Eti wengi wanatamani kutoka kuliko kuingia???

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Wanandugu ni vyema kuwashirikisha hili
nikiwa nakula kulizuka mjadala mkubwa pale rosegarden
ati wengi waliko ndan ya ndoa wanatamani kuruka na kurudi walipotoka
nilikuwa speechless naamini maoni yenu yatakuwa wakati muafaka kwa lengo
la kujenga jamii
 
mimi huko napasikia tu ndo maana sitaki kuingia kwa sasa, ngoja wenyewe waje
 
mimi sijaingia hata huko pia!! ila ninavyofahamu kwa kuangalia maisha ya wanandoa wengi wanaonizunguka, ndoa nyingi zina matatizo makubwa tu.. wengine wanaendelea kuishi pamoja kwa kuvumiliana ila sivyo wangekuwa wameshamwagana!!...

Ndoa za siku hizi zimebaki majina tu watu wanaoana lakini vimada/nyumba ndogo na mabuzi ni kama kawa, hawaheshimiani, hawasikilizani yaani ni tabu tupu.... imekuwa fashion mtu anaoa mtu kwa kuwa ni mrembo au mtu anaolewa na mtu kwa kuwa ana pesa ila ki ukweli si kwamba anampenda! matokeo yake akiwa ndani ya ndoa hana hisia na mumewe/mkewe na kuanza kutafuta kwingineko....
 
95% ya vijana ( wake kwa waume) walio single huwa wanatamani kuingia huko na 96% ya wanando wanatamani kutoka huko.
 
Ukweli sasa hivi pesa tu! wanawake walio wengi wanaingia/penda mtu kwa pesa yake,wanaume wengi tamaa, lkn hakuna inner feeling about da person. baada muda mfupi tifu zinaanza,maana huwezi ficha feelings
 
Mi napasikia ni jehanamu hivyo sitaki kuingia, ntaangalia wapi ntapata mbegu nzuri natafuta katoto kangu kakulinda jina langu lisife kwenye ukoo basi.
 
Mawazo ya wengi ambao hawajaingia kwenye ndoa
Ndoa ni taasisi na ni taasisi inayojitosheleza
Ndoa haipwaswi kulinganishwa au kufananishwa na huwezi kufananisha ndoa ya Mr Rocky na ya Pdiddy hata siku moja.
maisha anayoishi Rocky na Pdiddy ni tofauti na mitizamo na migongano ya ndoa hizo mbili ni vitu viwili tofauti

Tukisema ndoa ni mbaya au walio kwenye ndoa wanatamani kutoka wakati wengine wanaingia kila siku tunamaanisha nini.
Kwanza jiulize ulioa ili iweje
Kwa nini umemuoa huyo mwanamke uliye nae ndani ya ndoa yako? Ni nini kilikusukuma kuoa ni shinikizo au ni umri au wazazi walikulazimisha au ilitokea bahati mbaya msichana uliyekuwa nae akapata mimba na wewe bila kutarajia ikabidi uoe
Na je umemuoa mwanamke uliye nae kwa kuwa unampenda au kwa kuwa imebidi umuoe baada ya labda kusemwa na washkaji kuwa kwa nini huoi au umri umeenda sana au ulikutana nae kibahati bila hata kumjua na ukafunga nae ndoa

Pili je mwanamke wako kule ndani ya nyumba ni nani? Ni kama kifaa cha kukufanyia kazi na kikizeeka unatupa unanunua kingine? Au ni mtambo wa kuzalisha tuu watoto ili na wewe uonekane mtaani kuwa ni kidume kwa kuwa na watoto then unamchoka na kuanza kumsema kuwa matiti yamelala na siku hizi sio msafi tena ana harufu ya maziwa usiyoipenda na harufu ya chakula usiyoitaka. Na sio mzuri tena anaelekea kuzeeka kuliko yule kimada wako wa mtaa wa pili ambaye bado hana watoto na hana harufu ya maziwa wala vitunguu?

Tatu je mwanamke wako ndani ya nyuma mnamalizaje mambo yenu wakati wa ugomvi au shida au raha? Huwa magomvi yenu mnayasuluhishaje? Mnapandishiana kama moto wa kifuu wakati mmegombana au mkiwa na tofauti? Ndani ya nyumba mambo yakiwa hot mnafanyaje? mwanaume unakimbilia bar kunywa pombe au kukaa na washkaji kumkimbia mkeo?

