Eti ni kweli Rais wetu amesafiri na watu 50 & Freeman?

Eti ni kweli Rais wetu amesafiri na watu 50 & Freeman?

Status
Not open for further replies.
Mzee ES,
Boaz alikuwepo. Tena alikaa kiti cha mbele lakini inaonekana hana issue na JK kama alivyokuwa na Ben. Hata JK alimtaja na kumpa nafasi ya kusema.
Hizo rumours za ubalozi nimezisikia lakini sikuwepo kwenye hafla ya Millenium ambapo nasikia kuna watu walimtonya JK juu ya mabaya ya ubalozi wetu mbele ya mheshimiwa balozi.
 
Ni kweli balozi Daraja alipakwa mbele ya Kikwete na mbele Dr. Migiro.. I heard it from the reliable source ambaye alikuwepo hapo pembeni.... Si

Mzee ES, mimi niko unbiased...naripoti tu kile ninachokipata na kujaribu kuweka mambo sawa. Hakuna kitu kibaya kama rumours.. so ni bora kuwekana sawa mapema
 
Jasusi,
Bila shaka nikishuka mitaa hiyo nitakutaarifu.
Katika habari za udaku, eeeh bwana wee ebu nipe kweli ya maneno haya. Inasemekana kuna mchawi mmoja alisimama na kumwomba rais amuondowe EL ktk uwaziri mkuu kwa sababu ameiba sana mali ya UMMA na hata kudiriki kusema utajiri wake wote kaupatia kwa wizi..habari hii ya kweli?
Kwa habari zinazosambaa nasikia ktk hiyo dinner - JK aliuliza, huyo mshenzi gani ?...jamani hawa watu wanatoka wapi!
 
Mzee Mwanakijiji,

Mengi yanayoulizwa kuhusu hii safari ya rais wetu sio udaku, ila ni ukweli uliotendeka,

(1). Freeman alikuwepo DC, wakati rais akiwepo,

(2). Rais alifuatana na watu wapatao 50, 15 kati yao walitangulia DC kumtayarishia safari! rais wetu! Na wengine ilibidi wabaki NY rais akiwa DC kwa ajili ya kukosa nafasi za hoteli kutokana na kuwa wengi mno kuliko taratibu za itifaki! Na hata State Department ya US imeliona hili na kuliulizia!

(3). Hakukutana rasmi na Bush kama magazeti uchwara ya huku bongo yalivyojaribu kutupandisha mkenge!

(4). Na kwamba rais akiwa pale hotelini kuna kimwana wake mmoja toka Texas ambaye zamani alikuwa mwandishi wa magazeti, alikuwa akimvizia pale hatelini wazee wa secret service ikabidi wamrudishe Texas! (huyu mwanadada anaitwa Honeymoon amekuwa akijimwaga na mzee kwa muda mrefu sasa toka enzi zileeeeeeee! Sasa hakujua kuwa mambo yamebadilika!)

(5). Mzee JK alikataa zile hoteli za dola $ 5000 kwa siku, ambazo BM bado hadi leo anazifikia.

Sasa ninaandika hizi habari ili kuweka mambo yanapotakiwa na kwa usawa, ni mambo yaliyotokea hakuna udaku hapa wala hadithi, halafu tunapoandika hapa hatuzushi ila tunakuwa na data za kweli, sasa tunawezakutumia maneno kama "Nasikia" ili kudanganya toto, lakini ukweli tunakuwa nao, hatuandiki hadithi hapa,

Shukrani kwa wale wote mnaotuwekea ukweli wa mambo yaliyotokea live kwani ndio hasa kiini cha forum kuwa na credibility na ndugu zangu wote mliochangia hapa yote kumi hakuna tisa na tuendelee kuweka vitu hapa ili hawa viongozi wasifikiri wabongo wote tumelala ni lazima tuwafuatilie kujua kila wanachofanya kwa faida ya wananchi walipa kodi,


Mzee Jasusi,

Sasa I am troubled na news za mzee Boaz, kuwa amekuwa compromise kwa JK, hadi JK kumuinua aongee! I am lost kwa hiyo beef yake ilikuwa na BM kwa ajili ya nini? Kwa kweli nitamtafuta animegee yaliyomsibu au ameahidiwa cheo naye? Yaani I was banking on him kumtoa jasho JK!
 
