Eti dhambi ya Kikwete ni tabasam, uhuru wa kusema, kusikiliza wanyonge

Ukimya wa marafiki zako ni HATARI kuliko kelele za MAADUI wako.

Binafsi naamini kuwa Marafiki wa KIKWETE ni MAFISADI, nao wamekaa KIMYA na KIKWETE amekuwa akiwaunga MKONO na KUDHARAU walio wengi, WANANCHI WA KAWAIDA NA MASKINI.

Ndio maana anapoambiwa au kuulizwa juu ya MAFISADI UNAMUONA ANATABASAMU na KUCHEKA. JIBU LINALOFUATA, WOTE MNALIJUA!
 
Msukumo hasa ulionifanya kuandika Thread hii ni kuchoshwa na vyombo vya habari na baadhi ya wananchi kuchukua muda mwingi sana kulizungumzia tabasam la Kikwete kama upungufu mkubwa katika uongozi wake. Ni matumaini yangu kuwa katika siku zijazo hatutachanganya kati ya udhaifu (kama upo) na tabasam lake. Binafsi sipendi bosi wangu awe amenuna nyakati zote, ili nijue ndie Bosi mzuri. Kwa bahati mzuri Bosi wangu ni mcheshi na anatabasam zaidi ya Kikwete, lakini ni mchapaji kazi mzuri sana. Hii inanikumbusha wakati mgumu nilipokuwa sekondari, ambapo head master wa shule sikumuona kutabasam hata siku moja kwa kipindi cha miaka minne. Na kwa ukweli tulikuwa tukimuogopa kama simba. Hapana sipendi kukumbuka.
Ni haki yao kulalamikia yale wameona kiongozi wao amewaingiza mkenge.
Kumbuka vyombo vya habari na hao baadhi ya wananchi ndio tegemeo kubwa la JK kuingia madarakani.
 
Vyombo vya habari vilikuwa tegemeo kubwa la Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.

Mwaka 2010, tegemeo kubwa ni : kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Sasa hivi hahitaji sana vyombo vya habari kwa sababu wanyonge wameshaelewa kazi yake. Na silaha kubwa kati ya zote ni mzunguko wa pesa ulivyo rahisi na kumuwezesha kila mwenye ari ya kufanya kazi kujiwezesha. Wavivu ndio wanaokiona katika serikali hii ya Kikwete. Na nchi yeyote huendelea pale wananchi wake watapokuwa na juhudi ya kazi. Na kazi ya serikali ni kuwapa mianya hiyo na kuwawezesha.

Tamko hilo la mzunguko wa pesa utalisikia katika kila mkoa uendao, kitu ambacho chaonyesha jinsi watanzania wanavyoujua uchumi. Wale wanaodhaniaa watanzania ni wajinga, basi hawawaelewi watanzania. Watanzania walio wengi ni watu wavumilivu, makini, wasio na ndoto za ajabu na ni watu waishio katika uhalisia. WATANZANIA HAWAISHI KATIKA ULIMWENGU WA ABUNUASI. Wao ni wajuzi wa kutenganisha kati ya kampeni za uchaguzi na ukweli halisi kiutendaji. Na kwa mantiki hii ndio baadhi ya watanzania hukurupuka na kuwatukana watanzania kuwa ni wajinga.

Suala la kutotimiza ahadi zote wanazoahidi wagombea, si tatizo la Afrika au Tanzania tu, bali ulimwenguni kote hata huko Ulaya. Michezo hii ya kuigiza ya kukimbia nchi nzima na kucheza Zekamedi kwa kuahidi Paradise, wakati wote wanafahamu haiwezekani ndio ilizozifanya nchi kama China kukataa Demokrasia ya aina hiyo. Na Urusi ikavunja vunja upinzani na kuzingatia uchumi tu, huku ikipiga Gelesha kwa west kuwa wanavyama vingi.

