Euro 2020: Kweli lilikuwa kundi la kifo

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Yalipopangwa makundi ya michuano ya Euro 2020, kuna kundi liliitwa la kifo. Lilijumisha mabingwa wa dunia Ufaransa; mabingwa wa Ulaya watetezi Ureno; mabingwa wa kihistoria wa ulaya na dunia Ujerumani na Hungary.

Baada ya michezo ya makundi, Hungary akauwawa. Wakapona Ufaransa, Ujerumani na Ureno. Ikafuata michezo za 16 bora. Ufaransa akakipiga na Uswisi-kule kwenye akaunti za vibosile wetu. Ufaransa akafa kwa penati 5 kwa 4 baada ya sare ya kibabe ya 3 kwa 3.

Ureno akaingia kumi na nane za Ubelgiji alikotibiwa Lissu na kuzabwa bao 1 kwa bila. Akabaki Ujerumani. Jana naye akakutana na Uingereza-wazee wa maneno mengi. Ujerumani akapotea kwa kamba 2 kwa bila. Kundi likawa limeishia hapo.

Kweli lilikuwa la kifo. Wote wamekufa. Kundi limeua watoto wake wote. Hayati Ken Sarowiwa wa Nigeria aliwahi kuandika simulizi iitwayo 'Africa kills her own son'. Kundi limesambaratishwa na watanabe wa Ulaya.
 
Yalipopangwa makundi ya michuano ya Euro 2020, kuna kundi liliitwa la kifo. Lilijumisha mabingwa wa dunia Ufaransa; mabingwa wa Ulaya watetezi Ureno; mabingwa wa kihistoria wa ulaya na dunia Ujerumani na Hungary.

Baada ya michezo ya makundi, Hungary akauwawa. Wakapona Ufaransa, Ujerumani na Ureno. Ikafuata michezo za 16 bora. Ufaransa akakipiga na Uswisi-kule kwenye akaunti za vibosile wetu. Ufaransa akafa kwa penati 5 kwa 4 baada ya sare ya kibabe ya 3 kwa 3.

Ureno akaingia kumi na nane za Ubelgiji alikotibiwa Lissu na kuzabwa bao 1 kwa bila. Akabaki Ujerumani. Jana naye akakutana na Uingereza-wazee wa maneno mengi. Ujerumani akapotea kwa kamba 2 kwa bila. Kundi likawa limeishia hapo.

Kweli lilikuwa la kifo. Wote wamekufa. Kundi limeua watoto wake wote. Hayati Ken Sarowiwa wa Nigeria aliwahi kuandika simulizi iitwayo 'Africa kills her own sun'. Kundi limesambaratishwa na watanabe wa Ulaya.
Ni kweli nakubaliana na wewe,kundi F limekufa kweli.Kwenye kitabu cha Ken Sarowiwa badilisha isomeke Son bbadala ya Sun.Mkuu
 
Back
Top Bottom