Mzee ES, Mkandara,
Uliyoandika Mzee ES utadhani ulikuwepo. Boaz alipopewa nafasi ya kuuliza swali alianza kutoa maoni akimsifia JK kwamba kuna mengi mazuri amefanya lakini bado kuna mengi mabaya ambayo anahitaji kuyashughulikia. Lakini alitolewa nishai kesho yake alipokwenda hotelini kujaribu kuonana na JK. Alipopoanda juu akarudishwa na walinzi. Akasubiri pale nje karibu na gari lakini JK alipotoka nje aliingia haraka kwenye gari bila hata kusalimiana naye. Mzee ES umenitoa jasho juu ya Honeymoon. Huyu alinipigia simu akiuliza juu ya mipango ya Washington kumbe alikuwa na lake jambo? Na kuhusu Lowassa, walikuwepo vijana kadhaa pale, wakati rais anazungumza wakapaaza sauti zao wakiuliza juu ya Lowassa, lakini JK aliwapuuza akaendelea. Lakini hii ya entourage ya watu 50 haiingii akilini kabisa. Hii haikuwa state visit, na wote hawa walikuja kufanikisha nini?
 
Sasa Mzee Jasusi,

Hii habari ya Mzee Boaz inapaswa kuwa fundisho kwa wale wote wenye tabia za ufeki, kuwa wanasiasa ndio feki original haswa! Huyu mzee Boaz alifikiri kwa kumsifia mzee JK atakuwa sawa naye ili akamuombe kazi, LO! Aibu hiyo mtu mzima! Yaani mtu mzima hovyooooooooooooooo!

Huyu mwanamama yaani ni aibu tupu, halafu wazee wa Texas wanamuandika kwenye mitandao yao kuwa ni mmoja wa kina dada wa huko wenye ngoma! Sio siri!
 
Bravo kwa wabongo wote wa Texas kwa msimamo wao mkali, wa kuwafahmisha ndugu wabongo wote kuhusu kina dada na kinakaka wenye ngoma katika mitandao yao, huo ndio uungwana na huyu dada yumo kwenye list yao,

Hiyo inawasaidia wabongo kutopanda mkenge, wazee wa Texas BRAVO!!!
 
Jasusi said:
Mzee ES, Mkandara,
Uliyoandika Mzee ES utadhani ulikuwepo. Boaz alipopewa nafasi ya kuuliza swali alianza kutoa maoni akimsifia JK kwamba kuna mengi mazuri amefanya lakini bado kuna mengi mabaya ambayo anahitaji kuyashughulikia. Lakini alitolewa nishai kesho yake alipokwenda hotelini kujaribu kuonana na JK. Alipopoanda juu akarudishwa na walinzi. Akasubiri pale nje karibu na gari lakini JK alipotoka nje aliingia haraka kwenye gari bila hata kusalimiana naye. Mzee ES umenitoa jasho juu ya Honeymoon. Huyu alinipigia simu akiuliza juu ya mipango ya Washington kumbe alikuwa na lake jambo? Na kuhusu Lowassa, walikuwepo vijana kadhaa pale, wakati rais anazungumza wakapaaza sauti zao wakiuliza juu ya Lowassa, lakini JK aliwapuuza akaendelea. Lakini hii ya entourage ya watu 50 haiingii akilini kabisa. Hii haikuwa state visit, na wote hawa walikuja kufanikisha nini?

Jasusi,

Kumbe unafahamiana na huyo dada Honeymoon?! Nilimuona nilipotembelea Houston mwaka 2004. Ina maana mhishimiwa alikuwa hana taarifa naye, au?
 
