kwenu wanazuoni, wachambuzi, watafiti, watalaam wa JF na uongozi wa CHADEMA, asalaaaaaaaaaam Aleykum,
Leo nataka mnieleze uhusiano kati ya chadema na Jamii forums baada ya kufanana, kuoana na kurandana katika mambo yafuatayo;
(i) Rangi za ukuraza wa JAMII FORUMS zinafanana na rangi za BENDERA ya Chadema
(ii) Msimamo wa wana JF wengi na Chadema almost ni sawa.
(iii) Baadhi ya washirika wakuu wa JF pia ni washirika na viongozi wa Chadema
(iv) JF na CHADEMA wote kwa sasa wanadai wako kwenye vita dhidi ya ufisadi
(v) Walipua mabomu wa humu JF wanalipua na evidence (attachments) kama ilivyo kwa walipua mabomu wa Chadema (wazee wa nyaraka) ie Zito, Slaa, n.k
(vi) Kwa kufuatilia majadiliano mbalimbali ya humu JF inaonyesha kuna uhusiano wa kisiasa, kifamilia na ule wa kupashana habari kati ya wana JF na CHADEMA...
Kama kuna mtu nimemkwaza naomba aombe mungu amsamehe ila kwa sasa naomba kujifunza sihitaji kutukanwa wala kurushiwa maneno ya kejeri...
TUMSIFU YESU KRISTO