Eti jeshi linamtetea aliyeua watoto

Eti jeshi linamtetea aliyeua watoto

kuua ndio kosa kubwa zaidi duniani na mbinguni,mahakama ipelekewe kesi hii ili itafsiri sheria kama hajakosea.kwani alikua kikazi au eneo la kazi mpaka tuhitaji ufafanuzi wa jeshi?
 
ndo hapo jeshi linapochekesha
 
Haiingii hakilini jeshi kusimama na kumtetea meja aliyeua watoto waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya mwaka mpya. Hivi chombo kama jeshi kinaweza kuwa kinakurupuka hivi jamani, inamtetea kwanza hakijui mazingira ya tukio kwa sababu aliyekuwepo ni mtuhumiwa peke yake na hao watoto, wamewauliza watoto wengine wakasema wale walikuwa vibaka ???Hata kijana wa form six anaweza kuwa reasonable kuliko hao wanaotaka kumtetea huyu jamaaa. Ushahidi wa huyu meja ni nini? gari yake haina sehemu yoyote kuonesha kuwa waliipiga, hajachaniwa nguo, hakuna kitu chochote kuonesha kulikuwa na purukushani, sasa nini jeshi linakaa na kuanza kumytetea??? jeshi lilikuwepo kwenye tukio????

nimesikia kwenye magazeti leo asubuhi. . . .

Ndugu,hawa watoto walikua hawajalala usiku mkubwa namna ile?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
nimekuelewa mkuu

Mkuu wasikukutishie na hoja zao za kufilisika. Uliyoelezea kwenye thread yana busara kabisa kabisa. Ona hoja zao zilivyo za kipumbavu;
1. Kwa kuwa walikuwa hawajalala mpaka saa 7 basi sio watoto
2. Na kama sio watoto basi ni haki yao kuuawa.
3.Jeshi ni taaasisi na imeshasema wenye makosa ni marehemu basi lazima tuamini.
4. Ni sahihi kabisa kuuawa kwa sababu waliparamia gari yake.
 
Hujui ulisemalo kijana. Watu kadhaa wmeripoti kupigiwa magari yao kama sehwmu ya sherehe za mwaka mpya. Hata hivyo bado swali halijajibiwa, mtoto anakwenda kuzurura usiku wa manane kisa sherehe za mwka mpya? Kizazi cha dot com mnaokwenda na watoyo wenu baaa. Hovyo kabisa.

umeeleweka mkuu, hizo kesi za kjpigiwa magari zimeripotiwa wapi? mbona gari yake haijaumizwa? lakini nimekuelewa kiongozi . . .
 
Hiv alietoa ruhusa ya mwaka mpya kusherekewa kwa vurugu na kuleta bughudha kwa wengine ni nani??

Kwangu mimi naona mjesh alikuwa sahihi kujilinda yeye,mali zake (gari) na familia yake pia waliokuwa kwenye gari.
Ripoti za huko zinaonesha na kuthibitisha kuwa hao vijana (tena siyo watoto ,kama unavyosema) walikuwa wanafanya hizo vurugu kwa watu wengi na walileta uharibifu kwa magari mengine.
Ifike mahali tuwe tunaheshimiana.
 
Hujui ulisemalo kijana. Watu kadhaa wmeripoti kupigiwa magari yao kama sehwmu ya sherehe za mwaka mpya. Hata hivyo bado swali halijajibiwa, mtoto anakwenda kuzurura usiku wa manane kisa sherehe za mwka mpya? Kizazi cha dot com mnaokwenda na watoyo wenu baaa. Hovyo kabisa.

Ukinionyesha sheria yeyote inayosema mtoto akizurura usiku wa manane mwaka mpya basi na auwawe kwa kupigwa risasi basi kweli nitaamini sijui nilisemalo!
 
Baada ya kufanya tukio lile alitakiwa kutoa ripoti polisi lakini yeye kaenda nyumbani kwake katulia hadi aliposhikwa na polisi.
 
Kichwa cha habari ulio andika kinaonesha wazi kuwa weye ndg una hasira sana. Nilidhani ni mjeshi mwingine ameamua kuua watoto wake tu halafu anatetewa.
To the point;
Hivi weye umewahi kuendesha gari mahali ambapo pana giza giza usiku halafu ukute labda mawe makubwa njiani? Unajisikiaje? Uwe unaendesha gari usiku, ghafula uvamiwe na watu pande zote mbili za gari na hata mbele na nyuma wanapigapiga gari yako, wengine wamebeba fimbo na vitu mbali mbali usivyoweza kuvitambua kwa sababu ya kelele zao. Utajisikiaje?
Simtetei huyo mjeshi. Lakini mimi nasema kama mimi, alichanganyikiwa. Hakujua nia ya hao watu. Angekuja hapa jf na kulalamikiwa kuvamiwa na kuibiwa gari na bastola yenye risasi usiku wa saa saba, weye ungekuwa wa kwanza kumdharau.
Naomba hili liwe funzo kwa wananchi wa TZ kuwa tuepuke kusherehekea kupita kiasi. Sherehe yako isiwe kero kwa wengine. Mjeshi alikuwa anapita kwenye barabara ya watu wote inayotakiwa ipite magari sio uwanja wa sherehe. Wala hakukuwa na ishara kuwa kuna sherehe huko mbele hivyo endesha taratibu.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.
Hao wenye sherehe zao walizidisha kipimo yaani walivuka mpaka. Waliposikia hiyo risasi ya kwanza ilitosha kuwa alert kuwa huyu mtu ni kichaa wakimbie lakini wakazidi kushangilia kwa kuivamia gari. Akaongeza mzigo..
Mimi si wakili lakini nawasilisha
 
Hiv alietoa ruhusa ya mwaka mpya kusherekewa kwa vurugu na kuleta bughudha kwa wengine ni nani??

Kwangu mimi naona mjesh alikuwa sahihi kujilinda yeye,mali zake (gari) na familia yake pia waliokuwa kwenye gari.
Ripoti za huko zinaonesha na kuthibitisha kuwa hao vijana (tena siyo watoto ,kama unavyosema) walikuwa wanafanya hizo vurugu kwa watu wengi na walileta uharibifu kwa magari mengine.
Ifike mahali tuwe tunaheshimiana.

Lakini wewe huoni pana walakini kwenye hii issue ya mwanajeshi aliyeua? Kwanini jeshi likurupuke kumtetea mtu aliyeua wakati bado mazingira ya kuua hayajafanyiwa uchunguzi? Wa kusema ANA au HANA makosa ni mwajiri wake au ni mahakama? Nadhani waafrika wengi bongo zetu zimeathiriwa na mazingira tunayokulia ndio maana hatuoni uzito wa mtu kuua au kuuawa!
 
Kichwa cha habari ulio andika kinaonesha wazi kuwa weye ndg una hasira sana. Nilidhani ni mjeshi mwingine ameamua kuua watoto wake tu halafu anatetewa.
To the point;
Hivi weye umewahi kuendesha gari mahali ambapo pana giza giza usiku halafu ukute labda mawe makubwa njiani? Unajisikiaje? Uwe unaendesha gari usiku, ghafula uvamiwe na watu pande zote mbili za gari na hata mbele na nyuma wanapigapiga gari yako, wengine wamebeba fimbo na vitu mbali mbali usivyoweza kuvitambua kwa sababu ya kelele zao. Utajisikiaje?
Simtetei huyo mjeshi. Lakini mimi nasema kama mimi, alichanganyikiwa. Hakujua nia ya hao watu. Angekuja hapa jf na kulalamikiwa kuvamiwa na kuibiwa gari na bastola yenye risasi usiku wa saa saba, weye ungekuwa wa kwanza kumdharau.
Naomba hili liwe funzo kwa wananchi wa TZ kuwa tuepuke kusherehekea kupita kiasi. Sherehe yako isiwe kero kwa wengine. Mjeshi alikuwa anapita kwenye barabara ya watu wote inayotakiwa ipite magari sio uwanja wa sherehe. Wala hakukuwa na ishara kuwa kuna sherehe huko mbele hivyo endesha taratibu.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.
Hao wenye sherehe zao walizidisha kipimo yaani walivuka mpaka. Waliposikia hiyo risasi ya kwanza ilitosha kuwa alert kuwa huyu mtu ni kichaa wakimbie lakini wakazidi kushangilia kwa kuivamia gari. Akaongeza mzigo..
Mimi si wakili lakini nawasilisha
Maelezo yako yanaonyesha wewe ni muuaji mwenyewe. Back to the topic. Soma mchango namba 50 kwenye hii thread!
 