Nne je mwanamke wako unampa muda wa kutosha kukaa nae na kuongea mambo ya maendeleo yenu au kila siku wewe ni vikao na washkaji bar na kwenye luninga za mabaa kuangalia mechi kati ya Asernal na Manchester United?

Tano unaaapreciate anachofanya mkeo ndani ya n yumba au kila siku wewe ni kumkosoa na kumshushia hadhi kuwa hajui kitu? Na je unamfundisha hata pale ambapo hajui na kumwelekeza kama mkeo ?

Hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo tusipoviangalia vinaifanya tasisi ya ndoa kuonekana kituko. Ndoa ni maamuzi ya watu wawili kuishi pamoja na kufuata misingi ya maisha bora kukaa pamoja kwenye raha na shida. Iheshimu ndoa yako na muheshimu mwenzako haya maswala ya kusema kuwa walio kwenye ndoa wanalilia kutoka hayatakuwepo. Ukishaijua ndoa yako na ukishamjua mwenzako unawez akujipanga namna ya kuishi nae na kufanya kile ambacho hakitamuudhi mwenzako na kutojiingiza kwenye masuala ambayo yatakufanya ujute kumuoa yule uliye nae. Usregret kumuoa wala usilazimishe kumuona kuwa yeye ni chanzo ila fanya kila lillilo ndani ya uwezo wako kuitunza ndoa yako
 
Maisha ya ndoa ni mazuri; tatizo walio ndani wanafanya yaonekane mabaya. Ndio maana yanafananishwa na BAHARI kuwa walio nje wanayaangalia maji baharini na kutamani kuingia kuogelea, na walio ndani baharini wanachoshwa na harufu na mawimbi ya bahari kwa kukosa uvumilivu wanatamani kutoka :flypig:.

BAHARI HAIKOSI MAWIMBI!!!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Wanandugu ni vyema kuwashirikisha hili
nikiwa nakula kulizuka mjadala mkubwa pale rosegarden
ati wengi waliko ndan ya ndoa wanatamani kuruka na kurudi walipotoka
nilikuwa speechless naamini maoni yenu yatakuwa wakati muafaka kwa lengo
la kujenga jamii

Kama vile nilikuona Pdidy, si ulikuwa unaangalia mpira??!! ha ha

Bwana eeh..ndoa inategemea na utakaekutana nae..usisikilize stori za castle lite na halafu kwa muda kama ule mume wa mtu yupo bar unategemea ataiona ndoa nzuri??!!

Tunasahau kuwa maisha kwa ujumla yana changamoto hata uishi na na ndugu zako..hivyo kwenye ndoa hazikosekani, kadiri ya kukabiliana nazo ndiyo tatizo kubwa..
 
Maisha ya ndoa ni mazuri; tatizo walio ndani wanafanya yaonekane mabaya. Ndio maana yanafananishwa na BAHARI kuwa walio nje wanayaangalia maji baharini na kutamani kuingia kuogelea, na walio ndani baharini wanachoshwa na harufu na mawimbi ya bahari kwa kukosa uvumilivu wanatamani kutoka :flypig:.

BAHARI HAIKOSI MAWIMBI!!!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!

Mkuu mojawapo ya mambo ambayo yanawafanya walio ndani kutamani kutoka nje ni tamaa
Mtu umeoa ila macho yako yako juu juu kuangalia vimwana walio nje untamani uwaoe wote wakati uwezo wako haupo
Bado unatamani kurudia ujana na kwenda dicso mpaka usiku wa manane
Bado unatamani kukaa kijiweni mpaka usiku wa manane na washkaji unapiga story zile zile ulizokuwa unaongea nao wakati hujaoa
Hujajua majukumu yako wala hujajua kama una mwenzi wako nyumbani
Bado unatamani kutokuwa na mtu wa kukuuliza aise utachelewa nyumbani niwaruhusu watoto wale
Hayo yanawafanya walio ndani ya ndoa kutamani kutoka nje wanapoona kwamba wanapitwa na haya mambo ya dunia
 
mawazo ya wengi ambao hawajaingia kwenye ndoa
ndoa ni taasisi na ni taasisi inayojitosheleza
ndoa haipwaswi kulinganishwa au kufananishwa na huwezi kufananisha ndoa ya mr rocky na ya pdiddy hata siku moja.
Maisha anayoishi rocky na pdiddy ni tofauti na mitizamo na migongano ya ndoa hizo mbili ni vitu viwili tofauti