Katika yote yatazungumzwa lakini tofauti kubwa ya utawala wa Mkapa na Kikwete ni MZUNGUKO WA PESA. Wakati wa Mkapa uchumi ulikuwa lakini mzunguko wa pesa ulikuwa mgumu sana ukilinganisha na sasa. Na njia pekee ya kuwasaidia wanyonge ni kuhakikisha kuwa kuna urahisi wa mzunguko wa pesa. Hii inamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kirahisi, mjenzi vile vile, muuza vitambaa naye atafaidika sawa na mshonaji, halikadhalika kwa kuli na muuza madafu. Na huu ndio mtaji wa Kikwete kuelekea uchaguzi 2010.
 
Wala sababu si hizo zilizotolewa na mtoa mada. Pengine ana uswahiba na jk. Mara nyingi nasikia eti watu wanamshauri rais vibaya. Mara ooh, watendaji wa jk ndo wana kasoro. Lowasa akiwa rais na mambo yakaenda kombo tutasema eti wanamshauri vibaya? Tazama, jk anapoumwa anasema mwenyewe hakusikiliza ushauri wa walio karibu nae. Mambo ya nchi yanapokwenda kombo wanasema rais hakushauriwa vizuri. Tatizo ndo liko hapo-unafiki wa kutokutaka kuonekana mbaya. Jk mwenyewe anafanya makosa kibao ya kiutendaji halafu lawama zinaenda kwa washauri. Tufike hatua tumwambie jk, mkuu, hapo umechemsha! Unaposema eti smile, mara uhuru, huko ni kukwepa hoja za msingi. Hakuna taifa huru kama USA na marais wachangamfu kama wa USA lakini fanya fujo uone. Ishu hapa ni mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mi4. Serikali, bunge, mahakama na media. Hapo pakikaa sawa, ruksa jk kutabasam na kutoa uhuru
 
Umegusa maeneo ya msingi sana pale ulipoandika: "Ishu hapa ni mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mi4. Serikali, bunge, mahakama na media. Hapo pakikaa sawa, ruksa jk kutabasam na kutoa"

Vizuri, nipe pause kidogo.... Hebu andika mapungufu yaliyopo leo hii katika mihimili hiyo 4.

Ninavyoelewa mimi katika awamu hii ya 4, Bunge liko huru sana, mpaka hata wabunge BUBU wa CCM nao wameanza kusema. Media ndio zimebinafsishwa na hakuna muandishi anayekwenda kumuuliza Kikwete au waziri wa Habari na utamaduni nini aandike na ninin asiandike. Serikali ndio hiyo kama unavyoiona imejipunguzia nguvu zake. Ndio maana choko choko za Bungeni zimewalazimisha mawaziri kujiuzulu.

Mahakama ndio tatizo la wazi kwa muono wangu.

Nakuomba utoe mapendekezo yako vile mgawanyo wamadaraka ungependelea uwepo katika mihimili hiyo 4.
 
kama kweli wapinzani wanajiandaa kutumia hizo sababu tatu kama ndio kampeni kuelekea uchaguzi 2010, basi waelewe kuwa ccm itashinda kirahisi kuliko chaguzi nyingine zote.

maandalizi yao hayako hivyo, sijui unataka kumwaminisha nani kwamba hivyo ndivyo wapinzani wanavyojiandaa?
 
Vyombo vya habari vilikuwa tegemeo kubwa la Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.

Mwaka 2010, tegemeo kubwa ni : kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Sasa hivi hahitaji sana vyombo vya habari kwa sababu wanyonge wameshaelewa kazi yake. Na silaha kubwa kati ya zote ni mzunguko wa pesa ulivyo rahisi na kumuwezesha kila mwenye ari ya kufanya kazi kujiwezesha. Wavivu ndio wanaokiona katika serikali hii ya Kikwete. Na nchi yeyote huendelea pale wananchi wake watapokuwa na juhudi ya kazi. Na kazi ya serikali ni kuwapa mianya hiyo na kuwawezesha.

