EWURA yasitisha bei mpya za mafuta

EWURA yasitisha bei mpya za mafuta

Yani hata kama ulikuwa huoni umuhimu wa katiba mpya, kwa haya yanayoendelea lazima uone umuhimu wake.
 
Punguza kodi yatashuka bei.Dar 2500 zambia 1200 na yanapitia Bandari yetu plus Kusafirishwa hadi zambia.
Wenzetu wa mipakani fulltank zao wanawekea nchi jirani
 
Director: Serikali ya JMT
Producer:Serikali ya JMT
Make-up artist:Serikali ya JMT
Starring:Serikali ya JMT
Dereva:Serikali ya JMT
Lighting Director: Serikali ya JMT
Sound:Serikali ya JMT
 
Hili zuio si walitakiwa walitoe mapema kabla ya kuruhusu hiyo bei kuanza kutumika leo!
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kusitishwa kwa bei mpya za mafuta zilizotangazwa jana ambazo zilipaswa kuanza kutumika leo tarehe 1 Septemba.
Serikali imeelekeza bei za mafuta za mwezi uliopita kuendelea kutumika.

======

Serikali imeelekeza EWURA kusitisha bei mpya za mafuta zilizopaswa kuanza kutumika leo Septemba 01, 2021 na zile ambazo zilikuwa zinatumika mwezi Agosti ziendelee kutumika

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema, "Serikali imeunda Timu Maalum kwa ajili ya kuangalia bei zinavyopangwa na viashiria mbalimbali vinavyosababisha bei iendelee kwenda

Ameongeza, "Bei za zamani zitaendelea kutumika mpaka pale Timu Maalum ambayo imeundwa na Serikali kupitia na kutoa majibu"
Huu ni uthibitisho kuwa haya mambo hayana na uhusiano na sababu za soko bali ni typical hujuma za kisiasa tu kwa maumivu ya wananchi...!!
 
Sawa mama lakini ugeukie pia mafuta ya kula . Bei imepanda ambavyo haijawahi tokea.
 
Ni siasa au uhalisia ndio umeazingatiwa?

Tujipe muda kujua nini kime-determine bei kama ni professionalism au ni siasa inahusika.

Bei inaweza kupanda au kushuka kutegemeana na bei katika soko la dunia au sera zetu za kikodi humu nchini.

Wacha tusubiri.
Hakuna sababu ya kujipa muda, hapo hakuna cha soko la dunia wala la Kinondoni, kama jana walipandisha wao, na leo wameshusha wao, maana yake wao ndio walioamua yapande, nothing else.
 
Amepiga marufuku kwani yanachimbwa uwani kwake!
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kusitishwa kwa bei mpya za mafuta zilizotangazwa jana ambazo zilipaswa kuanza kutumika leo tarehe 1 Septemba.
Serikali imeelekeza bei za mafuta za mwezi uliopita kuendelea kutumika.

======

Serikali imeelekeza EWURA kusitisha bei mpya za mafuta zilizopaswa kuanza kutumika leo Septemba 01, 2021 na zile ambazo zilikuwa zinatumika mwezi Agosti ziendelee kutumika

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema, "Serikali imeunda Timu Maalum kwa ajili ya kuangalia bei zinavyopangwa na viashiria mbalimbali vinavyosababisha bei iendelee kwenda

Ameongeza, "Bei za zamani zitaendelea kutumika mpaka pale Timu Maalum ambayo imeundwa na Serikali kupitia na kutoa majibu"
Hii nchi ina sarakasi za kishamba sana !
 
Back
Top Bottom