Mzee Watu Wewe!,

Mheshimiwa lazima alikuwa na taarifa naye na ni lazima ndiye aliyemfahamisha kuwa anakuja kwani, isingwezekana yeye kuwa na details zote alizokuwa nazo kuhusu safari hiyo, Kwa sababu tunasikia alifika NY kwa ndege siku moja kabla,

na yeye akachukua chumba pale pale hoteli ya mzee, na mzee tunasikia ana mpambe wake pale ubalozi wtu Ny ndiye aliyekuwa co-ordinator, tatizo ni wazee wa Secret Service wao wanajua rais wetu kaja na mke wake that is it, nasikia mzee wetu alijaribu kila njia kushuka chini ili ajisuuze lakini wapi wazee waligoma kata kata ndipo baadaye wakshituka na kumchukua mwanadada na kumrudisha TX, to their suprise akatokea tena DC!
 
Mwanakijiji,
Lowassa naye anatinga karibuni NY eti kuhudhuria mkutano wa UN kuhusu ukimwi. Sasa si Waziri wa afya angetosha kabisa kuongoza delegation, lazima waziri mkuu?
 
Nimesikia hilo pia...halafu anafanya ziara falme za kiarabu (ambako Kikwete amekwenda wiki mbili zilizopita...) halafu London (kikwete amepita kuwasalimu huko)... halafu Marekani (Kikwete ametoka huko!) hii duplication ya safari ina ulazima gani!! Kwanini EL asiende kama Saudi Arabia au Kuwait.. halafu German etc....Unless kuna watu ambao Kikwete alikutana nao na Lowassa anafuatilia mitkasi!!!
 
Mzee mwanakijiji

Hizi safari zote unazoziona ni kwa ajili ya deals zao na sidhani kama ni kwa manufaa ya taifa. Mara nyingi, mkuu wa nchi huwa anakwenda kuongea na mkuu mwenzake wa nchi husika na kuangalia maeneo yanayohitaji attention. Wakishakubaliana wakubwa kwa wakubwa, kinachobaki ni watendaji wa maeneo husika katika nchi zote mbili kumalizia yaliyokubaliwa.

Mikataba ikishafikia mwisho, mabalozi wanaingia kuziwakilisha nchi hizo mbili katika hatua za mwisho za kumwaga wino. Hivyo basi, Raisi akimaliza ziara yake katika nchi fulani, wanaoweza kusafiri nyuma ya Raisi kwa ajili ya ufatiliaji na utendaji ni watendaji wa sehemu husika za serikali. Waziri mkuu ni mtu mkubwa katika serikali kumfuata Raisi nyuma. Anakwenda kufanya nini ambacho Raisi hakufanya? Mfano, Nyerere na Kaunda walikwenda china na baadae kukafuatiwa na ziara za mawaziri wao na siyo waziri mkuu. Baadae wasomi na watendaji wa wizara za ujenzi. Matunda yake, kitu hicho, Reli ya Tazara.

Mimi naziona hizo kama ziara za kuendeleza deals zao binafsi na siyo kwa manufaa ya taifa. Lowasa ni Tajiri. Mimi napenda sana mambo ya zamani. Badala ya kuanza upya tungeyaendeleza na kurekebisha yale mabovu. Tumeachana na ziara kwa wananchi tumekimbilia ziara za nje. Hata juzi nimesikia kuwa ziara za wanawake nje zitaongezeka. Tumesahau watu waliotuweka madarakani, hatuwashirikishi tena.

Siku hizi ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kutekeleza mambo ya nchi umefifia kidogo. Huko nyuma pamoja na matatizo makubwa ya usafiri viongozi walikuwa wanafanya ziara na mikutano mingi ya wananchi. Siku hizi kila kiongozi ana shangingi na hakuna kitu.

Ziara na mikutano hiyo ilikuwa na faida mbili. Kwanza viongozi walikuwa wanapata nafasi ya kutoa maelezo ya undani kuhusu sera na mipango ya utekelezaji. Viongozi wengi walihusika ikiwa ni pamoja na Rais, mawaziri na hata wajumbe wa halmashauri kuu ya chama pekee cha siasa kwa wakati ule. Wananchi waliohudhuria mikutano ya hadhara walikuwa wengi na kwa maana hiyo elimu kwa umma ilikuwa pana zaidi.

