EWURA imesitisha kufuta leseni ya Kampuni ya Mansoor Oil Industries Limited (MOIL) baada ya kuomba msamaha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,563
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesitisha kufuta leseni ya Kampuni ya Mansoor Oil Industries Limited (MOIL) baada ya kuomba msamaha, hivyo kulipishwa faini ya Sh milioni 10.

Aidha, imesema kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Olympic Petroleum lipo pale pale baada ya kukaidi maelekezo, japo kampuni hiyo ipo tayari kuomba msamaha, hivyo kuamriwa hadi jana saa 11 jioni iwe imesambaza mafuta katika maeneo waliyoelekezwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godfrey Chibulunje alisema Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya upatikanaji mafuta nchini.

Chibulunje alisema kutokana na taarifa za uhaba wa mafuta maeneo mbalimbali nchini, wamekuwa wakifuatilia hali ya upatikanaji wake kwa kutumia wakaguzi wake na kupata taarifa kutoka kwa uongozi wa wilaya au mkoa.

Alisema katika maeneo hayo yaliyotambulika kuwa na uhaba wa mafuta, Ewura ilielekeza vituo vya mafuta kununua petroli na dizeli kutoka katika kampuni zikiwamo MOIL, Total, Oryx, Star Oil na Olympic Petroleum.

“Hadi kufikia Juni 27, mwaka huu, Ewura iliwezesha mafuta kufikishwa au kupakiwa kutoka katika maghala kuelekea katika maeneo yenye uhaba wa mafuta. Maeneo hayo ni Ifakara, Ngara, Chato, Sirari, Geita, Kasulu, Tabora, Vwawa, Nkasi na Chunya,” alisema Chibulunje.

Aliongeza kuwa mafuta mengine yalitegemewa kupakiwa jana kwenda katika maeneo yaliyobainika kuwa na uhaba wa mafuta ambayo ni Geita, Biharamulo, Kibondo, Ilula, Iramba, Igunga, Kondoa, Kibaigwa, Mpwapwa, Kibondo, Kongwa, Mbande, Mvumi, Mlali, Manyoni na Kyela.

Awali alisema, Juni 27 mwaka huu, maghala ya mafuta yalikuwa na jumla ya lita 92,435,539 za petroli zitakazotosheleza matumizi ya mafuta hayo kwa takribani siku 25 na lita 147,398,593 za dizeli zitakazotosheleza mahitaji ya mafuta hayo kwa takribani siku 29.

“Vile vile maghala ya mafuta yana jumla ya lita 98,077,624 za petroli na lita 147,404,384 za dizeli kwa ajili ya soko la nje. Jumla ya kampuni 22 zina hifadhi ya mafuta ya petroli katika Bandari ya Dar es Salaam, huku kampuni 27 zikiwa na hifadhi ya mafuta ya dizeli,” alifafanua.

Akizungumzia uagizaji wa mafuta kwa Septemba, alisema shehena ya petroli yenye tani 39,771 sawa na lita 52,357,820 inategemewa kuwasili nchini kesho. Pia shehena nyingine yenye tani 38,759 sawa na lita 51,025,540 inategemewa kuwasili Julai 14 mwaka huu.

“Kwa ujumla, inategemewa kuwa na lita 103,383,360 za petrol zitapokelewa nchini Julai 2020. Kiwango hiki ni sawa na asilimia 89 ya matumizi ya petroli kwa Julai 2019 na asilimia 94 ya wastani wa matumizi ya Juni 2020,” alisema.

HabariLeo
 
Kishindo Cha Awamu Ya Tano
Serikali Ni Tajiri Sana
Hakuna Wa Kuitisha Serikali
Ukitumiwa Na Mabeberu Ujue Wazi Wazi Hatua Nzuri Sana Huna
 
Nape Nimemsamehe ingawa kusamehe kunaumaaaaa.

Kamishna wa Zimamoto na wenzake nao nimewasamehe wanahangaika sana mpk kutuma msg usiku wa manane ila nimewasamehe.

Nao Ewura wakaona waige beat la kusamehe,safi sana.
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesitisha kufuta leseni ya Kampuni ya Mansoor Oil Industries Limited (MOIL) baada ya kuomba msamaha, hivyo kulipishwa faini ya Sh milioni 10.

Aidha, imesema kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Olympic Petroleum lipo pale pale baada ya kukaidi maelekezo, japo kampuni hiyo ipo tayari kuomba msamaha, hivyo kuamriwa hadi jana saa 11 jioni iwe imesambaza mafuta katika maeneo waliyoelekezwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godfrey Chibulunje alisema Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya upatikanaji mafuta nchini.

Chibulunje alisema kutokana na taarifa za uhaba wa mafuta maeneo mbalimbali nchini, wamekuwa wakifuatilia hali ya upatikanaji wake kwa kutumia wakaguzi wake na kupata taarifa kutoka kwa uongozi wa wilaya au mkoa.

Alisema katika maeneo hayo yaliyotambulika kuwa na uhaba wa mafuta, Ewura ilielekeza vituo vya mafuta kununua petroli na dizeli kutoka katika kampuni zikiwamo MOIL, Total, Oryx, Star Oil na Olympic Petroleum.

“Hadi kufikia Juni 27, mwaka huu, Ewura iliwezesha mafuta kufikishwa au kupakiwa kutoka katika maghala kuelekea katika maeneo yenye uhaba wa mafuta. Maeneo hayo ni Ifakara, Ngara, Chato, Sirari, Geita, Kasulu, Tabora, Vwawa, Nkasi na Chunya,” alisema Chibulunje.

Aliongeza kuwa mafuta mengine yalitegemewa kupakiwa jana kwenda katika maeneo yaliyobainika kuwa na uhaba wa mafuta ambayo ni Geita, Biharamulo, Kibondo, Ilula, Iramba, Igunga, Kondoa, Kibaigwa, Mpwapwa, Kibondo, Kongwa, Mbande, Mvumi, Mlali, Manyoni na Kyela.

Awali alisema, Juni 27 mwaka huu, maghala ya mafuta yalikuwa na jumla ya lita 92,435,539 za petroli zitakazotosheleza matumizi ya mafuta hayo kwa takribani siku 25 na lita 147,398,593 za dizeli zitakazotosheleza mahitaji ya mafuta hayo kwa takribani siku 29.

“Vile vile maghala ya mafuta yana jumla ya lita 98,077,624 za petroli na lita 147,404,384 za dizeli kwa ajili ya soko la nje. Jumla ya kampuni 22 zina hifadhi ya mafuta ya petroli katika Bandari ya Dar es Salaam, huku kampuni 27 zikiwa na hifadhi ya mafuta ya dizeli,” alifafanua.

Akizungumzia uagizaji wa mafuta kwa Septemba, alisema shehena ya petroli yenye tani 39,771 sawa na lita 52,357,820 inategemewa kuwasili nchini kesho. Pia shehena nyingine yenye tani 38,759 sawa na lita 51,025,540 inategemewa kuwasili Julai 14 mwaka huu.

“Kwa ujumla, inategemewa kuwa na lita 103,383,360 za petrol zitapokelewa nchini Julai 2020. Kiwango hiki ni sawa na asilimia 89 ya matumizi ya petroli kwa Julai 2019 na asilimia 94 ya wastani wa matumizi ya Juni 2020,” alisema.

HabariLeo
Gari 1 tu tank tena trip 1 ya local inatosha sana kulipa hii faini, Nimefanya kazi sana kwenye hii kampuni, Gari za matank ya mafuta zinaingiza pesa sana kuliko sheli ndio maana jamaa hana sheli nyingi nchini na hana time nazo ila ana tanks za kutosha local, translocal na transit...
 
Back
Top Bottom