Eti Uzalendo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Uzalendo!!!

Discussion in 'Sports' started by Twilumba, Mar 17, 2011.

 1. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Wadau habari za Asubuhi

  Nimekutana na hii article Global publishers,

  Kampuni ya Global Publishers ikishirikiana na Clouds Media Group limeandaa tamasha la wazi na la bure lililopewa jina la “TAMASHA LA UZALENDO: TANZANIA KWANZA, SISI SOTE NI NDUGU”.

  Tamasha hili Kubwa, linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 26 Machi, 2011 katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam kuanzia, saa 5:00 asubuhi hadi saa 12:30 jioni.

  Madhumuni ya tamasha hili ni kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kuishi pamoja kwa upendo na amani bila kujali tofauti zao. Vilevile kuwahamasisha kuipenda nchi yao na kupendana kama binadamu na kuweka uzalendo mbele kwa maslahi ya taifa. Tamasha hili linakadiriwa kujumuisha watu kati ya 20,000 hadi 25,000 wa rika tofauti na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa makampuni na taasisi mbalimbali wanaoheshimika na jamii, ambao siyo wanasiasa.

  Tamasha linatarajiwa kuvuta watu wengi kutokana na maudhui yake pamoja na kauli mbiu yake ya kuhimiza na kuhamasisha mapinduzi ya kifikra kwa kuwajenga watanzania wawe na uzalendo na moyo wa kupenda nchi yao. Kwa kufanya hivyo, wataweza kuongeza upendo miongoni mwao na hii itasaidia kulinda amani na utulivu tulio nao na tunaojivunia.

  Kwa kipindi kirefu sasa, nchi ya Tanzania imekuwa katika vita ya maneno kati ya wanasiasa wanaokinzana na hivyo kwa namna fulani kuathiri watanzania wengi kutokana na misimamo na matamshi yanayowakatisha tamaa wananchi wengi. Tamasha hili litakuwa ni fursa ya kipekee ya kurejesha matumaini kwa kufufua chachu ya kutaka kuwa wazalendo, wenye uchu wa kulinda nchi yetu na kuonesha mapenzi kwa kila kitu kinachohusisha Utanzania, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi na vyama.

  Ujumbe wa tamasha hili ni muhimu sana kwa kila mtanzania atakayefika pamoja na wale watakaosikia habari zake. Ili ujumbe uweze kufika kwa ufasaaha, kunatarajiwa kuwepo wanaharakati watakaozungumza siku hiyo, wakiwemo Eric Shigongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Joseph Kusaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group na wengineo.

  Tamasha hili linatarajiwa kusindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa bendi na vikundi mbalimbali vya sanaa. Kati ya burudani hizo ni muziki wa dansi kutoka kwa bendi za African Stars, Msondo Music Band, DDC Mlimani Park, TOT Band na Stone Mayiyasika. Vile vile kutakuwa na muziki wa taarabu ambapo bendi za Jahazi Modern Taarab na Super Shine Modern taarab zitatumbuiza.

  Vijana wakiwa ndiyo kundi kubwa linalowakilisha idadi ya Watanzania wengi, burudani ya bongo flava itakuwepo huku wasanii wengi wakionesha nia ya kushiriki. Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Profesa Jay, AY, H. Baba, H-Mbizo, wasanii kutoka Zizzou Entertainment, mwimbaji wa injili, Flora Mbasha na wengineo wengi.

  Mbali ya wasanii hao, atakuwepo pia mwanamuziki mkongwe wa Reggae, Innocent Galinoma, Mtanzania aishiye nchini Marekani, ambaye amejipatia umaarufu kutokana na nyimbo zake za kizalendo kama vile “Sote ni ndugu” na “Kilimanjaro”.

  Maswali ninayojiuliza:

  1. Waaandaaji wana nia ya Dhati ya kupromote sambamba na madhumuni ya tamasha waliyoyataja?

  2. Organizers wa hii kitu wote ni wapinga mapinduzi, je huo uzalendo wanaotaka kuu-promote ni kwa faida ya nani?

  3. Nawasilisha kwa ajili ya mjadala wasanii watakaotumbuiza mbona ni wale waliokuwa kwenye kampeni za CCM kwenye kampeni za Urais 2010?

  34 Kuna wasanii kama Roma, JCB na Joe Makini hawajaona haja ya kuwaalika wakati ni wanamapinduzi muhimu?

  My take
  Kuna Ka-element ka -uchama na Ufisadi wa kujipatia Fund kutoka kwa sponsors kwa manufaa ya wachache.

  Na hivyo si Tamasha hili si kweli kuwa ni la kuwakumbusha watanzania habari ya uzalendo na kuishi pamoja kwa Amani, kuna zaidi ya hilo lenye manufaa kwa wachache!!!

   
 2. G

  Gathii Senior Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwenye macho haambiwi tazama,tumia mifumo yako yote ya fahamu utaona tu na kufahamu lengo la hilo tamasha..
   
 3. K

  Kana Amuchi Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  upuuzi mtupu. ni kuunga mkono hotuba ya JK. fullstop. hawa ni makuwadi wake tu, na wanaojaribu kujipatia kipato kwa ujanjaujanja. nenda kama hutaona wanaccm tu kila kona, na maneno na nyimbo na misamiati na mafumbo na nahau na vijembe vya kisisiemusisiemu.
   
 4. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivyo vyombo ni matawi ya CCM, huitaji kupata hata elimu ya chekechea kulijua hilo. Kimsingi ni tamasha la CCM lililoandaliwa kuwalinda viongozi mafisadi na litakuwa limeratibiwa na wao. Global Publisher Shigongo alidhibitiwa kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM , Clouds Media Groups wapiga kampeni wakuu wa CCM. Naamini fedha zetu za umma zitaendelea kutumika vibaya kufadhili usanii huu.
   
Loading...