Eti dhambi ya Kikwete ni tabasam, uhuru wa kusema, kusikiliza wanyonge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti dhambi ya Kikwete ni tabasam, uhuru wa kusema, kusikiliza wanyonge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Oct 10, 2009.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Huwezi kuamini kuwa baada ya Watazania kushindwa kutafuta makosa ya kuilaumu serikali ya Kikwete, wamekimbilia sababu zisizoshikika wala kukubalika. Tabasam lake ndio imekuwa nongwa na silaha ya wsiompenda kuelekea uchaguzi wa 2010. Aidha dhambi zake nyingine ni pamoja na kusaidia wanyonge na kuruhusu uhuru wa kusema kwa kila Mtanzania.

  Tony Blair na Bill Clinton ndio viongozi wanaoongoza kwa kuwa na tabasam la kila wakati. Wakati huo huo wao ndio viongozi waliofanikisha sana katika kukuza uchumi wa nchi zao. Na hata baada ya kutoka madarakani bado wanasufa kem kem. Joseph Starlin na Mabuto Seseseko ni viongozi waliosifika sana kwa kuwa na tabasam la nadra sana, na walipotoka madarakani majina yao yalikuwa mwiba kwa walimwengu. Sasa vipi tumhukumu Raisi kutokana na tabasam lake? Sioni mantiki katika hili!

  Sababu ya pili ninayoisikia sana ni ile ya kudhani kuwa serikali ya Kikwete ni dhaifu. Ukifanya uchunguzi, utakuta kuwa lawama hizo zinatokana na serikali kuwa na utamaduni wa kusikiliza wadau wote na hasa wanyonge. Aidha kutoifanya Tanzania kuwa Polisi State na kuwaswaga wanyonge ni dhambi waionayo wasiompenda. Wengi walizoea Tanzania kuwa Polis state kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa, na kudhani kuwa hiyo ndio tafsiri ya serikali strong.

  Kutoona mabomu yakishuka Pemba na Mwenbechai, haikuwafurahisha wengi. Ninashindwa kufahamu ni vipi binaadam akafurahia utawala wa mabavu kama ule wa chama kimoja, tulioupiga vita kwa miaka mingi? Tusiwe Egoist kwa dhana kwamba, la msingi ni kutimiziwa mahitaji yangu tu. Hii ni dhana potovu, na haitatufikisha mbali. Ni muhimu kwa watanzania wote kusikilizwa, hoja zao, matatizo yao na ushauri wao. Vinginevyo ni kukubali kuwa Demokrasia imeshindwa au hatuitaki, na pengine turudi kwenye Auktocrat au udikteta.

  Suala la tatu la udhaifu wake, eti ni uhuru wa kujieleza. Watanzania hatukuwahi kupata nafasi kama hii kwa kipindi cha miaka 40. Leo hii baada ya kupata nafasi hiyo, tunashindwa kuitumia vizuri, si watu binafsi hata vyombo vya habari. Hata kuna baadhi ya watu wamediriki kusema kuwa, kwanini Rais hajalifungia gazeti hili au lile. Hii yote ni kuonyesha uchanga wa demokrasia yetu na jinsi tunavyoshindwa kutumia mianya iliyopo kwa ajili ya maendeleo. Hivi kweli ni dhambi ya Kikwete kutoa uhuru wa kujieleza kwa mimi na wewe? Hatukumbuki jinsi Mkapa aalivyopata taabu na vyombo vya habari. Kwanini tusimsifu na kufurahia hilo?

  Kama kweli wapinzani wanajiandaa kutumia hizo sababu tatu kama ndio kampeni kuelekea uchaguzi 2010, basi waelewe kuwa CCM itashinda kirahisi kuliko chaguzi nyingine zote. Wakati ni huu kwa wapinzani na wapiga debe wao kubadili stesheni na kuja na sababu madhubuti zaidi, ambazo wananchi watawaelewa. Tunapenda CCM iondoke madarakani, lakini lazima tujue ni chama gani bora kitaingia madarakani. Tunahitaji chama bora, na si bora chama. Jipangeni vizuri ili msiumbuke, wakati ni huu.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kuna ukweli wowote katika hiyo paragraph ya mwisho.Ni chama gani kinataka kupiga domo na porojo hizo badala ya kuwakilisha sera nzito????

  Kama ulivyosema kuhusu Blair na Clinton,then kama tabasamu zao na uhuru wa kujieleza unaambatana na mageuzi ya kiuchumi then well and good!

  Sasa kinachowakera Watanzania ni pale Rais anapoulizwa jambo la msingi na kuanza kuchecheka kama ameona bia za bure badala ya kutoa hoja zenye msingi.

  Nadhani hata hao akina Blair walikuwa hawecheki kipuuzi kama huyu wa kwetu.

