Eti ndoa zimepitwa na wakati…………!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,332
Inaelezwa kwamba kupuuzwa kwa mila na desturi na maadili ya kidini kumechangia sana kuharibu tabia za vijana ikiwa ni pamoja na mambo ya urafiki, uchumba hadi ndoa. Ndio maana uchumba umegeuzwa kuwa ndiyo nafasi pekee ya vijana kukutana kwenye majumba ya starehe na hatimaye kufanya ngono. Na hapo ndipo unapokuja kugundua kwamba hata zile ndoa za kimila za kale zinazohusisha Kisarawanda, ili kuthibitisha kama bi harusi hajawahi kushiriki tendo la ndoa yaani kama bado ni Bikira, hazipo tena.

Utathibitishaje wakati hata kabla ya uchumba binti keshazipoteza zamani. Na ndio maana siku hizi hata ndoa zimeonekana kama zimepitwa na wakati. Vijana rijali tena wakiwa na siha nzuri hawako tayari kuoa tena, na badala yake wamekuwa wakiwabadilisha mabinti watakavyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,534
Mh hii mada hii ina mambo. Juzi nimekutana na rafiki yangu ambaye alitengana na mumewe ilhali wana mtoto mmoja; kanichekesha eti kwa kuwa anahitaji mtoto wa pili basi kamwambia huyo bwana ajiandae mkao wa kula amgaie tu hizo mbegu.... lakini kuishi pamoja kama mke na mume NO!. Inanifanya nitafsiri maana halisi ya ndoa!!
 
Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Kwahyo bora kutafuta mwanamke wakuzaa nae then kila mtu na kwake, afu mkitaka tena mtoto mnaitana mnageana mbegu zenu habari inaishia hapohapo.
 
Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,325
9,960
Mh hii mada hii ina mambo. Juzi nimekutana na rafiki yangu ambaye alitengana na mumewe ilhali wana mtoto mmoja; kanichekesha eti kwa kuwa anahitaji mtoto wa pili basi kamwambia huyo bwana ajiandae mkao wa kula amgaie tu hizo mbegu.... lakini kuishi pamoja kama mke na mume NO!. Inanifanya nitafsiri maana halisi ya ndoa!!

Marriage is like a dance,no matter how the music changes you keep on dancing............ wanandoa wakifuata falsafa hii bila shaka ndoa nyingi zitadumu. Na wanaoogopa kuoa wakiona ndoa zinadumu watapata moyo wa kuoa/kuolewa.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,951
287,542

MJ1, namjua mdada tena msomi wa hali ya juu. Alikuwa kaolewa na wakabahatika kupata mtoto mmoja lakini wakashindana. Basi ikafika wakati akawa anadai anataka mtoto wa pili ili huyo mkubwa asiwe mpweke lakini anataka na Baba yule yule wa mtoto wa kwanza. Huyu dada alikuwa majuu (jina la nchi kapuni) basi akamtafuta mwenzie na kumwambia kusudio lake. Jamaa hakumfanyia hiyana yoyote basi dada akafunga safari kwenda kuzichangamkia mbegu kwa huyo jamaa ambaye walishindana na ndoa kuvunjika. Hata mimi naona ndoa kwa siku za usoni zitapungua sana ukilinganisha na miaka ya nyuma na hizo chache zitakuwa hazidumu kwa miaka mingi.
 
AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,219
17,980
Mh hii mada hii ina mambo. Juzi nimekutana na rafiki yangu ambaye alitengana na mumewe ilhali wana mtoto mmoja; kanichekesha eti kwa kuwa anahitaji mtoto wa pili basi kamwambia huyo bwana ajiandae mkao wa kula amgaie tu hizo mbegu.... lakini kuishi pamoja kama mke na mume NO!. Inanifanya nitafsiri maana halisi ya ndoa!!

