EU, USA should ban CCM leaders and their families ....

Umeleta point moja nzuri sana. Hiyo ya ku-raise issue siku zote namlaumu Mrema kwa kukubali kujiingiza kwenye uchaguzi wa 1995 bila kusoma katiba. Simba na Yanga hawachezi mechi kama mmoja wao anapewa competitive advantage.

Anyway, wataalamu wanasema watu wenye oral traditions, mara nyingi wanatumia kauli za midomoni kuendesha shughuli zao. Mgombeaji wa uchaguzi akiona kwenye kampeni kakusanya watu wengi sana, basi anaamini kuwa atashinda.

Uchaguzi ukimalizika ndio anatambua kuwa wanaohesabu na kusimamia ni watu walioteuliwa na mpinzani wake. Lakini haya mambo yote yapo kwenye katiba.

Katiba ndilo jibu la ukombozi wa Tanzania. Zakumi you are quite coreeeeeeeeeeeeeeect, bila katiba ya uwazi, kupata haki zetu ni ngumu. Nibora tuwashinikize International community including USA, EU,UN and others watusaidie kupiga kelele ili tuwe na katiba mpya. Mbona Sudani wanapata refrendum tena Bwn Mkapa ni msimamizi?
 
Mabadiliko yatatokea ndani ya nchi....tusipoangalia tutatengeneza vibaraka wa wamarekani. Kama miaka ya kina Patrice Lumumba. America always will serve their interests period.

Kina post m,oja huko nyuma nilisema kuwa endapo adhabu inatimiza lengo lile lile, mimi sitajali kuwa inatolewa na nani. Maneno kama kibaraka (stooge/puppet), Ukoloni mamboleo (neo-colonialism), na mengineyo ya namna hiyo nilikutana nayo wakati nikiwa mdogo miaka ya sitini na sabini ikiwa ni sehemu ya elimu ya Siasa. Kibaraka halisi ni yule asiyejali maslahi ya watu wake bali ya kwake na ya mabwana zake, kama ambavyo watawala wa CCM walivyokuwa wanauza raslimali zetu kwa mabwana zao kwa bei nafuu ilihali wao wanapa kamisheni zao bila kujali atahari zake kwa watu wetu. mMtu yeyote anayepambana na watu wa CCM kwa ajili ya faida ya watu wote si Kibaraka. Anaweza kugeuka kuwa kibaraka huko mbeleni akishawaondoa vibaraka wa sasa lakini hilo ni jambo la mbeleni tusilojua; kazi ya kwanza ni kusafisha uchafu ulioko mbele yetu sasa hivi.
 
Sawasawa kabisa.

Suala la kuwabana mafisadi linawezekana sana tu. Mbona wazungu walirudisha fedha alizokwapua fisadi na muuaji Abacha? It is a matter of pressing right buttons tu na kuweka pressure kwa raia wa hizo nchi za dunia ya kwanza, maana wao at least hawacheki na nyani.

Taxpayers wao hawawezi kushawishika kienyejienyeji tu, ati wao wakatwe kodi ambayo inakuja huku Afrika kama misaada halafu wapuuzi wachache huku wazitumie tena kufanyia shopping vimada na familia zao Dubai, NY au Paris..Its a matter of commonsense tu.
 
Wadau natafuta team ya kuweza kuwakilisha documents kadhaa kwa nchi hasa za UK na USA ili hawa wanoko wakione cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya ... .....
 
Mkuu Wacha1, mimi naamini kabisa hao wahisani hawawezi kufanya lolote kama wananufaika na uongozi wa CCM ulioko madarakani hivi sasa, hawa ni wanafiki wakubwa. Kumbuka Kigamboni tayari watu wameshaanza kuambiwa wahame ili kupisha ujenzi wa Military base ya Wamarekani, na hii G.W. Bush alilimaliza alivyo kuja huku kumzuga Mkwere na Vyandarua ambavyo watu wanatumia kuvua samaki.

Nafikiri tusimame wenyewe kwanza kupigania haki zetu badala ya kuanza kutegemea wahisani kuja kutusaidia
 
Tatizo kwa TZ ni kwamba, viongozi wangi wa CCM na serikali wanawapa madini na maeneo muhimu bure hao USA na EU kwa hiyo hawawezi kuwazuia hata kidogo, lakini wangekuwa wamebana madini kama nyerere huku wanafanya uchakachuaji wa kura tangu 1995 zenji na 2010 Bara wangeshawazuia kuingia huko.

Kwa hiyo hata inchi kubwa hizo zina maslahi makubwa kwa CCM na TZ kwa ujumla.

Issue ni sisi wanaTZ tuwakomalie hadi tuwatoe. Kumbuka Uwezo tunao, Nia Tunayo na sababu tunayo ya kuwatoa madarakani.

peoples Power
 
WJC:

Umeleta point moja nzuri sana. Hiyo ya ku-raise issue siku zote namlaumu Mrema kwa kukubali kujiingiza kwenye uchaguzi wa 1995 bila kusoma katiba. Simba na Yanga hawachezi mechi kama mmoja wao anapewa competitive advantage.

Anyway, wataalamu wanasema watu wenye oral traditions, mara nyingi wanatumia kauli za midomoni kuendesha shughuli zao. Mgombeaji wa uchaguzi akiona kwenye kampeni kakusanya watu wengi sana, basi anaamini kuwa atashinda.

Uchaguzi ukimalizika ndio anatambua kuwa wanaohesabu na kusimamia ni watu walioteuliwa na mpinzani wake. Lakini haya mambo yote yapo kwenye katiba.

Wewe acha mambo ya 19kweusi tunahaitaji katiba mpya sasa. Mambo ya Mrema ya zamani. Wewe una maslahi gani na katiba ya sasa??????????? Bila shaka wewe na SISIEMU ni wamoja!!!!!!!!! Katiba ipi, hiyo imepitwa na wakati>>
 
[/COLOR][/I]

Sir, do I have the right to be stupid? Yes I do.
 
Tutoe shinikizo kwa EU na USA kuwapiga mkwala wa kwenda ulaya na marekani viongozi wote wa CCM pamoja na familia zao kwa wizi wa kura. Haiwezekani watuibie kura halafu waende kujichana kwa pesa zetu.

CHADEMA huu ni wakati wa kuanza kampeni kwa mabalozi na nchi zote marafiki ili hawa wanoko wakione cha mtema kuni.

Hii imekaa vizuri sana...
Nilikuwa naangalia Euronews, inaonyesha jinsi FFU wa JK walivyotumia maguvu kuvuruga Maandamano ya kidemokrasia kudai Katiba. Kitendo cha Euronews kuidaka hii ni pigo na anguko lingine kwa 'utawala huu wa giza' ambao ni mkusanyiko wa 'wachakachuaji' walioiba kura halali za watanzania na kujitangazia ushindi wa kifisadi, na kuendelea kutumia nguvu ya dola kukandamiza haki na uhuru wa kila mtanzania!

Nguvu ya Umma itazidi kuwaweka ktk ukingo wezi wote hawa na kama ulivyoshauri, inabidi wawe black-listed ili dunia izidi kuwatambua na ikiwezekana wawe banned kusafiri nje ya Tz ikiwa ni pamoja na majina yao kuwekwa ktk ICC prospective criminals list!
 
Back
Top Bottom