Tamko hilo la mzunguko wa pesa utalisikia katika kila mkoa uendao, kitu ambacho chaonyesha jinsi watanzania wanavyoujua uchumi. Wale wanaodhaniaa watanzania ni wajinga, basi hawawaelewi watanzania. Watanzania walio wengi ni watu wavumilivu, makini, wasio na ndoto za ajabu na ni watu waishio katika uhalisia. WATANZANIA HAWAISHI KATIKA ULIMWENGU WA ABUNUASI. Wao ni wajuzi wa kutenganisha kati ya kampeni za uchaguzi na ukweli halisi kiutendaji. Na kwa mantiki hii ndio baadhi ya watanzania hukurupuka na kuwatukana watanzania kuwa ni wajinga.

Suala la kutotimiza ahadi zote wanazoahidi wagombea, si tatizo la Afrika au Tanzania tu, bali ulimwenguni kote hata huko Ulaya. Michezo hii ya kuigiza ya kukimbia nchi nzima na kucheza Zekamedi kwa kuahidi Paradise, wakati wote wanafahamu haiwezekani ndio ilizozifanya nchi kama China kukataa Demokrasia ya aina hiyo. Na Urusi ikavunja vunja upinzani na kuzingatia uchumi tu, huku ikipiga Gelesha kwa west kuwa wanavyama vingi.

Katika yote yatazungumzwa lakini tofauti kubwa ya utawala wa Mkapa na Kikwete ni MZUNGUKO WA PESA. Wakati wa Mkapa uchumi ulikuwa lakini mzunguko wa pesa ulikuwa mgumu sana ukilinganisha na sasa. Na njia pekee ya kuwasaidia wanyonge ni kuhakikisha kuwa kuna urahisi wa mzunguko wa pesa. Hii inamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kirahisi, mjenzi vile vile, muuza vitambaa naye atafaidika sawa na mshonaji, halikadhalika kwa kuli na muuza madafu. Na huu ndio mtaji wa Kikwete kuelekea uchaguzi 2010.

Wewe ni mpumbavvu hujui kitu chochote,nadhani unachojua ni kula na kushiba tu!!
Jambo la kwanza kwa Serikali yoyote makini ni kucontrol INFLATION tafuta kiwango cha inflation miaka 5 iliyopita ulinganishe na sasa!!!

Nenda shule ukasome!!!
 
Na silaha kubwa kati ya zote ni mzunguko wa pesa ulivyo rahisi na kumuwezesha kila mwenye ari ya kufanya kazi kujiwezesha. Wavivu ndio wanaokiona katika serikali hii ya Kikwete. Na nchi yeyote huendelea pale wananchi wake watapokuwa na juhudi ya kazi. Na kazi ya serikali ni kuwapa mianya hiyo na kuwawezesha.

Mbona unatoa hoja chakavu kiasi hiki? wapo wepi hao unaowasemea wenye ari? Labda kundi lile lile, kwani nasikia sasa ndio wanaotaka kuuwana kukimbilia tenda ya kuingiza mashine za kilimo, katika hicho mnachoita "kilimo kwanza".

Mijitu mingine, hovyo kabisa! Sijui mnaipendea Tanzania mema yepi!
 
Wewe ni mpumbavvu hujui kitu chochote,nadhani unachojua ni kula na kushiba tu!!
Jambo la kwanza kwa Serikali yoyote makini ni kucontrol INFLATION tafuta kiwango cha inflation miaka 5 iliyopita ulinganishe na sasa!!!

Nenda shule ukasome!!!
Kati yake na yeye ambaye hajasoma nafikiri wewe ndio unatakiwa kuanza chekechea duh aibu!!!
ehee endelea akisha-control inflation.... kinachofuata...na una-control inflation kwa kufanyeje? fafanua...
 
Umegusa maeneo ya msingi sana pale ulipoandika: "Ishu hapa ni mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mi4. Serikali, bunge, mahakama na media. Hapo pakikaa sawa, ruksa jk kutabasam na kutoa"

Vizuri, nipe pause kidogo.... Hebu andika mapungufu yaliyopo leo hii katika mihimili hiyo 4.