  Rais anapo toa hoja kama kula uliwe hasa kwenye masuala mazito ya kifisadi na rushwa huu ni mzaha ambao haukubaliki kabisa.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Jk mimi binafsi simchukii kabisa. I think he is a nice guy na ana personalty ya kuvutia....

  but...

  Tukija kwenye swali la je yeye ni kiongozi mzuri.... hapo ndipo ninapokataaa.....i think urais kwake ni mzigo mzito saana.

  Angekuwa raisi mzuri kama angekuwa raisi asiye na madaraka kama India.

  Tunaaosema sio kiongozi mzuri hatusemi kwa sababu za binafsi

  its not personal.
   
 4. M

  Merchant Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zawadi,
  You' ll never convince me on your ideas as they have motives. Wewe katika hizo hoja zako umejiingiza kuwa sana kama mtetezi wa Rais Kikwete, halafu umewahi kuongelea jinsi Dini fulani ilivyo-onewa na wale uliowaosema. Infact, you acted on the divide and rule of this nation. You are not a great mind. You could have observed first the root cause of the whole situation.

  Kwa taarifa yako tu elewa kuwa Dikteta Mkapa au Dikteta Nyerere (Kama unavyotaka wewe watambulike hivyo) waliishi kwa wakati wao. The world is evolving everday every month and every year. So the era of Nyerere cannot be compared by any means from your liberals whom you are trying to tell us. In your mind and your thinking from your inherited ideals Mr. Mwinyi and Kikwete are the most Democratic presidents and you will be bend to think so. (Note that I am commenting this from the reference of your past postings). Kwa hiyo, being any comments from you as a divisive factor, who has been affected by the virus of religion racism, I cannot waste my time reading your crap.

  Lastly, please if for sure you are the one I know, fikisha hizi salamu kwa Abuu, halafu usiwasahau Salehe na Abdalarhmani!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Usitake kusingizia watu wengine. Wapinzani uliwasikia wapi wakijenga hoja hizo? Hayo ni mawazo yako na ni afadhali utafiute jinsi ya kuyatetea na si kusema ni hoja za watu wengine. Itakapofika wakati wa wapinzani kujenga hoja zao watazitoa hadharani na tutazisikia sote.... Au unamaanisha wapinzani gani?
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Nadhani unachanganya vitu viwili kwa wakati mmoja, udhaifu wa Kikwete na kushinda uchaguzi.

  Sijajua msukumo hasa uliokusukuma kuandika article kama hii, anyway watu wa aina yako ndiyo wengi tulionao nchi hii.

  Kumbuka Hitler pamoja na ubaya wake na 20 attempts za kuuawa, bado baadhi ya watu walimpenda!

  Ikifikia baadhi ya individual waliotawaliwa na:

  Ujinga

  Huwa hawajui kiongozi anatakiwa afanye nini, aseme nini, aaamue nini, asaidie nini, kwao kiongozi ni mtu asiye na effect yeyote katika maisha yao. Hii tunaiona kupitia, watu wasivyokuwa serious na kuchagua viongozi, kutoka tangu primary school. balozi wa nyumba kumi kumi n.k,hatujui nini maana ya kiongozi. Ukimkuta kiongozi naye hajui wajibu wake, basi mtawala na mtawaliwa hata siku moja hawatakuwa katika conflict maana wote hawajui!

  Ndiyo wenye tuhuma za ufisadi wanapokelewa kwa mazuri mekundu na ngoma, ndiyo Wezi wa mali zetu kamwe hawaonekani wezi, isipokuwa mashujaa.

  Jamii hii ya wajinga wanaweza na wataendelea kuchagua CCM, kwani hawajui. Mambo yakiaharibika, basi ni wakati kuna NJAA, MALI ASILI HAMNA, KILA KITU HAKIENDI basi ndio wanaamka , mara nyingi huwa too late, na ndio upelekea vita. Watu hawapigani hata siku moja wakiwa na raha ndugu

  Umimi/ubinafsi/kutojali wengine

  Hii inaonekana sana katika jamii ya walionacho/waliosoma/waliofanikiwa.

  Ukiweza kupata mshahara wa laki tano, umepanga sinza, una gari la mkopo wa CRDB, hukumbuki ndugu zako, kule Bukoba , kigoma na mtwara wanaishi vipi. Watu ambao dawa za malaria ni ndoto achilia mbali huduma za kijamii.

  Jamii hii ya walionacho, ndio hutawakuta katika maandamano, wakiona unaongelea siasa wanakuona hamnazo, ndiyo utawakuta maeneo ya UDSM na vyuo vyote vikuu. Wanashida gani?? chakula kipo, TV, ipo, hospitali ana insurance, what ever he needs he will get it!

  Ndiyo jamii hii inashindwa kupata picha ya hali halisi ya mtanzania, nchi iliyo katika kumi bora ya nchi maskini duniani, lakini ni moja ya nchi inayoongoza kwa mali asili duniani!

  Hii jamii kawaida hupeleka watoto wao international school, achilia mbali nje ya nchi, si zipo?

  Geographical reasons

  Nchi nyingi za kitropic ambazo zina hali nzuri ya hewa kwa mwaka mzima,chakula, watu siku zote huangukia katika group la kwanza(ujinga).

  Msukumo huu wa hali ya kijiografia ndiyo unapeleka vyama kama CCM vinaringia hii hali, watu hawana shida ati, shida kwao ni haki yao!

  Kijijini kwetu mtu anaweza akawa na sh. 200 kwa mwezi mzima akaishi, vyakula viko mashambani au vimetunzwa, akishiba, anawaza pombe na ngoma za kienyeji, miaka inaenda. Wakitokea akina Zawadi kwenda kuwapa kanga na kofia basi umemaliza kila kitu.

  Hizi hali chache hapo juu haziifanyi CCM kuwa superior hapana, zinawaweka katika wakati mgumu wa kuja kuhukumiwa, KWENYE MITI HAKUNA WAJENZI??

  Kuwa CCM inatakiwa itumie hali nzuri ya kisiasa kwa mendeleo

  kuwa inatakiwa ilinde mali asili zetu

  kuwa inatakiwa iwasomeshe wananchi wake wawe competent globaly

  Kulinda umoja wa kitaifa kutokuwa na matabaka ya maskini na matajiri

  Kupromote uanzishwaji wa viwanda vya nyumbani na wawekezaji wa hapa nyumbani, sio mpaka chungwa litoke afrika kusini wakati yanaoza Tanga

  Kuwa i-initiate serikali ya umoja wa kitaifa, itakayounganisha watu wote na vyama vya kisiasa

  Kuwa kubadilisha mifumo ya elimu na uongozi tuliyonayo sasa

  Kuwa, kuondokana na bajeti tegemezi

  Kupromote kilimo cha kisasa cha umwagiliaji maji

  Kuwa wale wooote waliohusika na kula mali za umma wachukuliwe hatua, kwanza waturudishie mali, pili waende jela( kwa miaka minne hatujaona hilo)

  Obama anatabasamu, Nyerere alikuwa anatabasamu na kuchekesha, watu wangemuita comedian , lakini wapi.

  Uhuru wa kujieleza ni silaha nyingine kali sana anayotumia JK, nimekueleza swala la ujinga, Kuwa watanzania huridhika kirahisi na kitu fulani

  Niambie nini kimefanyika baada ya uhuru wa kujieleza, ukijieleza basi ndiyo umemaliza? CCM wanajua watawapata watu kama nyie kirahisi. ALAMA ZA NYAKATI zinaonyesha there is no way CCM ingeweza kuzuia hili swala, katika dunia ya leo, kama hauamini kamuulize Mugabe, rais wa Iran au Bush! .Au muulize Dr. Slaa ni akina nani wanampa nyaraka za SIRI, some people are tired!

  2+2=4, lakini demorasia inaweza kuamua 2+2=6, na ikapitishwa, the fact that CCM was elected does not justify that CCM is a good party, there is high chance kuwa waliopiga kura wako kwenye makundi hayo hapo juu , na hasa la ujinga na katika hilo kundi na wewe humo!

  Haiwezekani umaskini wa nchi hii ukamkwepesha JK, he was ,since then the leader in many positions, even sensitive ones, he is the person that he have done all these dirty deals and contracts that country is now suffering from it.

  Zawadi, ebu niambie JK alifanya nini ikapeleka akachaguliwa kuwa rais, alipitia wizara ya nishati, mambo ye nje, wizara zote hizo hakufanya any remarkable work. CCM kumteua JK si ni sababu ni zile zile za ujinga na upumbavu. UNategema nini huyu mtu ukimpa urais wakati alishindwa uwaziri??. Kama alikuwa anashindwa kazi kwa sababu ya superiors wake , kwa nini hakujiuzulu??

  Unapokuja wewe na kumsifia JK wakati JK hakutakiwa hata kuwa rais; kama tunaamua kuchagua rais based on their previous good performance. tukueleweje? yaani ukae kwenye kundi gani?? ujinga, umimi ,au upumbavu

  Ok, sikuweki katika kundi lolote, piga picha una uwezo japo wa kusurf kwenye internet na kutoa maoni kama hayo. I am pretty sure your family is not from such elite groups kiasi cha wewe kumsifia JK. Naamini, tena nathibitishiwa kuwa hata unachoeleza hapa huna uwezo wa kuongea mbele ya wasioijua hata internet pale kariakoo, achilia mbali partner wako mwenyewe kama hatoki katika familia ya mifisadi! Hutaweza kuongea hata mbele ya watoto wa primary, waliomzomea Makamba fisadi!

  Nathibitishiwa kuwa JF haijakusaidia kukubadili mawazo, acha nikusaidie kidogo tena i, cha kufanya jikaze tu wakati unapigwa msasa

  Ushapata picha za wanafunzi wanaokaa chini, akina mama wanaokosa huduma nzuri za uzazi?

  ushapata picha ya vijana wanaolikimbia taifa lao, kwa kukosa kazi, na kwenda nje kufanya kazi kwenye kampuni mabayo malighafi wanatoa Tanzania?

  Je umepiga picha miaka 50 ijayo kuwa nchi takuwa vipande viwili, maskini sana na matajiri sana>?

  n.k,


  Miaka minnne hii, JK alitakiwa kufuta makosa ya CCM miaka 40 iliyopita, alitakiwa asimame katika Tanzania mpya na ile kaluli mbiu yake!

  JK hajafanya chochote zaidi Taifa linaangamia, Zawadi kama mawaziri tu walio katika serikali yake wanamponda wewe unamsifia??

  Najua ni maoni, na una uhuru, lakini maoni mengine ni insult, mabayo kamwe haitakuacha upite hivi hivi.

  Kwa hiyo ondoka kwenye hilo kundi la wajinga, au wabinafsi, achana kabisa na kundi la mafisadi. Ondokana kabisa na wingu lolote la kujipendekeza au kutafuta vyeo.

  Hakuna urafiki wa wezi.

  The reason that JK can do nothing nchi hii , zaidi ya kufungua shule zisizo na walimu ni kuwa alichaguliwa kifisadi, yeye ni baba na wajomba wa mafisadi, anaishi kifisadi, marafiki wake ni mafisadi, wanomuunga mkono ni aidha mafisadi , wajinga au walikuwa obsessed naye, sijasema umekua obsessed na JK otherwise watu wangefikira vingine, sijasema wewe ni fisadi , sina uthibitisho huo, wala sikufahamu

  Hila ninaamini wewe ni mjinga(sio tusi) uwezo wako mdogo sana wa kusoma japo internet web pages na post za akina waberoya, unaweza kujua marais wa wenzetu wanafanya nini, nini wajibu wa viongozi, itakusaidia sana

  Kumbuka sijamlaumu JK hapa, nalaumu wale waliomchagua bila criteria zozote, ambao nimewaita wajinga. Kama wewe hujaweza kutambua kuwa JK alikosewa kuchaguliwa , hujajiweka tena katika kundi la wajinga, bali ni kundi la mjinga wa mwisho sijaua kiswahili kizuri nikuiteje anyway let just say ni mjinga wa mwisho kabisa

  ujinga ni ignorance tungalie dictionary inasemaje


  Ignorant Meaning and Definition


  1. (a.) Unknown; undiscovered.
  2. (a.) Destitute of knowledge; uninstructed or uninformed; untaught; unenlightened.
  3. (n.) A person untaught or uninformed; one unlettered or unskilled; an ignoramous.
  4. (a.) Resulting from ignorance; foolish; silly.
  5. (a.) Unacquainted with; unconscious or unaware; -- used with of.
  Ikiwa ninachoamini hiki kwako si sahihi basi I am ready to be named equally the same.
   
 7. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Napenda ningekuelewa unachokizungumzia, kwani point zako haziko wazi (direct). Kwa vile umeandika: "Who has been affected by the virus of religion racism, I cannot waste my time reading your crap." Basi nitahisi tu kuwa point yako yote imejikita kwenye Udini.

  Hebu niweke wazi kabisa kuwa, thread hii niliyoiandika haina uhusiano wowote ule na Udini. Ni vitu viwili vilivyojitokeza katika maada hii: 1. Personality 2. Utendaji. Ningefurahi sana kama hoja zako zingezingatia mambo hayo mawili makuu.

  Hata hivyo nakushukuru kwa kushiriki katika kutoa hoja zako.
   
 8. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Hii ya tabasamu ngekewa la Kikwete (matamshi yako) ulishalitaja siku za nyuma, lakini wakati ule ilikuwa kwenye context ya kumsifia tofauti na leo.

  Nadhani tatizo siyo Kikwete kutabasamu mno, tatizo ni why is Zawadi Ngoda so freakingly obsessed with Kikwete's smile? I bet you must be nursing some kind of romantic crush on this dude! All in all what you've posted today takes everything you've ever said before to a whole new level of stupidity and outrageousness! It can't get dumber than this really!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyu Ngoda muoneeni tu huruma. Anahitaji professional psychiatric help.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Oct 10, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Serikali ya JK ilionekana na nguvu mwanzoni mwa utawala wake kwa sababu ya fis*** Lowasa! Alipoondoka ndio alipojiexpose vizuri! Mimi sina tatizo na tabasamu ila the guy is not serious in anything, just travelling around the world to wake up the international fisadis (in the name of wawekezaji) to come and finish what was left by others! Yet the President doesn't know why the country is poor and claims so! How then will fight poverty? This man is supposed to vacate the office even before January, 2010, he has overstayed in power really!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Hii dhambi nani amembatiza Kikwete? Au anayeandika ndio anataka leo kumbatiza? Hakuna shida JK kuwa mcheshi wala mtu wa karibu na wanyonge. Shida ipo kama atashindwa kuwa kiongozi imara na mtu mwenye uwezo wa kuyakabili matatizo yaliyopo bila kujifungia chumbani.Hii inyoitwa dhambi naona huu ni utunzi mzuri wa mwenye thread maana watu wengi hawamchukii JK. Wanachukia kuona mambo yanasuasua kama hakuna kiongozi na hadithi tele zisizo na vitendo
   
 12. M

  Merchant Member

  #12
  Oct 10, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zawadi,
  Politics za Tanzania kwa mtazamo wako sasa hivi ni kama Simba na Yanga, nani ni zaidi ya yupi, na tu kwa sababu tu wewe upo-affiliated with them on certain attittude then they are right. Maana huwezi kumconvince mwana Simba au Yanga kuwa kushindwa ni halali.

  Accept one thing, first a President is a mirror of the Nation. A president is the most top of our Nation decision making. We expect a lot from him or her. Kizuri hujiuuza na kibaya hujitembeza. Ati kama in a real sense Kikwete has been doing a good job and we are seeing it why somebody will complain? These complaints are coming because he promised too much than what he could accomplish. People have become poorer, no jobs and no job creation. No export growth (Don't bring those Data From CIA.gov). The terms of trade and all economic infrastructures are still held by a few and those who are not indigenous or foreigners. Even the government is not benefitting from those dealings let alone the people of this Nation. The gap between the haves and the havenots is growing. The elders who have retired from their jobs are still not getting their wages and their terminal benefits just to mention these.

  The fundamental and backbone of any nation is Agriculture, we still see that agriculture has been the same and not revamped, already 5 years gone (You will bring your Tobbaco datas). Kwenye kilimo ndiyo kwenye 80% ya waTanzania.

  Frankly speaking the honeymoon for Mr. Kikwete is gone, is already 5 years and we have to make sure that he explains to us who he has done. Usilete mambo ya Simba na Yangan ati kusema Mkapa alifanya nini au Nyerere alifanya nini. WE are living now and for the future, we must correct who our future to come.

  He is the only sitting President who has spoken bluntly that he doesn't know why Tanzania is poor. He is still going on and denying that there was no foul on Richmond and Kagoda. I wouldn't expect praising Dr. Slaa and ask Mr. Kikwete where is our money stolen from our banks, the money siphoned from the Richmond scandal etc only beacsue he thinks or he belives different from you.

  Tabasam la kikwete is only his physical appearance and attraction which attract some people to him. But in the real sense we need to tell him why he wants the second term; can he show us what he achieved in his 5 years?
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Zawadi hapa hoja zako ume generalize tena bila kutoa ushahidi. Umesema "Watanzania" ila hauja sema kama unamaanisha Watanzania wote milioni 40 au asilimia kubwa ya Watanzania na umepataje takwimu hiyo. Pia umesema Watanzania nawakimbilia kutumia tabasamu la Kikwete kama hoja sasa can you quote even one Tanzania on that? Na can you show that that person is using that as a means to attack Kikwete?


  Sasa hapa unakua very unscientific. Are you trying to say kuwa na tabasamu la kila wajati ina uhusiano wowote na mtu kuwa kiongozi bora? Na je una ushahidi kuwa Clinton na Blair ndiyo viongozi wanaoongoza kwa kutabasamu? Je unajua hata George W. Bush alikua ana tabasamu na kucheka cheka mara kwa mara? Hakuna uhusiano wowote kati ya tabasamu na kua kiongozi mzuri. Na umesema Clinton na Blair wamekuza uchumi wa nchi zao je Kikwete kakuzi uchumi wa Tanzania? Hapa toa ushahidi wa kitakwimu. Tanzania ilikua na hali gani ya kiuchumi 2005 wakati JK anaingia na sasa hivi. Hatutaki maneno tupu ya kihisia.

  Nguvu au udhaifu wa serikali yoyote inapimwa na uwezo wake wa kufanya yale iliyo ahidi ili kupata kura za wananchi wetu. Pia ina pimwa na uwezo wa serikali kutekeleza shughuli mbali mbali za serikali. Naomba uresearch kitu kinaitwa capacity kwenye comperative politics uta nielewa zaidi.

  Mbona Unguja na Pemba mpaka leo wana lalamika kuonewa na kulalamika kuwa polisi wana tumika? Ushahidi wa huu upo kutoka kwa thread za member mmoja hapa JF. Kama una taka ushahidi nita kutafutia. Je kama unayo sema ni kweli Maalim Seif Sharif Hamad bado ana lalamika nini?

  Demokrasia siyo uhuru wa kuongea tu. Kama unaweza kuongea na hakuna kitu kinacho fanyika kuna faidia gani? Uhuru wa kuongea ume fumbua mambo mengi kuhusu ufisadi je niambie kimefanyika nini cha maana mpaka leo hii kuhusu mafisadi? Na hata huyo Jk kaingia kwa pesa za mafisadi kama Lowassa. Na je Lowassa kapewa adhabu gani? Siyo demokrasia ya kweli kama tunacho ongea kina ingia kwenye sikio moja la serikali na kutokea sikio la pili.

  Sasa hapa una tudanganya Zawadi. Kwa nini una pangia upinzani agenda? Wamekuambia hizo ndiyo sababu watakazo tumia. Na mwanzo wa paragraph unaanza na "kama kweli" which means hata wewe mwenyewe hauna uhakika bali una kisia.

  When it's all said and done Jakaya Mrisho Kikwete......raisi wa awamu ya nne ya Jamhuru wa Muungano wa Tanzania.......ata hukumiwa kutokana na ahadi zake na mafanikio yake. Nakushauri Zawadi anzisha thread inayo orodhesha ahadi za Kikwete 2005 na kutoa mifano ya kiushahidi ya wapi kafanikiwa na wapi haja fanikiwa.

  I love Kikwete. He has a great personality. But I want to judge him on his leadership and this is how I would judge him.

  1.Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Je kafanikisho hilo kwa kiasi gani?

  2.Aliahidi ajira milioni moja. Je ni ajira ngapi zilizo tokana directly au indirectly na sera za serikali yake?

  3.Mafisai kawa shughulikiaje? Hasa wale walio kuwa chini yake kama waziri mkuu wa zamani na baadhi ya mawaziri ambao ali wateua mwenyewe?

  4.Je safari zake za nje kila wakati zimeleta mafanikio yapi?

  Na mifano kama hii. Kuwa objective. Asante....
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na Zawadi katoa hoja gani zaidi ya kuongelea personality ya Kikwete? Kama muanzisha thread ana toa hoja kwa kuangalia personality basi haina budi na yeye kujibiwa hivyo hivyo.
   
 15. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kwanza ningekupongeza kwa kuvigusa vitu viwili ambavyo ndio muhimili wa Thread hii. Personality na utendaji Nafikiri kwenye hili la tabasam tupo pamoja nikinukuu pale ulipoandika: "Obama anatabasamu, Nyerere alikuwa anatabasamu na kuchekesha, watu wangemuita comedian , lakini wapi."

  Msukumo hasa ulionifanya kuandika Thread hii ni kuchoshwa na vyombo vya habari na baadhi ya wananchi kuchukua muda mwingi sana kulizungumzia tabasam la Kikwete kama upungufu mkubwa katika uongozi wake. Ni matumaini yangu kuwa katika siku zijazo hatutachanganya kati ya udhaifu (kama upo) na tabasam lake. Binafsi sipendi bosi wangu awe amenuna nyakati zote, ili nijue ndie Bosi mzuri. Kwa bahati mzuri Bosi wangu ni mcheshi na anatabasam zaidi ya Kikwete, lakini ni mchapaji kazi mzuri sana. Hii inanikumbusha wakati mgumu nilipokuwa sekondari, ambapo head master wa shule sikumuona kutabasam hata siku moja kwa kipindi cha miaka minne. Na kwa ukweli tulikuwa tukimuogopa kama simba. Hapana sipendi kukumbuka.

  Kuhusu utendaji, naona umeandika mengi sana. Naelewa hapa JF hampendi Takwimu, hivyo sitawachosha na Takwimu na badala yake tutazungumza lugha zetu za kawaida(nyingi, kubwa, ndogo, hakuna kitu n.k). Si Lugha ninazozipenda sana lakini ndio lugha zetu.

  Sijui kama upo makini pale unapoandika


  "Uhuru wa kujieleza ni silaha nyingine kali sana anayotumia JK, nimekueleza swala la ujinga, Kuwa watanzania huridhika kirahisi na kitu fulani

  Niambie nini kimefanyika baada ya uhuru wa kujieleza, ukijieleza basi ndiyo umemaliza? CCM wanajua watawapata watu kama nyie kirahisi."

