kyalankota
JF-Expert Member
- Jul 27, 2014
- 2,594
- 1,463
Alichokisema Bulaya ni kuwa "Nitagombea Jimbo la Bunda Mjini lakini sitogombea kwa tiketi ya CCM, sina ugomvi na CCM wamenilea na nimekulia huko, na kutogombea kwangu kupitia CCM kusihusishwe na mtu na nafasi ya Urais.
Ila nimelitumikia Taifa langu nikiwa CCM naona nitalitumikia Vizuri zaidi nikiwa kwingine. Kumbukeni chama ni njia ya kupita ila umuhimu wa kulijenga Taifa letu ni la watanzania wote bila kujali vyama vyetu. Mungu ibariki Tanzania"
Mbunge wa viti maalum ameamua kuitosa CCM, asema atarudi bungeni kivingine kwa sababu hawezi kuhonga. Rushwa ndani ya CCM ndo imemkimbiza sasa kuhamia upinzani. Afuata nyayo za Lembeli.
Source : gazeti Nipashe la leo
Kalibu dada nakukubali sana mungu akutie nguvu twende tumtoe mkoloni mweusi ccm
Kama ndivyo,thumb up!karibu dada yetu jasiri na mpiganaji,vua gamba uvae gwanda!Mbunge wa viti maalum ameamua kuitosa CCM, asema atarudi bungeni kivingine kwa sababu hawezi kuhonga.
Rushwa ndani ya CCM ndo imemkimbiza sasa kuhamia upinzani. Afuata nyayo za Lembeli.
Source: Nipashe
Kalibu ni aina ya pombe au ni kitu gani?