Ninavyoelewa mimi katika awamu hii ya 4, Bunge liko huru sana, mpaka hata wabunge BUBU wa CCM nao wameanza kusema. Media ndio zimebinafsishwa na hakuna muandishi anayekwenda kumuuliza Kikwete au waziri wa Habari na utamaduni nini aandike na ninin asiandike. Serikali ndio hiyo kama unavyoiona imejipunguzia nguvu zake. Ndio maana choko choko za Bungeni zimewalazimisha mawaziri kujiuzulu.

Mahakama ndio tatizo la wazi kwa muono wangu.

Nakuomba utoe mapendekezo yako vile mgawanyo wamadaraka ungependelea uwepo katika mihimili hiyo 4.

kiufupi ni kwamba, bunge linapotaka kujiendesha wabunge wa chama tawala wanaitwa kando na kupewa opium of the mind. Spika nae anawindwa. Wabunge wapinga ufisadi wanaandamwa. Kwenye media ndo kama hivyo. Ukizungumza kidogo kuhusu ufisadi unaandamwa na serikali. Vyombo vyako vitaandamwa na biashara zako kusulubiwa. Lazima useme ndio mzee! Serikalini kuna haja ya kuzungumzia? Mara ngapi imeingilia bunge na mahakama? Mahakama je. Inaonyesha udhaifu kiasi gani. Kwanza hazina uwezo wa kujiendesha. Kesi zinachukua mda hadi zinachacha. Ni watoto wa wakubwa wangapi wamefanya makosa lkn wako juu ya sheria? Ni vigogo wangapi wako juu ya sheria? Kifupi hao akina mramba ni zengwe la next election. Liyumba ni chuki binafsi. Kwani alianza kula jana? Kesi za rada, richmond, epa, zombe, n.k ziko wapi? Hayo ni kwa muhtasari tu. Mengine naomba uongezee
 
Naona umegeneralize sana. Nilitegemea ungetoa point moja moja na mifano halisi. Kwa mfano unapozungumzia EPA, si mambo bado yanaendelea. Kesi ziko mahakamani, wengine wamekimbia nchi na wengine wamerudisha pesa. Si hatua kamili lakini ni mwanzo mzuri kuelewa kuwa hakuna wateule.

Liyumba wasema chuki binafsi, na Mramba wasema ni geresha sasa serikali ifanye nini ili uridhike. Au ndio wewe ni uliyekwishaweka NO kwa serikali hii.

Chama kimoja huwa na lengo moja, si Tanzania tu bali kila nchi. Unaposema wabunge wa wanaitwa, hapo bado sijakuelewa. Ninavyoelewa mimi iwe ni maDemocrat au Republican (Marekani) kila chama wanakuwa na lengo lao. Na ni lazima wabunge wake wakusanywe na kuelezwa msimamo wao ili watapopiga kura ndani ya Bunge iwe rahisi kupitisha ajenda yao. Hivyo ndivyo vyama vya siasa vinavyofanya kazi.

Tatizo letu hatuna wabunge wengi kwa wapimzani. Mbona akina Slaa na Zitto wanasema na bado wapo. Tungelikuwa na wabunge wengi wa upinzani, tungefaidika na sauti zao. Ni bora kuwa na wabunge wengi wa upinzani kuliko kuwa na Rais toka upinzani na tukiwa na idadi ileile ya wabunge wa CCM.

Tatizo jingine wabunge wetu (CCM) HAWAKWENDA KUTETEA HOJA ZA WANANCHI ila ni mishahara na marupurupu yao tu. Kwani hata wakisema kwani serikali itawafanya nini. Ni lazima wawe watu wa principles, wakielewa kuwa wao ndio wanaowakilisha wananchi. Ububu eti kwa kuogopa kukatwa majina yao na CCM NI UPUNGUFU WA AKILI. Nafasi ya kusema wanayo, inachobidi ni kuitumia tu, kwani CCM si wao.
 