Sipendi tabia ya wamiliki wa siraha ku shoot hovyohovyo.Siku ya tukio tunaambiwa kulikua na fujo kubwa eneo la tukio-kigogo fresh(rejea uzi wa nyuma kuhusu habari hii).Mabina wa Mwanza alipiga risasi kadhaa za kwanza hewani,kuna aliyeelewa,unakumbuka nini kilimtokea?Watanzania wengi[ hatuzijui siraha za moto,milio yake wala madhara yake.Sasa fikiria una 5mm Revolver ya 6 catriges. Umeshapiga hewani warning shots 2 bullets.Unaona bado kundi la watu linakuja na mawe na marungu na nondo,mbele na nyuma ya gari,usiku!. Umebakiwa na 4bullets,utafanyaje. QUOTE=trafficante;8281877]Mimi naona huyu mjenda alitakiwa kupuga risasi hewani wangekimbia tu sema ni kwamba yeye ni mwanajeshi na depo wanafundishwa kupiga kwanzia kiunoni kuja mpaka juu ya kichwa hawana option ya hewani hawa na kuhusu jeshi kumtetea itakua ni yupo kwenye kitengo muhimu sana ila ilo halifanyi yeye kutetewa haki itendeke[/QUOTE]
 
Ukitetea mijizi na mivibaka na wewe vile vile ni li mwizi tuu!
 
Maelezo yako yanaonyesha wewe ni muuaji mwenyewe. Back to the topic. Soma mchango namba 50 kwenye hii thread!

Sina haja ya kujibizana ila nakuambia, ni rahisi saana weye kumsema vibaya huyu mjeshi kwani hujawahi kujikuta kwenye kitu kama hicho. Tembea uone. Nielewe, nilisema simtetei mjeshi bali nasema Watz tubadilike, tuwafundishe hata watoto wetu kukimbia wakisikia ajali au mlipuko.
Si umeona pale ubungo juzi. Kitu kimeonekana kama bomu, watu wazima na akili zao, wanaona polisi wenyewe wanakichukua kwa uangalifu na mtetemo wao wako macho kodo. Lingekuwa bomu kweli leo tumgekuwa tunahesabu watu wasiopungua 20 wapoteza maisha kwa kulipukiwa na bomu.
Weye ungekuja hapa jf kuilaumu serekali.
Ninayesema nawe tulimzikaga jirani yetu; alipigwa risasi na majambazi, kisa, katoka nje kuangalia risasi zinavyolia kwa jirani huku hana hata kisu cha mkate. Tanzanians ni noooma.
Haiingi akilini, weye mzazi mwanao yuko nje saa saba usiku ati anashangilia mwaka. Hayo ndiyo malezi au bora malezi. Lawama umpe paka kwa kula kipanya wapi na wapi.
 
Well said pal!
Sina haja ya kujibizana ila nakuambia, ni rahisi saana weye kumsema vibaya huyu mjeshi kwani hujawahi kujikuta kwenye kitu kama hicho. Tembea uone. Nielewe, nilisema simtetei mjeshi bali nasema Watz tubadilike, tuwafundishe hata watoto wetu kukimbia wakisikia ajali au mlipuko.
Si umeona pale ubungo juzi. Kitu kimeonekana kama bomu, watu wazima na akili zao, wanaona polisi wenyewe wanakichukua kwa uangalifu na mtetemo wao wako macho kodo. Lingekuwa bomu kweli leo tumgekuwa tunahesabu watu wasiopungua 20 wapoteza maisha kwa kulipukiwa na bomu.
Weye ungekuja hapa jf kuilaumu serekali.
Ninayesema nawe tulimzikaga jirani yetu; alipigwa risasi na majambazi, kisa, katoka nje kuangalia risasi zinavyolia kwa jirani huku hana hata kisu cha mkate. Tanzanians ni noooma.
Haiingi akilini, weye mzazi mwanao yuko nje saa saba usiku ati anashangilia mwaka. Hayo ndiyo malezi au bora malezi. Lawama umpe paka kwa kula kipanya wapi na wapi.
 
