Ewe mume usiruhusu mkeo kuwa na "dressing-table"

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,680
2,000
Hii dressing table ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya ndoa. Kwanini?

1. Huyu mwanamke alikudanganya kimuonekano siku ya kwanza ulipomuona. Ulidhani ana ngozi laini ama rangi fulani kumbe ni dressing table. Ukija kuifahamu ngozi na rangi yake kamili kuwa iko viwango vya chini ya vile ulivyojiwekea moyoni, tayari kipande cha upendo humegeka. Mgogoro unaibuka.

2. Hii dressing table ni meza ya kutafuna hela, sawa kabisa ama kuzidi gharama ya kusomesha mtoto English medium schools. Kila iitwapo leo hela inapukutishwa na meza hii? Siku ukiwa huna fedha za kuijaza meza hii itakuwaje? Mgogoro unaibuka. Ukisikia wanawake humu wakisema kuna wanaume wana mikono ya birika, wanailenga pia meza hii.

3. Meza hii malengo yake ni maovu. Huyu mtu umekwisha muoa tayari, sasa sababu za kumiliki vichupa vya rangi tofauti kama fine-artist ni zipi? Mabachelor wanafanya hivi ili wavutie, kisha wanase. Huyu wa kwako naye?

Basi ukiona hivi, huyu mkeo ana ushetani wa kuendelea kupendwa na wengine. Ànataka kunasa mtu mwingine. Ndiyo ndiyo motive behind ya kuwa na machupa mengi kama bwana mifugo. Maana kama ni mapele ama mabaka usoni wewe mumewe umeyaona.

Hebu ewe mwanaume, jiulize: mkeo matiti yamelala, halafu yeye anahangaika kupaka mchina au kutumia sindiria zenye vifuu vya nazi ama kigodoro ili yaonekane yamesimama. Aonwe na nani ili iwe nini?

Mkeo hana makalio na umempenda jinsi alivyo lakini anahangaika kupaka mchina au kuvaa skini tight zilizoshonewa hips za vigodoro ili akivaa aonekane ana hips. Aonwe na nani ili iwe nini? Mkeo hajaridhika na wewe ama amekuchoka au ana hulka ya ukahaba.

Wahenga walisema mwanamke mwenye kujilemba hupenda na kulambwa pia
Amka mwanaume, hakikisha mkeo ana nawa uso kama wewe, una share naye mafuta yako ya mgando na ile losheni yako uliyonunua ukiwa bar. Cha nyongeza kwake iwe kitana kikubwa cha kulazia nywele tu.

ONYO: Ushauri huu unafanya kazi kwa walio kwenye ndoa tu.
 
ONTARIO

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
1,891
2,000
Kuanzisha drama za kishamba, ili kuonekana wewe ndio mkuu, ni upopoma. Ukuu unakuja automatically, ukisikia mwanaume anasema 'unajua mimi ndio baba' jua huyo keshapoteza mwelekeo - ubaba hauji kwa kushindwa kuhudumia dressing table.

Mwanaume haujiamini, kwamba mkeo akijiremba basi analiwa nje - akili za vibamia hii. Hawa mabinti ni 'pambo' bwana, muda wote lazima wawe nadhifu, scent nzuru, ukitembea nae kajipiga mapoda hata wewe kidume kifua kinakua mbele, sio binti unakuta manyusi yametapakaa kila kona ya jicho, unakuta binti ananuka harufu ya feri. Boss sambaza matunzo kwa huyo mlimbwende, sifa za kung'aa kwake zinarudi kwako.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,680
2,000
Inasikitisha sana...

Tafuta pesa kwanza... ukizipata hivyo vitu utaona kawaida sana kumuhudumia mwanamke/mke wako... tena utakuwa unampeleka mwenyewe madukani...

usione vyaoelea...

cc: mahondaw
Umeona sasa ? Unarudi pale pale kwenye hoja yangu. Kula umekula na kula umelala. Eti huduma ni kununua hiyo mirangi. Kama una sura mbaya vumilia tu ndiyo mungu aliyokupatia hiyo. Sasa unafikiri utajipapaka mpk lini ?
 
daudthefarmer

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,466
2,000
Inasikitisha sana...

