Eti Kila Mwalimu atapewa laptop?

jaxonwaziri

JF-Expert Member
Feb 17, 2010
375
195
Najiuliza, haka ni kale ka-mwimbo ka Prof J kanatimia ama?

I like dreaming, and I dream big but this kind of dreaming is completely insane Mr Presida..!

Nimesikia ukiwasimulia watoto waliokuja kukuona hapo magogoni kuwa eti, kwenye hako ka-kauli mbiu kanakosema "..Tanzania beyond tommorrow.." eti kila mwalimu atakuwa anamiliki laptop yake! Mr Presidaa are you serious? Sane? Napata picha kama babu anawasimulia wajukuu zake hadithi vile? Na tunajua kuwa hadithi wakati mwingine hazina ukweli, ila zinafundisha! Napata tatizo ninapojaribu kufanya uamuzi wa ama ulikuwa unasimulia hadithi kwa wajukuu zako ama ulikuwa unaota wakati wa mchana (day dreaming)

Hebu twende pamoja:
Lini huo utafiti umefanywa kuonyesha kuwa what teachers need is laptops na sio malipo mazuri, mazingira mazuri ya kazi, shule zilizojitosheleza kwa kila kitu kuanzia maabara, maktaba n.k, kurejeshewa heshima na hadhi yao mbele ya jamii, na pia mafunzo ya kutosha kwa waalimu hawa?

Ndugu Presidaa, shule ngapi zina umeme unahitajika ku-chaji hizo laptops?

Halafu Mr. Presidaa, hizo laptop wazifanyie nini? Dont tell me ni za kuandalia masomo na kutunza kumbukumbu!

Mr Presidaaa, unafahamu hatutakiwi kuangalia laptop kama kitu cha kifahari na tunatakiwa kurudi kwenye ukweli kuwa laptop ni kitendea kazi kama vitendea kazi vingine mfano wa kalamu, nyundo, msumeno n.k?

Kuna haja gani ya kumpatia mtenda kazi kitendea kazi ilhali hathaminiwi, mazingira ya kazi ni mabovu, taaluma ya utendaji kazi haijaboreshwa?

Mbona nahisi mawazo haya yana serious error??

Is this the way Mr Presidaa is supposed to be thinking? Kweli? Yeye na wasaidizi wake?
Its horrifying to have a president who thinks this way!

Haya, lets say wamepewa, and lets suppose zimegawiwa kwa waalimu wa sekondari tu, za kata included, zimekadiriwa kuwa na life-span ya muda gani? Ama matengenezo yatahitajika baada ya muda gani? Yatafanywaje? Yata simamiwa na nani? Kwa fedha ipi? Tunahakikishaje laptop hizo zitakuwa zinafanya kazi iliyokusudiwa? Re-placement ni baada ya muda gani? Serikali hii itakabiliana-je na habari za .." ...laptop zimeeibwa.." ama "...zimepotea..."
Mr Presidaa, zitakuwa na internet? Kweli? How?

Isije kuwa kuna ka-kampuni ka teknolojia kanatafuta soko na ka-meshafanya lobbying ya kutosha ili kuju kuzimwaga huku kwetu tanzania, hata kama ki-uhalisia hatuzihitaji?
Mr Presidaa, unayaangalia haya yote kwa macho matatu?

Halafu, mbona kama wazo hili la laptop limekaa kama la-ki "..ACADEMY...." ama .."...Ki-international school..." flani hivi. For sure mtu unayetaka kuboresha elimu shule ya sekondari Nkuu, ama shule ya msingi Kwembetutu kule Mbinga, shule ya msingi Mwinyi kule mjini Tabora huwezi kuanza kuzungumzia laptop, nildhani ungeanza kuzungumzia vyumba vya madarasa, madawati na hata White boards ili kuondokana na vumbi la chaki linalotokana na utumiaji wa blackboards!

Mr Presidaaa, are you serious?
 
Anatania tu, ukimbana sana atasema. Watu wengine hawajui utani, mimi nilikuwa naongea na watoto kitotototo.... halafu wao wanachukulia serious!!!

Anatania tu.... si unajua prezidaa wetu ni mtu wa matani sana.
 
Hi lini President wetu amekuwa serious? Ni kitu gani kipya ume learn from him in the last five years?
 
Jamani uchaguzi si unakaribia! au mmeshasahau?
Zitakuja ahadi kem kem za kupendeza zaidi ya hiyo.
 
Ndo ahadi kabla ya uchaguzi hizo subiri baada ya uchaguzi ndo umuulize utapata yalo moyoni mwake!
 
umeme wenyewe hakuna...muwape kwanza nyumba za kuishi....
 
Maskini Watanzania! Hivi tumefika mahali Rais wa nchi anaweza kuwachezea wananchi kiasi hiki? Laptop kwa Walimu wote? Labda angelisema laptop kwa lecturers wote wa vyuo vikuu kidogo tungemuelewa!!
 
Jamini tunashangaa nini na mkulu tuliambiwa alipimwa akili? nadhani sio uchaguzi tu, hii inaitaji tafakari ya kila . Either hii kauli ni vijembe kwa walimu au ni dharau.
 
Yaani mkwere kaona laptop ndiyo ishu??!! Kwa umeme upi hasa?? Hao walimu wanaolalamika kila siku hawajalipwa kesho ukampe laptop, si 'ataiuza' apate japo pesa ya kujikimu?!
 
Anatafuta kupoza ile kasheshe ya kauli yake kuwa hataki kura za wafanyakazi wakati walimu ni sehemu kubwa ya wafanyakazi aliosema hataki kura zao. Si unajua bado mzimu huo unamwandama?
 
Kama kuna baadhi ya shule hazina madawati wanafunzi wanasomea chini ya miti,hakuna vitabu,chaki na vibao kauli hii ni kebei kwa Watanzani (walalahoi) wanafunzi na walimu MUNGU IBARIKI TANZANIA
umeme wenyewe hakuna...muwape kwanza nyumba za kuishi....
 
tsk tsk tsk! watanzania wenzangu, why are we so ready to jump to conclusions without questioning the true situation? if one is able to log on to jamii forum and post something au kuchangia maada then nini kinawashinda ku google? umeskia a program called Tanzania beyond tomorrow, inahusiana na walimu kupata laptops na hiyo kitu inakushangaza then why not go to google and get the truth of the matter? haya kama unashindwa au unaona uvivu or something, let me help you out....Titled Tanzania Beyond Tomorrow, the initiative is intended to supplement the long-term government recruitment of teachers to curb the huge shortage of the personnel in primary and secondary schools.
yaani the key issue sio kuprovide laptops, ni kuprovide ICT solutions to cover the deficit of 85,000 teacher shortage! so no JK is not selling pipe dreams to teachers to keep them sweet, it's about providing a solution (And a rather innovative one in fact) to a problem that is affecting our children. so if it's not too much trouble please click.... www.tbtschools.org
The Tanzania Education Trust
 
Kwa kweli hapa presidaa kaingia chaka shule kibao hata walimu hazina,maabara wanaenda kwenda shule za majirani,umeme hakuna,madawati hakuna sasa unataka kuwapa laptop je umewawekea umeme au watatumia betri?hapa kwa kweli presidaa kaingia chaka.Afikirie jambo lingine.sikubali hata kidogo na hiyo issue
 
WATU mnaimani ndogo sana.......mliambiwa maishabora kwa kila mtz hayo hapo sasa mnafikiri kuna kitu hakiwezekani kwa jk
 
Back
Top Bottom