Eti nchi Masikini!! Ni wangapi wapo Istanbul?

Mkasika

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
391
155
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Dkt. Anna Tibaijuka akiwa na Waziri wa Ofisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyihaji Makame (katikati) na Mbunge wa Kigamboni, Dar es Salaam, Dkt. Faustine Ndugule wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano wakati walipohudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 
Chukua Chako Mapema,ndiyo philosophy ya nchi yetu,tangu enzi ya Mzee Ruksa mpaka sasa!
 
Hivi heading na maelezo mbona naona tofauti..??au labda nina matatizo!!
 
hivi inakuwaje waziri wa serkali ya muungano akae pembeni mwa waziri wa zanzibar? au kwa vile mkutano uko uturuki inchi ya kiislam kama zanzibar?
 
Seminars na mikutano kila kukicha na bado tupo pale pale.
Wanaenda kupunga upepo naona. Si ajabu wakirudi ya huko yote washayasahau.
 
waliweza kuwahi semina elekezi?

kwa kweli ukiwa mwanasiasa bongo wala huhitaji mshahara kabisa. posho za semina na mikutano pekee unajenga na mapocho[pocho yote unapata. kumbuka vigari kama tu VX ni bure kabisaa, jamani, ngoja na mimi nianze kuweka mikakati ya kuwa mwanasiasa! nimechoka kufanyishwa mikazi na wanasiasa huku mshahara wangu wao wakiupata kwa sitting moja tu.
 
Huyo ustaadhi hapo kati ni vipi tena au kala kungu??

Duuh sheikh hivi haya maneno huwa mmelala nayo ni kuyachomoa tu na kurusha? yaani nimecheka mbavu sina. Kweli JF in raha hata km ulikuwa na jhasira utacheka tu.

Mie sisemi.
 
Back
Top Bottom