Pole rafiki yangu Felix Ngamlagosi. Kichwa chako tayari kimekwishaliwa. Kwa nini? Business as usual? Mpaka kichwa cha DG kiliwe ndipo watu wapate akili. Niwashauri MDs wanaoongoza TANESCO, PPRA, EWURA, STAMICO, TMAA, TPA, TCRA, TCAA, TANROADS, NHC, TIC na TBS. Maeneo yenu ya kazi (nishati, madini, viwango, manunuzi ya umma, mawasiliano, uchukuzi, ujenzi, uwekezaji) yalikuwa strategic investment targets za kundi la akina Rostam Aziz wakati wa tawala za Mkapa na Kikwete. Kundi hilo lili-adulterate sera, sheria na kanuni zinazoongoza maeneo hayo ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha ufisadi wao unalindwa na sheria. Mnachoweza kufanya kwa sasa ili kudhibiti vichwa vyenu kuendelea kuliwa bila kuwa na hatia ni [board na management zenu] kuanzisha review ya sheria zinazokuundeni na kukupatia mamlaka ya kufanya shughuli zenu, na kisha kupendekeza mabadiliko ya sheria kupitia wizara mama zenu. Vinginevyo, viti vyenu vitaendelea kuwa vichungu. Pole Felix. Nakumbuka mwaka 2000 (enzi za waziri wa maji Nkangaa) tulikula good time pale Den Haag, Uholanzi.