Pili, wananchi walipata nafasi ya kutoa mawazo yao. Mawazo hayo yalitolewa kwa njia mbali mbali, kama vile risala, nyimbo, ngonjera, mashairi, ngoma, maigizo, maswali na maoni. Siku hizi ziara na mikutano ya wananchi imepungua sana. Hata hizo ziara zinazofanywa na viongozi nyingi ni ziara za kukagua miradi. Mazungumzo ya kiongozi anayetembelea mradi yanakuwa finyu kwa sababu yanalenga zaidi kwenye mradi unaohusika. Baadhi ya viongozi hawajulikani sana vijijini kwa sababu hawaendi huko mpaka kuwe na mradi.

Mawasiliano kati ya uongozi na wananchi siku hizi ni kupitia vyombo vya habari. Ni kweli vyombo vya habari vimeongezeka sana. Kuna magazeti mengi sana, redio nyingi, televisheni, majarida na tovuti. Ni kweli pia kumekuwa na uwazi mkubwa katika kutoa habari.

Serikali na taasisi nyingine, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, vinatoa habari nyingi sana. Rais anazungumza na wananchi kila mwezi na mazungumzo yake yanalenga kwenye masuala muhimu kwa nchi. Hutuba za viongozi zinachapwa kwenye magazeti, zinasikika na kuonekana kwenye redio na televisheni.

Redio na televisheni zinaendesha vipindi vya
majadiliano na katika baadhi ya vipindi hivyo wananchi wanapata nafasi ya kutoa maono na kuuliza maswali. Matangazo ya shughuli mbali mbali yanatolewa kwenye vyombo vya habari. Habari nyingi sana za Serikali na taasisi nyingi zinapatikana kwenye tovuti. Siku hizi inawezekana kujua hata kiasi cha fedha za Serikali zilizopelekwa wilayani na mchanganuo wake. Kwa maana hiyo elimu kwa umma imepanuliwa.

Hata hivyo kuna matatizo ambayo yanafanya elimu kwa umma bado iwe finyu kuliko huko nyuma. Kwanza, pamoja na wingi wa vyombo vya habari, ni wananchi wachache walio na nafasi ya kupata habari kupitia vyombo hivyo. Televisheni zinaonekana zaidi mijini kwa watu wenye uwezo. Hali ni hiyo hiyo kuhusu magazeti na redio nyingi. Redio chache zinafika sehemu kubwa ya nchi lakini kwa sababu ya umasikini si watu wengi wanaweza kuwa na redio. Tovuti bado ni ndoto kwa wananchi walio wengi.

Pili, vyombo vya habari vinatoa mambo mengi ya burudani na porojo zaidi kuliko elimu kwa umma. Redio nyingi zinafahamika zaidi kwa muziki na televisheni zinafahamika zaidi kwa maigizo na michezo. Magazeti yanayosomwa sana Dar es Salaam ni yale ya burudani na porojo. Zaidi ya hapo mwelekeo wa vyombo vya habari ni wa biashara zaidi, hivyo habari za malumbano na kukosoa ndizo zinapewa uzito zaidi.

Tatu ni kwamba mawasiliano ya vyombo vya habari zaidi ni ya upande mmoja. Wananchi wanapata habari lakini nafasi ya kutoa mawazo yao ni finyu. Wachache wanapata nafasi kwenye magazeti, redio na televisheni lakini walio wengi hawapati.

Kuna semina na mikutano mingi ambapo watu wanatoa mawazo lakini nafasi ya kuhudhuria semina zaidi ni kwa viongozi na wasomi. Watu wa kawaida wanahusishwa kwenye utafiti lakini kuhusishwa kwao si huru kwa sababu hadidu za rejea za utafiti zinatayarishwa na watu ambao watakuwa wameamua malengo ya utafiti huo.

Matokeo ya yote haya ni kwamba wananchi hawashiriki sana katika kuamua sera na kupanga mikakati ya utekelezaji. Pamoja na msisitizo wa ushirikishwaji wa wananchi, ukweli ni kwamba sera zinaundwa zaidi kutoka juu kwa msukumo wa utandawazi na wananchi wanashawishiwa tu kuzielewa na kuzikubali. Kwa sababu ya utandawazi wafadhili wana nafasi kubwa zaidi katika kuandaa sera kuliko wananchi.

