angalau kuwa wamemaliza hilo tatizo la mafuta, lakini kwa kweli nilipoanza kusoma na kukutana na maelezo ya kuwa uchakachuaji umemalizwa kwa kupandisha mafuta ya taa kwa kweli nimetaka kulia kwa hasira, hata wenzangu niliokuwa nao waliniuliza nimepatwa na nini ghafla. Wenzangu kwenye jamvi hili naomba niulize au nieleze vyovyote itakavyo fahamika, ina maana mafuta ya taa yamepandishwa tu kwasababu ya kupunguza uchakachuaji, kweli hii sababu inaingia akilini, na kama vile haitoshi mamlaka nzima ambayo ilitakiwa imalize tatizo hilo kwa njia yenye kuleta unafuu kwa wananchi wao ndiyo kwanza wanaongeza ugumu wa maisha na bado eti WANATAMBA, je huko nyumbani watu wanaichukuliaje hii.
   
Loading...