Kichwa cha habari ulio andika kinaonesha wazi kuwa weye ndg una hasira sana. Nilidhani ni mjeshi mwingine ameamua kuua watoto wake tu halafu anatetewa.
To the point;
Hivi weye umewahi kuendesha gari mahali ambapo pana giza giza usiku halafu ukute labda mawe makubwa njiani? Unajisikiaje? Uwe unaendesha gari usiku, ghafula uvamiwe na watu pande zote mbili za gari na hata mbele na nyuma wanapigapiga gari yako, wengine wamebeba fimbo na vitu mbali mbali usivyoweza kuvitambua kwa sababu ya kelele zao. Utajisikiaje?
Simtetei huyo mjeshi. Lakini mimi nasema kama mimi, alichanganyikiwa. Hakujua nia ya hao watu. Angekuja hapa jf na kulalamikiwa kuvamiwa na kuibiwa gari na bastola yenye risasi usiku wa saa saba, weye ungekuwa wa kwanza kumdharau.
Naomba hili liwe funzo kwa wananchi wa TZ kuwa tuepuke kusherehekea kupita kiasi. Sherehe yako isiwe kero kwa wengine. Mjeshi alikuwa anapita kwenye barabara ya watu wote inayotakiwa ipite magari sio uwanja wa sherehe. Wala hakukuwa na ishara kuwa kuna sherehe huko mbele hivyo endesha taratibu.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.
Hao wenye sherehe zao walizidisha kipimo yaani walivuka mpaka. Waliposikia hiyo risasi ya kwanza ilitosha kuwa alert kuwa huyu mtu ni kichaa wakimbie lakini wakazidi kushangilia kwa kuivamia gari. Akaongeza mzigo..
Mimi si wakili lakini nawasilisha
Kwa hiyo uliua wa kwanza ukaona bado wanaendelea ukaongeza wa pili.?
 
Sina haja ya kujibizana ila nakuambia, ni rahisi saana weye kumsema vibaya huyu mjeshi kwani hujawahi kujikuta kwenye kitu kama hicho. Tembea uone. Nielewe, nilisema simtetei mjeshi bali nasema Watz tubadilike, tuwafundishe hata watoto wetu kukimbia wakisikia ajali au mlipuko.
Si umeona pale ubungo juzi. Kitu kimeonekana kama bomu, watu wazima na akili zao, wanaona polisi wenyewe wanakichukua kwa uangalifu na mtetemo wao wako macho kodo. Lingekuwa bomu kweli leo tumgekuwa tunahesabu watu wasiopungua 20 wapoteza maisha kwa kulipukiwa na bomu.
Weye ungekuja hapa jf kuilaumu serekali.
Ninayesema nawe tulimzikaga jirani yetu; alipigwa risasi na majambazi, kisa, katoka nje kuangalia risasi zinavyolia kwa jirani huku hana hata kisu cha mkate. Tanzanians ni noooma.
Haiingi akilini, weye mzazi mwanao yuko nje saa saba usiku ati anashangilia mwaka. Hayo ndiyo malezi au bora malezi. Lawama umpe paka kwa kula kipanya wapi na wapi.

Umejuaje sijawahi kujikuta kwenye mazingira kama hayo! Back to the topic... hicho unachohimiza kuhusu kubadilika hata mimi nakuunga mkono.... lakini si ''kuwafunza watanzania kwa kuwaua kwa risasi''. Itumike njia nyingine!
 
Wewe ndio unakurupuka. Habari hii iliripotiwa mapema zaidi humu jf na wadau wengi walipata balanced story. Sipendi kurudia hasa kwa vile wewe unaongozwa na emotions. Wewe mtu akitaka kukubaka utatulia amalize ili upate ushahidi? Lakini kitu ninachojiuliza, hawa watoto walikuwa,wanafanya nini barabarani saa saba usiku? Hivi wana wazazi hawa?

I like the way you have worded your thread...in deed we you strive to inform the public balanced stories
 
Back
Top Bottom