Ushirikishwaji wa wananchi ni jambo la lazima katika kujenga muafaka wa kitaifa. Wananchi wakishirikishwa kwa ukamilifu wataelewa kwa urahisi sera za nchi, kuzikubali na kuwa na mshikamano katika utekelezaji.

Msingi wa kutumia vyombo vya habari kwa mawasiliano na wananchi ni mzuri. Lakini katika hatua ya sasa ya maendeleo bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwasiliana moja kwa moja na wananchi. Kwa hiyo bado kuna umuhimu wa viongozi kufanya ziara nyingi na kuwa na mikutano ya kawaida na wananchi badala ya kuwa mangimeza au kuona ziara za nje ni muhimu zaidi.

Siku hizi baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanafanya ziara vijijini na kuzungumza na wananchi. Hilo ni jambo la kutia moyo. Lakini bado viongozi wengi wanapendelea zaidi kukutana na waandishi wa habari. Ukumbi wa Maelezo umekuwa ndio uwanja mkubwa wa siasa. Hakuna sababu ya msingi kwa nini viongozi wasikutane moja kwa moja na wananchi, hata wa Dar es Salaam tu, na waandishi wa habari wakawafuata huko. Wakifanya hivyo wananchi watapata nafasi ya kutoa maoni na kuuuliza maswali. Hivi utaratibu wa kukutana na "wazee" wa Dar es Salaam ulikuwa na kasoro gani?
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala hii na kusema ukweli nimevutiwa na michango ya nguvu na iliyoenda shule inayotolewa na wanabodi.

Kyoma mimi nina ombi kwako , jee una mpango wowote wa kuandika kitabu ? kusema ukweli mawazo yako ni mazuri sana na ninahisi jamii ingenufaika sana kama yangewekwa kwenye maandishi .
 
Kyoma,
Vipi mbona unatutukana tena?...
Unajua huyo mtaalam wala hakufanya kitu zaidi ya kuuliza wavuvi ambao aliwakuta ufukoni. hakugusa maji wala kupanda mashua. Aliambiwa hivi - Enfwi zyona zafilwe!...ilibidi nae aombe tafsiri. :lol: :lol:
 
Mzee Mkandara

You are so funny! At a more serious note though, haya mambo yanatokea kweli kweli ingawa umeyaandika kwa njia ya kuchekesha. Si unakumbuka Abushiri aliuza ardhi kwa kipande cha nguo. Umesahau yale maandishi ya ulaghai ndani ya mikataba ya Karl Peter? Nadhani mababu zetu walikuwa wanaona kizungumkuti mithiri ya mgogo kusoma maandishi ya kikerewe. Ndiyo maana walitia dole gumba na kuzidiwa kete.

Ziara za viongozi wetu nje ya nchi, zimezaa akina Abushiri tele. Badala ya kukaa mahotelini wanapofikia na kuisoma mikataba ili waielewe, they all end up into promenade and shady avenue or complexes containing shops, restaurants, and other businesses and facilities for shopping. Wakirudi mahotelini wanakuwa wamelewa huku wakijivinjari na vifurushi mikononi mwao. Muda wa kupekuwa ile mikataba unakuwa umewatupa mikono. Wanachofanya ni kumwaga wino. Hivi ndivyo nchi yetu inavyouzwa.

Kama hivi ndivyo basi, nini tofauti kati ya Abushiri wa zamani na hawa ambao Jasusi aliwaona wamebeba vifurushi wakati wa ziara ya Kikwete huko Marekani? These new species are intellectually very proficient. I mean very educated but sadly, never cultivated.

Mzee Mkandara, ngoja niache porojo. You made my day too!
 
Kyoma,

Post zako ni ndefu, kutokana umuhimu wa elimu yenyewe, nakubali inabidi ziwe hivyo, Great thinking brother!

Wanabodi

Inakuwajekuwaje, hii mikataba inapita pita na tuna wazee wa system, whats their role ktk mikataba, Mzee Es/Babu Ubwete any idea.? wananchi tunaumia na mizigo ya mikataba feki!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom