EU statement on the closure of The East African

EU statement on the closure of The East African

Kwa kuchapisha katuni ya DHAIFU

B8DwzysCcAAct_2.jpg:large

This comes from a nation where someone is serving a long jail term for, allegedly, insulting the president!
 
Eric Cartman unena vizuri sana...lakin mbona wao wanadai ni kutosajiliwa na sio kwa sababuza "national interest" kwanini wanaficha??
 
Last edited by a moderator:
The Delegation of the European Union calls upon the Government to make every effort to preserve the freedom of expression in Tanzania

We hope they will also meet and make a joint statement that all contracts entered by the multinational companies from their countries with the Tanzania Government, that such contracts should be transparent and be published in every newspaper in their own countries and in Tanzania as a part of a right of giving information to the public.We hope such a joint statement will be made as soon as possible.
 
Waende zao wakakemee mataifa yao pia na uzuizi wa habari indirectly kupitia sheria zao sio kuja kutaka kutuletea culture imperialism na demokrasia ambazo hatujafikia kama jamii.

Gazeti aliwezi kuwa lina andika nakala za kichochezi na kui-represent serikari with negative stories kila mara lika achiwa, kama washazoea kuandika nakala za kibaguzi ni makwao huko huko Rwanda sio Tanzania kwanza ni move ambayo imechelewa sana.

Hao EU kwanza watueleze kanuni na sheria za nchi mwanachama wao ambae anamasharti luluki yenye kukandimiza kwa malengo ya ku-shape reporting zenye mlengo wa utaifa kabla ya kuja kwetu sisi.

Huko uingereza kuna chombo chao cha 'Press Complaint Commission' ambapo magazeti yote ni wanachama na wanatakiwa kufuata kanuni kadhaa za uandishi na ku-report habari nenda kinyume kama hawajakuwakia. Moja ya masharti ya uandishi ni acting in the public interest (this has wide interpretations to mean national interest) andika nakala ambazo zinatetea taifa lingine au policy ambazo za national interest uone kama gazeti alitawekewa mizengwe.

Zidi ya hapo ikiwa kama part of censorship kwa vyombo vya habari kuna sheria luluki za ku-shape reporting; sheria mbili muhimu zikiwa 'The official secret act' ambapo maswala sensitive ya kitaifa haya andikwi hovyo na gazeti likijaribu utaona bunge litakavyowaka moto kutaka kujua source of information na hiyo sheria imewekwa mahususi kuzuia habari sensitive kuandikwa. Sheria ya pili 'Race relation act' ambapo ni marufuku kuandika nakala zenye uchochezi au zenye malengo ya kugawa jamii, jamaa wamezidi kuiandika Tanzania kama nchi isiyotaka amani kati ya wahutu na watutsi na mambo mengi ya kipuuzi na uchochezi.

Huo uhuru wanaotaka kutulazimishia kwanza wangefanya kwa wanachama wao na sheria luluki zinazochora mipaka ya uandishi, hawa jamaa walizidi na imechukua muda mrefu sana wafungiwe tu indefinitely kwa maandishi yao ambayo sio sahihi kwa taifa we have the right to defend our shores and our peaceful ways sio watu kulishwa values ambazo sio sahihi na mamluki wa Kagame na Kenyatta.
Wewe ndiye Zuzu no one...Uhuru wa vyombo vya habari ni mihimu. Esrow imewaumiza watawala,washirka wao na familia zao,na ndio maana ya kufungia Gazeti hili.
 
Hawa jamaa ni wa hovyo

Haya ni mambo ya ndani ya nchi
 
Kama wanaona gazeti ni mhimu basi walichukue kwenye nchi za EU wasituletee ujinga wa kutupangia kila kitu
 
Ujinga hauondoki kwa sababu unajua kuandika, kusoma na kuongea kiingereza. Ina maana wewe hujui hata mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhia?

Tanzania ni nchi huru, na ina sheria na taratibu zake zilizowekwa katika upashanaji wa habari, hakuna uhuru pasipo kutii sheria za nchi.

Kama wanataka, wakalichapishe hilo gazeti EU countries.
 
Ujinga hauondoki kwa sababu unajua kuandika, kusoma na kuongea kiingereza. Ina maana wewe hujui hata mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhia?

Haya tupe mkataba mmoja wa kimataifa ambao unasema gazeti lina haki ya kuchapishwa na kusambazwa kwenye nchi bila kusajiliwa!!!! Hebu tupe mfano wa huo mkataba mmoja.
 
Tukijitambua kama Taifa ndipo kauli kama hizi tutaweza kuzikabili kwa ujasiri!
Ni kweli EU wanaingilia mambo yetu ya ndani lakini ni sisi wenyewe (kupitia viongozi tulionao) tuliowapa fursa hiyo.
 
hatuna jema.... sheria isiposimamiwa tunalaumu......sheria ikisimamiwa tunalaumu.......
PONGEZI SERIKALI KWA KUSIMAMIA SHERIA
1. Ila na nyie msiwe mnachelewa sana, oneni lawama zote zinakuja kwenu kwa kutosimamia.....
2. Justice delayed is justice denied...... (SERIKALI MMEONA)
3. Kifanyike kitu kwa walisababisha kadhia hii, kuruhusu kwa miaka 20 kitu ku operate bila kibali.....(huenda waliruhusu wameshastaafu)
 
waliachiwa miaka yote sababu walikuwa wanaiandika vizuri ccm,sasa hivi imekuwa opposite plus na kile kibonzo cha jk wamepigwa ban!!!!
 
Tanzania ni nchi huru, na ina sheria na taratibu zake zilizowekwa katika upashanaji wa habari, hakuna uhuru pasipo kutii sheria za nchi..

Right. Baada ya miaka 20 ndio tumegundua kwamba tuna ''sheria zilizowekwa katika upashanaji wa habari''.
 
Hawa EU ni wanafiki sana, katika uchaguzi wa 2010 waliondoka kimya kimya bila kutoa tasmini ya uchaguzi kutokana na wizi wa kura. Leo wanatoa statement ya ajabu kuhusu serikali inayoongozwa na CCM wakati wao ndio walikuwa wa kwanza kuipa support 2010..

Sio kweli, EU walitoa tathmini na report ndefu tu. Nilikuwepo wakati wa kutolewa report. Moja kati ya mambo waliyosisitiza ni uhuru wa habari.
 
kwani hizo sheria ziliwekwa juzi? si zilikuwepo wapi tokea miaka 20 ambayo gazeti lilikua linauzwa tanzania? kwanini wasilizuie toka kipindi hicho waje walizuie juzi?? mimi ni mtanzania lakini sikubaliani na huu uozo!!

Sheria itatumikaje kama hujaivunja, wameivunja ndiyo ikatumika. Hili gazeti kwa kiasi fulani siku za hivi karibuni ni kama lilianza kutumiwa vibaya kana kwamba ndani ya Africa Mashariki Tanzania pekee ndiyo ina habari mbaya nchi nyingine zina habari nzuri. Mara Tanzania inawatetea Waasi wa Kihutu, mara Tanzania inakwamisha umoja wa Afrika Mashariki, Tanzania imejiweka mbali na mapambano dhidi ya Al Shabaab. Hakuna uhuru husiyo na mipaka.
 
Wewe ndiye Zuzu no one...Uhuru wa vyombo vya habari ni mihimu. Esrow imewaumiza watawala,washirka wao na familia zao,na ndio maana ya kufungia Gazeti hili.

Bila shaka wewe ndiyo zuzu, kama ni masuala ya escrow media nyingi zingefungiwa hata hii JF. Hawa jamaa walikuwa wanaandika habari za uchonganishi dhidi ya Tanzania na nchi jirani, hakuna uhuru pasipo mipaka.
 
Tanzania ni nchi huru, na ina sheria na taratibu zake zilizowekwa katika upashanaji wa habari, hakuna uhuru pasipo kutii sheria za nchi.

Kama wanataka, wakalichapishe hilo gazeti EU countries.

Tusichukie matamshia yao tu...na hela zao pia tuache kujikomba komba kuziomba. Ndio tutaweza kuwa na uhuru kamili. Vinginevyo we will continue to dance to their tune
 
Haya tupe mkataba mmoja wa kimataifa ambao unasema gazeti lina haki ya kuchapishwa na kusambazwa kwenye nchi bila kusajiliwa!!!! Hebu tupe mfano wa huo mkataba mmoja.

Ina maana miaka 20 yote walikua hawajui gazeti halijasajiliwa??
 
Sheria itatumikaje kama hujaivunja, wameivunja ndiyo ikatumika. Hili gazeti kwa kiasi fulani siku za hivi karibuni ni kama lilianza kutumiwa vibaya kana kwamba ndani ya Africa Mashariki Tanzania pekee ndiyo ina habari mbaya nchi nyingine zina habari nzuri. Mara Tanzania inawatetea Waasi wa Kihutu, mara Tanzania inakwamisha umoja wa Afrika Mashariki, Tanzania imejiweka mbali na mapambano dhidi ya Al Shabaab. Hakuna uhuru husiyo na mipaka.

Uko sahihi..na mimi siungani nao katika swala la uchochez!! HOJANI KWAMBA WAO WANASEMA WAMELIFUNGIA KWASABABU HALIJASAJILIWA, JE KWA MIAKA YOOOOTE 20 NDIO WANAGUNDUA LEO KWAMBA GAZETI HALIJASAJILIWA??
 
Back
Top Bottom