Tafuta pesa kwanza... ukizipata hivyo vitu utaona kawaida sana kumuhudumia mwanamke/mke wako... tena utakuwa unampeleka mwenyewe madukani...

usione vyaoelea...

cc: mahondaw
stegemei ukinzane na huu uzi, maana ukikinzana nao utakipata cha moto.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,680
2,000
Kuanzisha drama za kishamba, ili kuonekana wewe ndio mkuu, ni upopoma. Ukuu unakuja automatically, ukisikia mwanaume anasema 'unajua mimi ndio baba' jua huyo keshapoteza mwelekeo - ubaba hauji kwa kushindwa kuhudumia dressing table.

Mwanaume haujiamini, kwamba mkeo akijiremba basi analiwa nje - akili za vibamia hii. Hawa mabinti ni 'pambo' bwana, muda wote lazima wawe nadhifu, scent nzuru, ukitembea nae kajipiga mapoda hata wewe kidume kifua kinakua mbele, sio binti unakuta manyusi yametapakaa kila kona ya jicho.
Acha kutetea uongo mkuu, mwanamke ajipake marangi kama ukuta ndiyo unaona sawa ? Haya ma make up yamekuja juzi tu, lkn kujiremba kupo miaka kibao. Vaa nguo nzuri. Usibadili maumbile na muonekano wako
 
Msweet

JF-Expert Member
Mar 26, 2014
1,963
2,000
Kuanzisha drama za kishamba, ili kuonekana wewe ndio mkuu, ni upopoma. Ukuu unakuja automatically, ukisikia mwanaume anasema 'unajua mimi ndio baba' jua huyo keshapoteza mwelekeo - ubaba hauji kwa kushindwa kuhudumia dressing table.

Mwanaume haujiamini, kwamba mkeo akijiremba basi analiwa nje - akili za vibamia hii. Hawa mabinti ni 'pambo' bwana, muda wote lazima wawe nadhifu, scent nzuru, ukitembea nae kajipiga mapoda hata wewe kidume kifua kinakua mbele, sio binti unakuta manyusi yametapakaa kila kona ya jicho, unakuta binti ananuka harufu ya feri. Boss sambaza matunzo kwa huyo mlimbwende, sifa za kung'aa kwake zinarudi kwako.
Pata Likes 100. Umenena vema
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,680
2,000
Naunga hoja mkono, kwangu ninachotumia mm ndicho wife anatumia, ata Pafyum, ukimnunulia ya kike aitaki anapenda za kwangu plus losheni, sinaga gharama mm.
Safiii. Siyo unajaza makolomakolo ndani hadi chumba kinabadilika harufu utadhani wodini
 
Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
67,215
2,000
Inasikitisha sana...

Tafuta pesa kwanza... ukizipata hivyo vitu utaona kawaida sana kumuhudumia mwanamke/mke wako... tena utakuwa unampeleka mwenyewe madukani...

usione vyaoelea...

cc: mahondaw
Kumbe umegundua tatizo ni pesa eeeh!!!
Kweli magu kakaza.
 
Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
67,215
2,000
Kuanzisha drama za kishamba, ili kuonekana wewe ndio mkuu, ni upopoma. Ukuu unakuja automatically, ukisikia mwanaume anasema 'unajua mimi ndio baba' jua huyo keshapoteza mwelekeo - ubaba hauji kwa kushindwa kuhudumia dressing table.

Mwanaume haujiamini, kwamba mkeo akijiremba basi analiwa nje - akili za vibamia hii. Hawa mabinti ni 'pambo' bwana, muda wote lazima wawe nadhifu, scent nzuru, ukitembea nae kajipiga mapoda hata wewe kidume kifua kinakua mbele, sio binti unakuta manyusi yametapakaa kila kona ya jicho, unakuta binti ananuka harufu ya feri. Boss sambaza matunzo kwa huyo mlimbwende, sifa za kung'aa kwake zinarudi kwako.
Baambie baelewe
Heshima haishikiwi mtutu, heshima is earned.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom