Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,491
- 19,323
Wanaolalamikia move ya aina hii sijui wanafikiria nini. Kwa nyumbani hapa CCM ndio wameshika mpini wakiwa na mapesa mengi ya kuchezea ili mradi kuvuruga haki za raia wengine kwa manufaa yao binafsi. Tunapotaka kuwaondoa kwa kura za halali wanatukatalia kwa mabavu. Kwa hiyo kwangu mimi nakubaliana na adhabu yoyote itakayowezekana kwa hao CCM hata kama adhabu hiyo inatolewa na watu wa nchi nyingine hata nisiowapenda. Adhabu ni adhabu tu kama itafanikiwa kutimiza malengo yangu.