Wewe ni mpumbavvu hujui kitu chochote,nadhani unachojua ni kula na kushiba tu!!
Jambo la kwanza kwa Serikali yoyote makini ni kucontrol INFLATION tafuta kiwango cha inflation miaka 5 iliyopita ulinganishe na sasa!!!

Nenda shule ukasome!!!
Haya mwenzetu mwerevu tupe mwanga. Ni tabu kweli maana nyie werevu hamkupewa nchi, wapumbavu wakapewa nchi na ndio wanaharibu.

Lakini mimi najiuliza kwa nini msitumie werevu wenu kuingia madarakani? Hivi hapa si ndio mahala pa kuonyesha werevu wenu.

Sitozungumzia hayo ya Inflation, badala yake nitawangoja mwaka 2010 ili mje kuchukua Nchi na mtukomboe toka katika ujimga wa kiza kizito.
 
Zawadi Ngoda said:
Tatizo letu hatuna wabunge wengi kwa wapimzani. Mbona akina Slaa na Zitto wanasema na bado wapo. Tungelikuwa na wabunge wengi wa upinzani, tungefaidika na sauti zao. Ni bora kuwa na wabunge wengi wa upinzani kuliko kuwa na Rais toka upinzani na tukiwa na idadi ileile ya wabunge wa CCM.

Zawadi Ngoda,

..naomba ufafanuzi zaidi kuhusu kipengele nilichokunukuu hapo juu.

..naomba pia nikumbushe kwamba Katiba inaelekeza kwamba serikali itaundwa na chama chenye wabunge wengi wa kuchaguliwa.

..pia Katiba inaelekeza kwamba Waziri Mkuu atachaguliwa miongoni wa wabunge kutoka chama chenye majority bungeni.

..je, katika hoja yako unapendekeza kwamba Tanzania tutafaidika zaidi ikiwa Raisi atatoka CCM, na Waziri Mkuu atatoka chama kingine ambacho pia kitaunda baraza la mawaziri/serikali?
 
Vyombo vya habari vilikuwa tegemeo kubwa la Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.

Mwaka 2010, tegemeo kubwa ni : kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Sasa hivi hahitaji sana vyombo vya habari kwa sababu wanyonge wameshaelewa kazi yake. Na silaha kubwa kati ya zote ni mzunguko wa pesa ulivyo rahisi na kumuwezesha kila mwenye ari ya kufanya kazi kujiwezesha. Wavivu ndio wanaokiona katika serikali hii ya Kikwete. Na nchi yeyote huendelea pale wananchi wake watapokuwa na juhudi ya kazi. Na kazi ya serikali ni kuwapa mianya hiyo na kuwawezesha.

Tamko hilo la mzunguko wa pesa utalisikia katika kila mkoa uendao, kitu ambacho chaonyesha jinsi watanzania wanavyoujua uchumi. Wale wanaodhaniaa watanzania ni wajinga, basi hawawaelewi watanzania. Watanzania walio wengi ni watu wavumilivu, makini, wasio na ndoto za ajabu na ni watu waishio katika uhalisia. WATANZANIA HAWAISHI KATIKA ULIMWENGU WA ABUNUASI. Wao ni wajuzi wa kutenganisha kati ya kampeni za uchaguzi na ukweli halisi kiutendaji. Na kwa mantiki hii ndio baadhi ya watanzania hukurupuka na kuwatukana watanzania kuwa ni wajinga.

Suala la kutotimiza ahadi zote wanazoahidi wagombea, si tatizo la Afrika au Tanzania tu, bali ulimwenguni kote hata huko Ulaya. Michezo hii ya kuigiza ya kukimbia nchi nzima na kucheza Zekamedi kwa kuahidi Paradise, wakati wote wanafahamu haiwezekani ndio ilizozifanya nchi kama China kukataa Demokrasia ya aina hiyo. Na Urusi ikavunja vunja upinzani na kuzingatia uchumi tu, huku ikipiga Gelesha kwa west kuwa wanavyama vingi.