  Hapa napata wasiwasi kama unamaanisha ulichokiandika. Kwasababu huko China maeneo kama haya yanafungiwa. Kumbuka Skandal ya Google na kutoa taarifa za siri na serikali ya China. Sitaki kujadili sana katika hili maana kila mmoja anaelewa maana na umuhimu wa uhuru wa kujieleza. Nchi nyingi hazifaidi matunda haya. Unaposema CCM inajua kuwa itatupata watu kama sisi kirahisi kwa kutumia uhuru wa kujieleza, hapa ndio sikuelewi kabisa. Kwasababu uhuru wa kujieleza unatunufaisha sote, mimi na wewe. Sasa mwenzangu hufurahii na hilo. Kwangu hiyo ni positive No 1, nafikiri itaniongezea hata umri kidogo.

  Nanukuu paleulipoandika kuwa "Nathibitishiwa kuwa JF haijakusaidia kukubadili mawazo, acha nikusaidie kidogo tena i, cha kufanya jikaze tu wakati unapigwa msasa" Ni kweli ndugu yangu kwa mawazo hayo, kuwa uhuru wa kujieleza hauna faida itakuwa vigumu JF kunibadili. Lakini siamini kama wana JF wote wanafikiri kama wewe.

  Kama nilivyoahidi kuwa nitajibu kama mtakavyo bila Takwimu:
  Kikwete kafanya nini mpaka achaguliwe: Kafanya mengi, Kashirikiana na Nyerere, Mwinyi na Mkapa kuleta umoja wa kitaifa, Kakuza Lugha ya kiswahili, Katoa ukabila na udini, kaleta amani, kasaidia kuleta uhuru Msumbiji,A Kusini, Zimbabwe n.k. Kashiriki katika kuleta mabadiliko toka chama kimoja mpaka vyama vingi kwa amani, na sasa hivi kaleta matumaini kwa wananchi na vyama vya upinzani. Na mengi tu, sitajaza huu ukurasa.

  Kilimo: kimekuwa na mazao mengi yamepatika na mwaka jana

  Baada ya miaka 50 tutakuwa na uchumi sawa na A. Kusini (Takwimu ninazo ila tunamkataba wa kuzungumza lugha za ki-JF)

  Hasifiwi na mawaziri wake kwa sababu kawatema marafiki zao kwa ulaji (Lowassa + walaji group).

  Ni mengi ya kuyataja, lakini napenda kukufungua macho kuwa hata huko mbeleni Raisi yeyote yule atakaye kuwa mtendaji mzuri hatapendwa na mawaziri wake. Hata waziri akiwa mtendaji mzuri hawezi kupendwa na mawaziri wenzake. Uliza kama Magufuli anapendwa na mawaziri wenzake, au jiulize ni nini kilimkuta Sokoine baada ya kufanya kazi kwa haki. Ili upendwe ni lazima uwe Bla Bla na kuficha siri za serikiali kwa wizi wote. Na hapo ndio utaelewa nini faida ya uhuru wa kujieleza.

  Wake up Waberoya!!!!!!!
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Oct 10, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,069
  Trophy Points: 280
  Zawadi Ngoda,

  ..labda nikupe mfano: mtu akiweza kununua suruali, shati na viatu, basi next time atataka anunue suti etc etc.

  ..wapiga kura nao ni hivyo hivyo. inawezekana walipomchagua JK walikuwa wana hamu ya kupata Raisi anayetabasamu kama JK.

  ..sasa wameshapata Raisi anayetabasamu mahitaji na matarajio mengine yanaanza ku-kick in. wataanza ku-demand barabara, maji, umeme, ajira, fursa za biashara etc etc.

  ..au, chukulia mfano wa harakati za serikali ya JK kujenga shule za sekondari kila kata. mwanzo wananchi walipokea mafanikio hayo kwa furaha kubwa sana na walimpongeza JK.

  ..sasa baada ya kupata shule za sekondari za kata, tusione ajabu wananchi wakianza ku-demand kwamba shule hizo sasa ziwe na waalimu waliofuzu, maabara, maktaba etc etc.

  ..tatizo la JK ni kushindwa ku-keep up na mahitaji na matarajio ya wananchi.

  ..utendaji wa JK ni kinyume kabisa na kauli mbiu ya kampeni yake ya uchaguzi. binafsi siridhishwi na kasi, ari, na msukumo ktk utekelezaji wa majukumu ya uongozi ya JK.

  NB:

  ..hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere analaumiwa kwa kushindwa kuviendesha viwanda vilivyojengwa wakati wa utawala wake.

  ..Mzee Mwinyi anapongezwa kwa kufungua milango ya biashara na shughuli za uchumi, lakini analaumiwa kwamba wakati wa utawala wake biashara haramu na ukwepaji kodi vilishamiri nchini.
   