Yaani simlaumu huyo dada... nimemuelewa kabisa where she is coming from... ingawa kwa kweli inategemea mliachana kwa ajili gani... na mawasiliano kati yenu yapo vipi... maana kuachana then mna fanya tendo... nayo ngumu aisee! Nafikiri kubwa linalomsumbua ni kwamba ataki watoto wa baba mbali mbali... aidha kwa ajili ya kuhakikisha ukaribu wa watoto ama kuepusha kuzaa na mtu mwingine mwenyewe hamjui...
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,951
287,542
56181f0c464aa3739d0e2844f6ef.jpeg
The concept of rent-to-own is one usually applied to the purchasing of furniture, large appliances and various other household items. But should it be used in matters of the human heart too? Would human beings benefit from low-risk short-term commitments to each other rather than losing their hearts, homes and savings in one fell swoop with the all-or-nothing contract that is marriage?
It's a question being tossed around in Mexico at the moment.

Lawmakers in Mexico City are considering legislation that would radically alter the concept, if not the traditional meaning, of marriage. To combat high rates of divorce and the expensive legal process that results from dissolving the old 'Til death do us part' vow, legislators are proposing the creation of short-term marriage licenses that come with a built-in option to renew or dissolve at the end of a fixed term.
The licenses would be two years in length and would include clauses relating to custody rights and property division. At the end of the two-year term, the couple would be given the option to continue on in wedded bliss or to bid adios to one another once and for all.
To renew or not to renew? That would be the question facing the happy couple after two years.

The benefit to the Mexican legal system seems clear: it would cut down on lengthy divorce proceedings. But what are the benefits to the betrothed? On the one hand, the legislation appears to encourage a minimum commitment, as it requires people to give marriage a shot for at least two years-those who bail on a marriage before the end of the two years would have to go through regular divorce proceedings.

But that seems the only 'positive' aspect of the renewable license idea for couples. If anything, the trial nature of the arrangement seems to take the significance of commitment out of the equation-if there's no risk involved in commitment, what's the point? If you're married but not really married why bother with a wedding at all?

If it passes, the legislation may also necessitate some adaptations in the language of commitment. The first 18 months of marriage, which has traditionally been considered the 'honeymoon period', may need to be redubbed the 'should I stay or should I go?' period. And that's about as romantic as a new fridge don't you think?
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,812
12,406
Mh hii mada hii ina mambo. Juzi nimekutana na rafiki yangu ambaye alitengana na mumewe ilhali wana mtoto mmoja; kanichekesha eti kwa kuwa anahitaji mtoto wa pili basi kamwambia huyo bwana ajiandae mkao wa kula amgaie tu hizo mbegu.... lakini kuishi pamoja kama mke na mume NO!. Inanifanya nitafsiri maana halisi ya ndoa!!
Mmh!! Tunaelekea kwenye ndoa za mikataba sasa!
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,534
Katavi umeona eh?!

AishaDii nakuelewa kabisa na yeye hata alivyonielezea nilimwelewa but why the pretendency? Its either urudiane naye for good (second and forever chance) kuliko unarudi nusu! Suppose naye akitaka mtoto wa tatu kwa mama yule yule? Akimfuata atakubali?
 
nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Na hapo kutakuwa kuna mtu/watu wanadhulumiwa. Hainiingii akilini watu kuachana afu waendelee ku do; just for the kid na wote waone ni good idea. Bado wanapendana hao na watarudiana tu.

Tukirudi kwenye mada; ndoa ni ya wawili na kila mtu ana experience ambayo ni tofauti na mwingine; For me I still believe in marriage; I might be old fashioned ila hata wanangu ntawalea kuwa na maadili hayo. Sifagilii kabisa maisha ya kisela.

Katavi umeona eh?!

AishaDii nakuelewa kabisa na yeye hata alivyonielezea nilimwelewa but why the pretendency? Its either urudiane naye for good (second and forever chance) kuliko unarudi nusu! Suppose naye akitaka mtoto wa tatu kwa mama yule yule? Akimfuata atakubali?
 
AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,219
17,980
Katavi umeona eh?!

AishaDii nakuelewa kabisa na yeye hata alivyonielezea nilimwelewa but why the pretendency? Its either urudiane naye for good (second and forever chance) kuliko unarudi nusu! Suppose naye akitaka mtoto wa tatu kwa mama yule yule? Akimfuata atakubali?

Hapo sasa mtihani kwa kweli.... inakua kama mnadimba fulani hivi....
 
The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,615
5,966
Katavi umeona eh?!