tukisema ndoa ni mbaya au walio kwenye ndoa wanatamani kutoka wakati wengine wanaingia kila siku tunamaanisha nini.
Kwanza jiulize ulioa ili iweje
kwa nini umemuoa huyo mwanamke uliye nae ndani ya ndoa yako? Ni nini kilikusukuma kuoa ni shinikizo au ni umri au wazazi walikulazimisha au ilitokea bahati mbaya msichana uliyekuwa nae akapata mimba na wewe bila kutarajia ikabidi uoe
na je umemuoa mwanamke uliye nae kwa kuwa unampenda au kwa kuwa imebidi umuoe baada ya labda kusemwa na washkaji kuwa kwa nini huoi au umri umeenda sana au ulikutana nae kibahati bila hata kumjua na ukafunga nae ndoa

pili je mwanamke wako kule ndani ya nyumba ni nani? Ni kama kifaa cha kukufanyia kazi na kikizeeka unatupa unanunua kingine? Au ni mtambo wa kuzalisha tuu watoto ili na wewe uonekane mtaani kuwa ni kidume kwa kuwa na watoto then unamchoka na kuanza kumsema kuwa matiti yamelala na siku hizi sio msafi tena ana harufu ya maziwa usiyoipenda na harufu ya chakula usiyoitaka. Na sio mzuri tena anaelekea kuzeeka kuliko yule kimada wako wa mtaa wa pili ambaye bado hana watoto na hana harufu ya maziwa wala vitunguu?

Tatu je mwanamke wako ndani ya nyuma mnamalizaje mambo yenu wakati wa ugomvi au shida au raha? Huwa magomvi yenu mnayasuluhishaje? Mnapandishiana kama moto wa kifuu wakati mmegombana au mkiwa na tofauti? Ndani ya nyumba mambo yakiwa hot mnafanyaje? Mwanaume unakimbilia bar kunywa pombe au kukaa na washkaji kumkimbia mkeo?

Nne je mwanamke wako unampa muda wa kutosha kukaa nae na kuongea mambo ya maendeleo yenu au kila siku wewe ni vikao na washkaji bar na kwenye luninga za mabaa kuangalia mechi kati ya asernal na manchester united?

Tano unaaapreciate anachofanya mkeo ndani ya n yumba au kila siku wewe ni kumkosoa na kumshushia hadhi kuwa hajui kitu? Na je unamfundisha hata pale ambapo hajui na kumwelekeza kama mkeo ?

Hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo tusipoviangalia vinaifanya tasisi ya ndoa kuonekana kituko. Ndoa ni maamuzi ya watu wawili kuishi pamoja na kufuata misingi ya maisha bora kukaa pamoja kwenye raha na shida. Iheshimu ndoa yako na muheshimu mwenzako haya maswala ya kusema kuwa walio kwenye ndoa wanalilia kutoka hayatakuwepo. Ukishaijua ndoa yako na ukishamjua mwenzako unawez akujipanga namna ya kuishi nae na kufanya kile ambacho hakitamuudhi mwenzako na kutojiingiza kwenye masuala ambayo yatakufanya ujute kumuoa yule uliye nae. Usregret kumuoa wala usilazimishe kumuona kuwa yeye ni chanzo ila fanya kila lillilo ndani ya uwezo wako kuitunza ndoa yako

mwenye macho na asome maneno ambayo mr rocky awaambia wana jf
ukiachika walahi ata kwanghu uwezi kukaa soma hapo juu ujifunze machache lakini ni zaidi ya serengeti
 
mwenye macho na asome maneno ambayo mr rocky awaambia wana jf
ukiachika walahi ata kwanghu uwezi kukaa soma hapo juu ujifunze machache lakini ni zaidi ya serengeti

Asante sana mkuu
tatizo watu wanaingia kwenye ndoa wakati hata ule utayari wa kuingia kwenye ndoa haupo
wanaingia kwa sababu wamelazimishwa au wakati umewatupa mkono au mimba zisizotarajiwa au shinikizo
Watu kama hao hawawezi kamwe kuikubali ndoa na kuiona ni ya maana na watakuwa kila siku wanawadiscourage wenzao wasiingie maana kwao ndoa ni utumwa
 
Heeeheeee mpwa hi ya bar sikuiona samahan bana nilikuwa na mama didy kabisa aka mama "kijacho""usiulize zaidi
mmhh kwa kweli bar sipapendi ila linapokuja swala la mpira hata mamuy didy analiheshimu pamoja na dstv nyumbani siwezi bila kelele mpwa wangu nimesoma hayo manenno yako mama didy anasema kwa nini amechelewa kuingia jf ...angenifunda kikweliii nkasema usizidishe kama unashda aende kwa wakubwa tukafundane mpwa
thanks for advs....ni kweli nimeona wengi wao waliokuwa pale wana midhahabu yao kwenye kidole bila wenzao..ila siwezi ingilia maana huujui makubaliano labda bibie nae anapenda disco kaachwa disco mzee akitoka anampitia usiniulize disco yuko na nani??hiyo ndio ndoa see u altare
 
Mpwa ungejaribu kuwauliza hao wanaosema kuwa ndoa zao ni chungu uchungu wake ni nni
Kwa nini wanatamani watoke
Kwa nini wanatamani maisha ta kuwa single
Kwa nini hawako na wenzi wao kwenye maeneo kama yale
Kwa nini wako pale muda huo wakati nyumbani kwao kuna DStv wanaweza kuangalia mpira mle
Ni kwa sababu wanajua nini tatizo la ndoa zao na kwa nini ndoa zao ni chungu
 
Ndoa ni taasisi,na taasisi inaundwa na watu ambao wana mawazo na mitizamo tofauti ambayo huweza zaa migogoro ambayo huwa inajenga au kubomoa.
Katika migogoro inategemea huwa inaishaje katika ndoa/taasisi husika.Ama taasisi ivunjike,itengane kwa muda,wasimamishane kazi au kuifanya taasisi izidi kuwa imara.
Kila mmoja ana uzoefu wake wa ndoa ambao unatofautiana na mwingine.
 
Ndoa ni taasisi,na taasisi inaundwa na watu ambao wana mawazo na mitizamo tofauti ambayo huweza zaa migogoro ambayo huwa inajenga au kubomoa.
Katika migogoro inategemea huwa inaishaje katika ndoa/taasisi husika.Ama taasisi ivunjike,itengane kwa muda,wasimamishane kazi au kuifanya taasisi izidi kuwa imara.
Kila mmoja ana uzoefu wake wa ndoa ambao unatofautiana na mwingine.

Na ndo maana tunasema ndoa zote hazifanani
Huwezi ukakaa kijiweni ukaanza kuutangazia umma kuwa aise ndoa ni ngumu
Au kusema kuwa walio ndani wanatamani kutoka
Isemee ndoa yako na wala usimsemee fulani
Ndoa yako na ya mwingine kamwe haziwezi kuwa sawa na kila moja ina mambo yake na ina migogoro yake na ina namna ya kuishughulikia
 
KABISA ROCKY
MIMI NILICHOJIFUNZA KWA WAZAZI NA KWA BABU ZETU NA BIBI ZETU NI MOJA
TUNAITAJI KUOMBEA WATOTO ZETU TANGU WAKIWA WACHANGA..WEWE UMEJIFUNGUA MTOTO WA KIKE UNAULIZWA KAZINI AMA BAR UMEPATA BARMED AMA JAMBAZI UNAJIBU BARMED AKIUKOSA UBAMED UTAMKUTA LASVEGAS UTAPIGA KELELE????KUWENI MAKINI NA MIDOMO MANENO YANAUMBA..NIMEONA KAMA HAWA WAZAZI WAKIWA WANAJUA WAZAZI WAO WALIACHANA WALITAKIWA KUWAOMBEA WATOTO WAO WAACHANE NA LAANA NA VISASI VYA FAMILIA NI NZURI KUMUAANDA MTOTO KABLA UJAPIGWA UKAKIMBILIA MOSHI KUSEMA AMELOGWA KUMBE MGANGA MWENYEWE

SO NI VYEMA UKIPATA MTOTO KWENYE MAOMBI MWAMBIE MUNGU UNAITAJI NINI JUU YAKE..MI SIKUFICHI NAMWOMBEA MUNGU MWANANGU KILA USIKU APATE SHULE NZURI AFIKE CHUOKIKUU AMALIZE APATE PHD kama babu yake ingawa babayake aliikimbia
aolewe na mwanaume mwema kutoka kwa MUNGU asipende anasa ampende MUNGU amtamani Mungu katika maisha yake yote nakwambia mama didy anafika wakati anasema jamani mbona mdogo nkamwambia unataka kuletewa watoto hapa mtoto ajaolewa useme MUNGU amekuacha...so ni vyema wazazi kuona mbele badala ya kunusa
kila lakheri
 
Back
Top Bottom