 17. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kikwete anajitahidi lakini as long yeye ni Rais ni Public Good! kwahiyo habari ya kusemwa atasemwa sana ama kwa faida yake au kwa kumchukia tu hilo hawezi kukwepa; Aliandamwa Nyerere, Mkapa, Mwinyi who is he? lazima apate chake kwakuwa ni "PUBLIC GOOD"

  Public opinion inataka achukue hatua haraka haraka kuliko anavyofanya hasa kwa mafisadi na issues sensitive kama Mahakama ya Kadhi, Waraka na Mwongozo na kama hivyo..it seems the guy is very slow to comment ...kama ni style yake basi watu wengi wanadhani ni udhaifu....(might be wrong)

  Kuna tume nyingi sana zinafanya zinachunguza kitu kilekile kwa kutumia a meager public funds nafikiri wananchi wanataka jamaa aende direct to the point...sijui katiba na sheria za nchi zikoje kufanya hivyo
  So far mimi na nampa BIG UP to me it was an Historical moment kufikishiwa mafisdi mahakamani (Mramba -hata tukila majani ndege lazima tutunue kiburi...sasa anahangaika mahakamani, yona, mgonja na hata kum drop his friend lowassa that was BIG time in Tanzanian History.
  University enrollment imeongezeka kwa kiasi kikubwa so after some years tunaweza kuwa na wasomi wengi...Kaza buti JK..2010 itabidi ujibu msemo wa kasi mpya na ari mpya uliutumiaje? mbona uliuacha baada ya miaka minne?
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu nilipenda nikujibu kwa Takwimu, lakini safari hii nimepigwa marufuku. Soma #13 ..."(Don't bring those Data From CIA.gov)." Safari hii nitaheshimu maombi ya wasomaji, kwa vile najua hapa JF watu wanaogopa sana Takwimu.

  Lakini ukipenda angalia sehemu walioandika "compare" katika www.aneki.com. Utakuta takwimu nzuri kabisa lakini nakuhakikishia kuwa uchumi umepanda, nashindwa kujizuia nitakudojezea kidogo tu (GDP ni $1400) 2008.

  Kuhusu kuzungumziwa sana Tabasam kama udhaifu katika vyombo vya habari na kwa watanzania, hili naweza kukuletea ushahidi. Ushahidi ninao tena ukitaka hata hapa JF.

  Lawama Pemba, bado zipo wala haihitaji ushahidi. Napenda unielewe nilizungumzia kushushwa mabomu hata kupata wakimbizi. Nasisitiza kushushwa mabomu na kusababisha vifo vya watanzania ndani ya Tanzania wakiuawa na watanzania wenzao. Malalamiko hayako Pemba tu hata Mara, Mbeya n.k.

  Unaandika "Nguvu au udhaifu wa serikali yoyote inapimwa na uwezo wake wa kufanya yale iliyo ahidi ili kupata kura za wananchi wetu." Sijui ukweli wa maneno yako yanachukua takwimu zipi. Ninachoelewa mimi katika awamu zote 4, hakuna awamu iliyoahidi na kufanya angalau 40% ya mambo iliyoahidi. Tukianza na kipindi cha miezi 18 ya shida (Nyerere), tukaja kwenye fagio la chuma(Mwinyi), tukaingia kwenye muafaka (Mkapa) na sasa ni Maisha bora kwa wote. Sioni uhusiano wa ahadi na kuchaguliwa kwa Kiongozi. Tatizo ni kwamba Watanzania wanawaona wanasiasa wote kuwa ni waongo. Na ndio maana tafsiri rahisi ya siasa kwa mtanzania ni Uongo uliokomaa. Sidhani kama watanzania walio wengi wanaangalia ilani ya uchaguzi kama kigezo cha kumchagua kiongozi. Wao wanavipimo vyao vingine kabisa, ikiwa ni pamoja na matatizo sugu ya karibu yanayowakaribia.

  Kuhusu ajira, hapa usisema tafuta mwenyewe Hizo Takwimu. Maana ni nzuri mno, tena hapa nitakushika. Natamani kutoa takwimu lakini kwa leo lazima nijizuie. Nenda kwenye shirika la takwimu Tanzania (si bure, zinauzwa). Binafsi ninazo 2005- March 2009. Muombe kibali #13 ili nizimwage.
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Duh! Halafu unaweza kukuta Zawadi ni Kiongozi mkubwa tu ktk Serikali. Yaani Tabasamu Zuri linamfanya mtu awe Kiongozi Mzuri? Yaani Zawadi unakuja Kumdhalilisha Rais hapa jamvini kwamba kwa Tabasamu lake Zuri Ndege ya Uchumi wetu ina take Off? Mwenyewe unafikiri unamteteeeea kumbe unamdhalilisha
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naamini hujasoma story nzima au umeamua kupotasha kwa makusudi???go and read between the lines
   
Loading...