AishaDii nakuelewa kabisa na yeye hata alivyonielezea nilimwelewa but why the pretendency? Its either urudiane naye for good (second and forever chance) kuliko unarudi nusu! Suppose naye akitaka mtoto wa tatu kwa mama yule yule? Akimfuata atakubali?
Nimesoma comment yako nimecheka sana ila it does make a lot of sense
 
The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,615
5,966
Marriage is like a dance,no matter how the music changes you keep on dancing............ wanandoa wakifuata falsafa hii bila shaka ndoa nyingi zitadumu. Na wanaoogopa kuoa wakiona ndoa zinadumu watapata moyo wa kuoa/kuolewa.
Watu wakifuata maadili na nini kinahitajika kwenye ndoa basi ni hakika ndoa nyingi zitadumu sana
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,748
7,756
Mh hii mada hii ina mambo. Juzi nimekutana na rafiki yangu ambaye alitengana na mumewe ilhali wana mtoto mmoja; kanichekesha eti kwa kuwa anahitaji mtoto wa pili basi kamwambia huyo bwana ajiandae mkao wa kula amgaie tu hizo mbegu.... lakini kuishi pamoja kama mke na mume NO!. Inanifanya nitafsiri maana halisi ya ndoa!!

dahhhh,....yaani nishaachana nae...mimi na maisha yangu naye ana yake, halafu anijie eti nimzalishe?
HAPANA AISEE...hata kama nilishazaa nae watoto wengine, hiyo haikubaliki.
anyway,...siwezi wasemea wengine kwakuwa tu mimi nilipitia bad breakups....acha nilee niliojaaliwa.
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,748
7,756
Marriage is like a dance,no matter how the music changes you keep on dancing............ wanandoa wakifuata falsafa hii bila shaka ndoa nyingi zitadumu. Na wanaoogopa kuoa wakiona ndoa zinadumu watapata moyo wa kuoa/kuolewa.

Watu wakifuata maadili na nini kinahitajika kwenye ndoa basi ni hakika ndoa nyingi zitadumu sana

...lol,...naomba ufafanuzi!
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,534

dahhhh,....yaani nishaachana nae...mimi na maisha yangu naye ana yake, halafu anijie eti nimzalishe?
HAPANA AISEE...hata kama nilishazaa nae watoto wengine, hiyo haikubaliki.
anyway,...siwezi wasemea wengine kwakuwa tu mimi nilipitia bad breakups....acha nilee niliojaaliwa.
Loh Mbu watu wanazo guts aisee. Yaani mie nilivyokuwa nasimuliwa sikutaka kuamini. But the ishu ni kuwa mke kashiklilia mpini mume makali. Maana mume alishaleta za kuleta akalazwa ndani kwa RB. Baada ya muda anabembeleza kurudi kwa familia yake so mke anaweka condition............hakuna kuishi pamoja but kwa kuwa nahitaji mtoto wa pili, jiandae, zitayarishe mbegu hizo mie najazichukua naincubeti.......... mwisho wa mchezo!!

Maisha haya! Ni hakika kabisa kuwa ni mchanganyiko balaa
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,615
5,966

dahhhh,....yaani nishaachana nae...mimi na maisha yangu naye ana yake, halafu anijie eti nimzalishe?
HAPANA AISEE...hata kama nilishazaa nae watoto wengine, hiyo haikubaliki.
anyway,...siwezi wasemea wengine kwakuwa tu mimi nilipitia bad breakups....acha nilee niliojaaliwa.
Mbu mimi bado natafakari huyo rafiki yake MJ1 mimi naona kama is more of a pleasure ila dah hata kama ni mimi no way ila sijui wana makubaliano gani au wako katika hali gani
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

God bell

JF-Expert Member
May 13, 2011
591
208
Maisha ya ndoa ni matamu sana. Mimi mwenye nimekufa na kuoza kwa ndoa yangu ilivyo nzuri. Sasa nilipoisoma hii thread ya huyu jamaa na wengine jinsi wanavyoilalamikia ndoa, haijaniingia akilini kabisa kwani kwa upande wangu nimefika jamani. Yani mim na mke wangu tunapenda na kuheshimiana c kawaida jamani. Ila hatukomi kumpiga shetani vita kila kukicha. Polen wenye matatizo ya ndoa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom