Ewe mume usiruhusu mkeo kuwa na "dressing-table"

Bangi naisikia tu sijawahi iona hata hayo madawa pia ila wewe mwanza mpaka hapa unajua mengi ya wadada mpaka kutushinda wahusika wenyewe
Hé hé hé ! Na siyo Mwanza mjini. Kolomije ndani
 
Ukishakuwa na pesa, hivyo vitu hata huna muda wa kuvifuatilia... wewe unajua kutoa pesa tu... watoto wamevaa nini, mke kavaa nini, mara nyingi unakuwa huna habari na hizo issue.. wewe unaumiza kichwa usifilisike... hao unaowahudumia wao ndiyo watafanya hayo yote...

cc: mahondaw

Ofcourse sweetheart..
Namshukuru sana Mungu for Smart911 love you are responsible father and husband as well
Nakupenda sana S wangu[/USER]
 
Ushamba wako tu!
Mm ninapenda mke ambaye yupo simple and has natural look. Siyo yule ambaye akitokwa jasho unampotea. Akiwa kwenye kadamnasi akapigwa jua unaweza kupishana naye usimfahamu. Manake anakuwa kama dubwasha fulani hivi
 
Aliyekwambia mwanamke akiwa na dressing table hawi natural nani?
 
Kuanzisha drama za kishamba, ili kuonekana wewe ndio mkuu, ni upopoma. Ukuu unakuja automatically, ukisikia mwanaume anasema 'unajua mimi ndio baba' jua huyo keshapoteza mwelekeo - ubaba hauji kwa kushindwa kuhudumia dressing table.

Mwanaume haujiamini, kwamba mkeo akijiremba basi analiwa nje - akili za vibamia hii. Hawa mabinti ni 'pambo' bwana, muda wote lazima wawe nadhifu, scent nzuru, ukitembea nae kajipiga mapoda hata wewe kidume kifua kinakua mbele, sio binti unakuta manyusi yametapakaa kila kona ya jicho, unakuta binti ananuka harufu ya feri. Boss sambaza matunzo kwa huyo mlimbwende, sifa za kung'aa kwake zinarudi kwako.
Fact...point...meelewa!
 
Hii dressing table ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya ndoa. Kwanini ?
1. Huyu mwanamke alikudanganya kimuonekano siku ya kwanza ulipomuona. Ulidhani ana ngozi laini ama rangi fulani kumbe ni dressing table. Ukija kuifahamu ngozi na rangi yake kamili kuwa iko viwango vya chini ya vile ulivyojiwekea moyoni, tayari kipande cha upendo humegeka. Mgogoro unaibuka.

2. Hii dressing table ni meza ya kutafuna hela, sawa kabisa ama kuzidi gharama ya kusomesha mtoto English medium schools. Kila iitwapo leo hela inapukutishwa na meza hii ? Siku ukiwa huna fedha za kuijaza meza hii itakuwaje ? Mgogoro unaibuka. Ukisikia wanawake humu wakisema kuna wanaume wana mikono ya birika, wanailenga pia meza hii.

3. Meza hii malengo yake ni maovu. Huyu mtu umekwisha muoa tayari, sasa sabb za kumiliki vichupa vya rangi tofauti kama fine-artist ni zipi ? Mabachelor wanafanya hivi ili wavutie, kisha wanase. Huyu wa kwako naye ?

Basi ukiona hivi, huyu mkeo ana ushetani wa kuendelea kupendwa na wengine. Ànataka kunasa mtu mwingine. Ndiyo.... Ndiyo motive behind ya kuwa na machupa mengi kama bwana mifugo. Maana kama ni mapele ama mabaka usoni wewe mumewe umeyaona.

Hebu ewe mwanaume, jiulize: mkeo matiti yamelala, halafu yy anahangaika kupaka mchina au kutumia sindiria zenye vifuu vya nazi ama kigodoro ili yaonekane yamesimama. Aonwe na nani ili iwe nini ?

Mkeo hana makalio na umempenda jinsi alivyo lkn ànahangaika kupaka mchina au kuvaa skini tight zilizoshonewa hips za vigodoro ili akivaa aonekane ana hips. Aonwe na nani ili iwe nini ? Mkeo hajaridhika na wewe ama amekuchoka au ana hulka ya ukahaba.

Wahenga walisema mwanamke mwenye kujilemba hupenda na kulambwa pia

Amka mwanaume, hakikisha mkeo ana nawa uso kama wewe, una share naye mafuta yako ya mgando na ile losheni yako uliyonunua ukiwa bar. Cha nyongeza kwake iwe kitana kikubwa cha kulazia nywele tu.

