EWURA yasitisha bei mpya za mafuta

EWURA yasitisha bei mpya za mafuta

Nawaza tu bei mpya ilishaanza kufanya kazi
Ebu tuone kesho itakavyokuwa

Ila hii nchi hii ni ngumu sana
Wapo watakaogomea kushusha...

Tamko limetoka lakini bado bei naziona zile zile 1511
 
Wakuu EWURA imetangaza kusitisha bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Septemba Mosi 2021, na kuagiza bei za mwezi Agosti kuendelea kutumika.

Mama ameamua kuwa mkali kwa EWURA akiwachekea mambo yatakuwa magumu.
Kwani EWURA si wanatumia vigezo vilivyo wazi, sasa hundred clocks anatumia vigezo gani?
 
Kazi kweli kweli...kama dar yalifika 2500 sjui mikoa ya mbali kama mara ,kigoma na kagera yangeuzwaje
 
Wakuu EWURA imetangaza kusitisha bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Septemba Mosi 2021, na kuagiza bei za mwezi Agosti kuendelea kutumika.

Mama ameamua kuwa mkali kwa EWURA akiwachekea mambo yatakuwa magumu.
Mimi Jana nimepita sheli saa 11 nikakuta mafuta yanauzwa 2400 nimerudi saa mbili nakuta yanauzwa 2490 ina maana leo nikienda nakuta yanauzwa 2400 sijui na kesho itakuaje.

Swali la kujiuliza ni Je nani anapanga Bei ya Mafuta?Kuna watu wana PBPA ambao nafikiri ndo wanaagiza mafuta kwa niaba ya wauzaji wa jumla na kuna EWURA sasa sijua BEI inapandia kutoka kwa waagizaji nje au ni hapa nchini michezo inafanyika.

Anyways,Nafikiri mama anapaswa kuangalia zaidi ya EWURA sasa.

Ushauri wangu,Wanunuaji wa mafuta waruhusiwe kutafuta mafuta POPOTE kwa bei yoyote mradi viwango vya ubora vifikiwe.TIPER ianze kufanya kazi kama REFINERY ili tupate faida ya Products nyingine za CRUDE OIL.
 
Back
Top Bottom