Katika yote yatazungumzwa lakini tofauti kubwa ya utawala wa Mkapa na Kikwete ni MZUNGUKO WA PESA. Wakati wa Mkapa uchumi ulikuwa lakini mzunguko wa pesa ulikuwa mgumu sana ukilinganisha na sasa. Na njia pekee ya kuwasaidia wanyonge ni kuhakikisha kuwa kuna urahisi wa mzunguko wa pesa. Hii inamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kirahisi, mjenzi vile vile, muuza vitambaa naye atafaidika sawa na mshonaji, halikadhalika kwa kuli na muuza madafu. Na huu ndio mtaji wa Kikwete kuelekea uchaguzi 2010.

Ni kweli kwamba Watanzania Hawaishi katika Ulimwengu wa Abunuasi ila Zawadi Ngoda sijui kwa nini anang'ang'ania Huo Ulimwengu
 
Kati yake na yeye ambaye hajasoma nafikiri wewe ndio unatakiwa kuanza chekechea duh aibu!!!
ehee endelea akisha-control inflation.... kinachofuata...na una-control inflation kwa kufanyeje? fafanua...

Wee nadhani ndiyo utakuwa Ngedere dume, sasa bado Ngedere kinda safu ya Mangedere wa JF ikamilike...
 
Vyombo vya habari vilikuwa tegemeo kubwa la Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.

Mwaka 2010, tegemeo kubwa ni : kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Sasa hivi hahitaji sana vyombo vya habari kwa sababu wanyonge wameshaelewa kazi yake. Na silaha kubwa kati ya zote ni mzunguko wa pesa ulivyo rahisi na kumuwezesha kila mwenye ari ya kufanya kazi kujiwezesha. Wavivu ndio wanaokiona katika serikali hii ya Kikwete. Na nchi yeyote huendelea pale wananchi wake watapokuwa na juhudi ya kazi. Na kazi ya serikali ni kuwapa mianya hiyo na kuwawezesha.

Tamko hilo la mzunguko wa pesa utalisikia katika kila mkoa uendao, kitu ambacho chaonyesha jinsi watanzania wanavyoujua uchumi. Wale wanaodhaniaa watanzania ni wajinga, basi hawawaelewi watanzania. Watanzania walio wengi ni watu wavumilivu, makini, wasio na ndoto za ajabu na ni watu waishio katika uhalisia. WATANZANIA HAWAISHI KATIKA ULIMWENGU WA ABUNUASI. Wao ni wajuzi wa kutenganisha kati ya kampeni za uchaguzi na ukweli halisi kiutendaji. Na kwa mantiki hii ndio baadhi ya watanzania hukurupuka na kuwatukana watanzania kuwa ni wajinga.

Suala la kutotimiza ahadi zote wanazoahidi wagombea, si tatizo la Afrika au Tanzania tu, bali ulimwenguni kote hata huko Ulaya. Michezo hii ya kuigiza ya kukimbia nchi nzima na kucheza Zekamedi kwa kuahidi Paradise, wakati wote wanafahamu haiwezekani ndio ilizozifanya nchi kama China kukataa Demokrasia ya aina hiyo. Na Urusi ikavunja vunja upinzani na kuzingatia uchumi tu, huku ikipiga Gelesha kwa west kuwa wanavyama vingi.

Katika yote yatazungumzwa lakini tofauti kubwa ya utawala wa Mkapa na Kikwete ni MZUNGUKO WA PESA. Wakati wa Mkapa uchumi ulikuwa lakini mzunguko wa pesa ulikuwa mgumu sana ukilinganisha na sasa. Na njia pekee ya kuwasaidia wanyonge ni kuhakikisha kuwa kuna urahisi wa mzunguko wa pesa. Hii inamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kirahisi, mjenzi vile vile, muuza vitambaa naye atafaidika sawa na mshonaji, halikadhalika kwa kuli na muuza madafu. Na huu ndio mtaji wa Kikwete kuelekea uchaguzi 2010.
Hapa ndipo umeniacha hoi!
"Katika yote yatazungumzwa lakini tofauti kubwa ya utawala wa Mkapa na Kikwete ni MZUNGUKO WA PESA. Wakati wa Mkapa uchumi ulikuwa lakini mzunguko wa pesa ulikuwa mgumu sana ukilinganisha na sasa. Na njia pekee ya kuwasaidia wanyonge ni kuhakikisha kuwa kuna urahisi wa mzunguko wa pesa. Hii inamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kirahisi, mjenzi vile vile, muuza vitambaa naye atafaidika sawa na mshonaji, halikadhalika kwa kuli na muuza madafu. Na huu ndio mtaji wa Kikwete kuelekea uchaguzi 2010".
Cheap politicking; higher growth with low liquidity; lower growth with higher liquidity; au ndiyo mmeshaanza ku-print pesa!
 