ONYO: ushauri huu unafanya kazi kwa walio kwenye ndoa tu.
Umenena mkuu ...ila hawa viumbe ni kuomba Mungu tu akupe anayejitambua.sio kwamba kila linaloibuka basi na yeye yumo Yani yeye sio mtu wa kushabikia mambo yakileo..ambao ndo wanaitwa washamba..ila mi nashangaaga sana unakuta mdada ameondoa nyusi zote...halafu anapaka marangi mekundu..au wengine unakuta ameweka makope yale anafanana kama mdoli..hapo ndo huwa nachoka kabisa nikimtafakari huyu kiumbe mwanamke...akili zao wanazijua wenyewe...
 
wengine wanaongeza mpk mboni za bandia. Watapofuka bure !!
 
wengine wanaongeza mpk mboni za bandia. Watapofuka bure !!
Akili zao wanazijua wenyewe..ila ndo hivyo inabidi kwenda nayo yote ...kuna mwingine hata umwambiaje wala hawezi kukuelewa na huwa najiuliza hivi we mwanaume kweli unasema eti mkeo ni mrembo kwa kuondoa manyusi na kubandika yale ya mdoli..yani kipindi natongoza nilikuwa siangaliagi mara mbili hawa wa dizaini hii...yani sinaga mvuto nao..
 
Yawezekana. Lkn sidhani. Coward ni yule asiyejiamini jinsi alivyoumbika anaamua kuongeza mirangi, minyuzi, minyusi na migodoro
Hapana coward ni yule anaona anakuwa intimidated na uwezo au muonekano wa mwingine.In this case anaogopa mke wake akipendeza ataibiwa au lengo la mwanamke ni ku attract mwanaume.
Kuvaa vizuri au kujiremba ni vitu mtu anafanya kwasababu anajipenda na anajali muonekano wake kwa watu wengine.
Urembo ni ku enhance beauty au uzuri ambao tayari upo na sio kutojiamini.
Sema tu unapenda muonekano natural na sio enhanced,sio kuanza kuita wanawake wanaojiremba wana ushetani.
 
Akili zao wanazijua wenyewe..ila ndo hivyo inabidi kwenda nayo yote ...kuna mwingine hata umwambiaje wala hawezi kukuelewa na huwa najiuliza hivi we mwanaume kweli unasema eti mkeo ni mrembo kwa kuondoa manyusi na kubandika yale ya mdoli..yani kipindi natongoza nilikuwa siangaliagi mara mbili hawa wa dizaini hii...yani sinaga mvuto nao..
MM huwa napata kichefuchefu kabisa
 
Hapana coward ni yule anaona anakuwa intimidated na uwezo au muonekano wa mwingine.In this case anaogopa mke wake akipendeza ataibiwa au lengo la mwanamke ni ku attract mwanaume.
Kuvaa vizuri au kujiremba ni vitu mtu anafanya kwasababu anajipenda na anajali muonekano wake kwa watu wengine.
Urembo ni ku enhance beauty au uzuri ambao tayari upo na sio kutojiamini.
Sema tu unapenda muonekano natural na sio enhanced,sio kuanza kuita wanawake wanaojiremba wana ushetani.
Naomba univumilie sehemu ambazo nimetia chumvi sana mkuu
 
Umeona sasa ? Unarudi pale pale kwenye hoja yangu. Kula umekula na kula umelala. Eti huduma ni kununua hiyo mirangi. Kama una sura mbaya vumilia tu ndiyo mungu aliyokupatia hiyo. Sasa unafikiri utajipapaka mpk lini ?
Kwa wife kupendeza mwisho siku ya harusi sio?mgonjwa wewe eh! Kwa hiyo na wewe sasa no kunyoa ndevu wala nywele yaani zero unadhifu ukioga asubuhi mpaka kesho tena asubuhi full kikwapa hakuna unyunyu dume wala nini bali kunuka kupu kama beberu mzee si ndio hivyo?
 
Naunga hoja mkono, kwangu ninachotumia mm ndicho wife anatumia, ata Pafyum, ukimnunulia ya kike aitaki anapenda za kwangu plus losheni, sinaga gharama mm.

Hehehehehee nimewaza hivii.. .
Kuna wale wanawake wanaopenda kutumia marashi na mafuta ya kiume ya waume zao ili hata akichepuka na mchepuko wake wakakumbatiana hutastuka utajua ananukia yako kumbe ......

Anyways ni mawazo tuu sihihitimisho
 
Back
Top Bottom