Nilifikiri kwenye free economy factor zote zinaenda automatically. Wewe mwenzetu unasema ati uchumi haukui lakini fedha nyingi lakini wakati uchumi ulikuwa unakua pesa zilikuwa hazipo. Lakini si goods zinavyo- exchange ndiyo tunaona activities za biashara zinakua. Sasa kama uchumi haukui hizo pesa zinatoka wapi; kama siyo mmeanza kuprint? Zawadi hebu tuambie usiwe unaleta hiyo kubwabwaja bila facts.
 
Naona umegeneralize sana. Nilitegemea ungetoa point moja moja na mifano halisi. Kwa mfano unapozungumzia EPA, si mambo bado yanaendelea. Kesi ziko mahakamani, wengine wamekimbia nchi na wengine wamerudisha pesa. Si hatua kamili lakini ni mwanzo mzuri kuelewa kuwa hakuna wateule.

Liyumba wasema chuki binafsi, na Mramba wasema ni geresha sasa serikali ifanye nini ili uridhike. Au ndio wewe ni uliyekwishaweka NO kwa serikali hii.

Chama kimoja huwa na lengo moja, si Tanzania tu bali kila nchi. Unaposema wabunge wa wanaitwa, hapo bado sijakuelewa. Ninavyoelewa mimi iwe ni maDemocrat au Republican (Marekani) kila chama wanakuwa na lengo lao. Na ni lazima wabunge wake wakusanywe na kuelezwa msimamo wao ili watapopiga kura ndani ya Bunge iwe rahisi kupitisha ajenda yao. Hivyo ndivyo vyama vya siasa vinavyofanya kazi.

Tatizo letu hatuna wabunge wengi kwa wapimzani. Mbona akina Slaa na Zitto wanasema na bado wapo. Tungelikuwa na wabunge wengi wa upinzani, tungefaidika na sauti zao. Ni bora kuwa na wabunge wengi wa upinzani kuliko kuwa na Rais toka upinzani na tukiwa na idadi ileile ya wabunge wa CCM.

Tatizo jingine wabunge wetu (CCM) HAWAKWENDA KUTETEA HOJA ZA WANANCHI ila ni mishahara na marupurupu yao tu. Kwani hata wakisema kwani serikali itawafanya nini. Ni lazima wawe watu wa principles, wakielewa kuwa wao ndio wanaowakilisha wananchi. Ububu eti kwa kuogopa kukatwa majina yao na CCM NI UPUNGUFU WA AKILI. Nafasi ya kusema wanayo, inachobidi ni kuitumia tu, kwani CCM si wao.

nadhani mtu ambaye anaichukia hii serikali ni prince bagenda aliyemtungia jakaya kitabu. Kiufupi siitamani hii serikali. Imeruhusu uhuru ila imeshindwa kutumia fursa ya kuruhusu uhuru. Sabodo aliwahi kusema kuwa ile kauli mbiu ya Ari Nguvu na Kasi mpya ni ANGUKA kama ilivyo sasa. Tunahitaji mzalendo. Mzalendo ana sifa kuu mbili. Zaidi ya hapo ni chumvi tu. Dhamira iliyo hai na uwezo wa kujibainisha (empathy). Hizo sifa viongozi wetu hawana. Tuombe na Mungu ili tupate chaguo sahihi toka kwake
 
Back
Top Bottom